Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini wameahidi kutenga Bajeti kiasi cha sh. milioni 50.5 kwa ajili ya kuwezesha mikopo kwa wazee kupitia vikundi.
Wadau wa masuala ya wazee kutoka Halmashauri za wilaya ya Songea Vijijini, Songea Manispaa na Halmashauri ya Madaba wameamua kutosubiri Bajeti za serikali kuu katika kuwasaidia wazee bali wameanza kuwashughulikia kupitia vyanzo vya ndani na fedha zao za mifukoni kwa kuchangia mahitaji ya wazee wasiojiweza.
Wazee wa barabaza Huru la Wazee wa Manispaa ya Songea wameomba Jamii kutambua umuhimu wa wazee katika jamii zao wamesema wapo watu ambao bado wanawabeza wazee na kuwasingizia kujihusisha na imani za kishirikina.
Watumishi wa shirika la PADI wakifuatilia hoja za wakuu wa Idara katika kupanga maazimio ya namna watakavyoweza kuwasaidia wazee kwa kushirikiana na Shirika la PADI.
Afisa Biashara wa Manispaa ya Songea akielezea namna atakavyotumia mapato yatokanayo na Biashara katika kuhakikisha wananufaisha na wazee kupitia vikundi vya ujasiliamali.
Wakuu wa idara wa Manispaa ya Songea wakipanga mikakati ya kuwaingiza wazee katika Bajeti kutokana na Bajeti wanayoipata kwa kila idara. Wakuu hao wamejadili hayo wakiwa katika viwanja vya shirika la PADI Unangwa Manispaa ya Songea.
Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri 3 za wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma walipokutana na wazee na Viongozi wa Shirika la Kuhudumia wazee la Padi na kuweka maazimio ya kuwasaidia wazee ikiwemo kutunga sheria ndogo ndogo katika kila Halmashauri za kuwalinda wazee.
Halmashauri ya Madaba imetenga Kiasi cha Shilingi Milioni 50,231,500 katika Bajeti ya 2016/2017 kwa ajili ya huduma za wazee ikiwemo na kuwatengenezea vitambulisho vya matibabu. |
No comments:
Post a Comment