WAFANYABIASHARA 4 WA
BIASHARA YA MBAO MKOANI RUVUMA WAUNGA MKONO
SERIKALI KWA KUICHANGIA MBAO 350 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 4 KWA AJILI
YA UTENGENEZAJI WA MADAWATI
Mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya amewashukuru wafanya
biashara hao Asia Chakwela,Mussa
Mwingira Ticson Luvanda na Rajabu Mbaja na kusema suala la utengenezaji wa
Madawati ni la kila mmoja na siyo Serikali peke yake, Hivyo amewaomba wadau
wengine waige mfano huo.
Afisa wa Wakala wa Misitu Mkoa wa Ruvuma Manyisye Mpokigwa amesema kazi
kubwa kwake ni kuwahamasisha wafanya
Biashara za Mbao kuungana na Serikali ili kupunguza tatizo la uhaba wa Madawati.
Mwenyekiti wa Wafanya Biashara hao wanne Asia Chakwera amesema baada ya kutmbela Shul za Msingi mbili alipata uchungu kuona wanafunzi wakikaa chini ndipo alipowashauri wafanyabiashara wenzak kusaidia kutatua tatizo hilo
Wafanya Biashara wa
Mbao Mkoa wa Ruvuma wameWameunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr John Pombe Magufuli ya kuwataka wanafunzi wote ifikapo June 2016 wanafunzi
wote wawe wanakaa kwenye Madawati.
Wafanya Biashara za
Mbao wanne Mkoani Ruvuma wametoa Mbao zipatazo 350 zikiwa na Thamani ya Shilingi
Milioni 4.4 kwa ajili ya utengenezaji wa madawati wilaya ya Songea.
Juhudi za Utengenezaji wa Madawati wilaya ya Songea hivi
sasa unaenda kwa kasi karibu shule nyingi watoto wanakaa kwenye Madawati.
No comments:
Post a Comment