Mahakama Kuu Kanda ya Songea imetoa hukumu Kesi ya
Madai ya Gharama za Kesi ya Uchaguzi dhidi ya Joseph Fyime na Leonidas Gama ya
Madai ya Shilingi Milioni `13 aliyotakiwa kulipwa Leonidas Gama.
Msajili wa Mahakama kuu Kanda ya Songea George Herbert
amesema ametoa hukumu hiyo baada ya kuangalia hali halisi ya uendeshaji wa Kesi
ya Madai dhidi ya ndugu Joseph Fyime ambaye alikuwa akidaiwa alipe gharama ya
shilingi Milioni 13,000,000/kwa ajili ya garama za uchaguzi lakini mahakama kuu
imemwamuru joseph Fyime wa chadema kulipa shilingi milioni 12,000,000./= kukidhi
garama hizo
MAHAKAMA KUU KANDA YA SONGEA IMEMALIZA KESI DHIDI YA
ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA NA ALIYESHINDA UBUNGE JIMBO LA
SONGEA KWA KUMUAMURU MGOMBEA WA CHADEMA ALIPE GHARAMA ZA UENDESHAJI WA KESI YA
UCHAGUZI. TS. 12,395,000/=
Mgombea Ubunge kupitia Chama cha CHADEMA Joseph Fuime
amesema kutokana na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Songea ya kumtaka alipe Milioni 12,395,000
ameipokea na anaangalia jinsi ya kuitekeleza kama
ataweza kukata rufaa.
Mgombea Ubunge kupitia CHADEMA Joseph Fuime amesema Chama
chake cha CHADEMA toka Kesi imeanza mpaka imeisha kimeshindwa kutoa msaada na
hali hiyo siyo yeye tu hata wengine walio na kesi za uchaguzi hakuna
aliyesaidiwa hiyo ni kukatisha Tamaa wanachama.
No comments:
Post a Comment