Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya ambaye aliona taarifa
kwenye Vyombo vya Habari kuhusu kutelekezwa kwa Shule ya Ngunguti iliyo katika
Tarafa ya Muhukuru Songea Vijijini , amekanusha kuwepo kwa Shule hiyo bali
kilichopo Wananchi wanahitaji watoto wao wapate Elimu, Serikali itafanya kila
linalowezekana ili Shule iweze kusajiliwa
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngunguti amesema tayari wameweza
kuandikisha watoto 30 na kumtafuta Mwalimu ambaye hana taaluma ya uwalimu ili
aweze kuwafundisha watoto hao baada ya watoto kukosa Elimu kwa kipindi cha
miaka saba kwa sababu ya shule hiyo kuto kusajiliwa.
Moja ya changa moto inayo ikabili shule hii ya ngunguti iliyo kilometa 176 ina ukosefu wa madawati pamoja na ubao wa kuandikia watoto kama unavyo waona wana kaa chini hawana sare, Mkuu wa wilaya ya songea Beson Mpesya ameahidi kuipa usajili pamoja na kuwa tafutia mwalimu wa muda wakati taratibu za usajili zikifanyika
Afisa Elimu Msingi wilaya ya Songea Vijijini Mtani Kameka
amesema wilaya ya songea vijijini haina
shule inayo itwa ngunguti ila wanachi wamewakusanya watoto pamoja ili waweze
kupata elimu hivyo gazeti { la uhuru
}ililo andika habari hizo siyo kweli
Wananchi wa kitongoji cha Ngunguti songea vijijini kilometa 176 wakitoa mawazo yao kwa vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya kitongoji hicho changamoto wanazo kabiliana nazo kuhusu Elimu na Afya ,Shule haina choo .uwanja wa michezo.hata walimu wenye taluma Serekari imeahidi kutatua matatizo hayo
Wananchi wa Kijiji cha ngunguti Kitongoji cha Ngunguti
kijiji cha Muhukuru barabarani Songea vijijini wameiomba Serikali kuwasaidia
Usajili wa Shule pamoja na kuchangia
vifaa vya ujenzi ili waweze kumalizia
Shule waliyoanza kuijenga.
Kijiji cha Muhukuru Barabarani kina Vitongoji 4 vyenye kaya
375 ambapo Kijiji hicho ni cha wakulima wakulima waliohamia kutoka wilaya ya
Mbinga kwa kufuata rutuba kwa ajili ya Kilimo.
hII NI SHULE YA NGUNGUTI SONGEA VIJIJINI AMBAYO INA TEGEMEA NGUVU YA WAZAZI MPAKA SASA HAIJA SAJILIWA INA DAIWA KUWA NA WANAFUNZI 80 LAKINI WALIO JISAJILI WAPO 30
No comments:
Post a Comment