Mzee Daudi Mpangala aliyezaliwa miaka 75 iliyopita ameweza kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha yake na kuweza kuzishinda ikiwemo na kuweza kuimili kuishi maisha ya peke yake bila mke kwa muda wa miaka 34 jambo ambalo si rahisi kwa wanaume wengi.
Katika Maisha yake Mzee Mpangala alisoma na kufanya kazi katika sekta ya Elimu idara mbalimbali mpaka sasa ambapo alistahafu akiwa na cheo cha Afisa Elimu Mkoa wadhifa aliokuwa nao kwa muda wa mikaka 6. Pichani ni Padre Simon Ndunguru na wahudumu walioongoza ibada ya jubilei nyumbani kwake Bombambili Mtaa wa Muungano manispaa ya Songea.
Wanakwaya wa kanisa parokia ya bombambili Kigango cha Bombambili wakishangilia kwa nyimbo jubilei ya Mzee Mpangala katika ibada ya jubilei hiyo iliyofanyika Nyumbani kwa Mzee Mpangala.
Padre Simon ndunguru amewaasa wakristu kuishi maisha ya mfano wa kristo kwa kufuata maandiko kama alivyofanya Mzee Mpangala ni kidhibiti kuwa anafuata maandiko kuwa pamoja na changamoto za migogoro ya ndoa inayojitokeza katika maisha lakini haipaswi kuwa sababu ya kutengana hivyo amesema Mpangala awe mfano kwa wengine.
Padre Ndunguru alitumia jubilei hiyo kuwakumbusha wakristo wengine kujitathmini kama wana mkiri kristu kwa kiasi gani na kama wanakumbuka kushukuru kwa mema wanayojaliwa ama wanamkumbuka pale wanapopatwa na matatizo kwa kumuomba awaondolee matatizo. Ni swali linalotugusa wote si muislamu au mkristu.
Padere Simon Ndunguru akiongoza Misa ya jubilei ya Miaka 75 ya kuzaliwa kwa Mzee Daud Mpangala Nyumbanik kwake Bombambili Manispaa ya Songea.
Katika maisha ya Elimu Mzee mpangala ameiomba Serikali kuangalia upya mitaala ya Edlimu amesema zamani kulikuwa na elimu ya kujitegemea inayomjenga mwanafunzi kumudu kufanya shughuli binafsi badala ya kutegemea kusoma ili apate Ajira Serikalini.
Pia ameshauri katika kuboresha kiwango cha Elimu nchini nik vema ungeongezwa muda wa mafunzo ya walimu na wakufunzi ili kupata walimu wenye tija pia kuangalia suala la maadili kuanzia kwa waalimu mpaka wanafunzi ili kupunguza kizazi chenye mmomonyoko wa maadili ambacho kitakuwa ni hasara kwa taifa tutakosa viongozi waadilifu.
Mzee Mpangalka ameendelea kusema hata kama Elimu itakuwa juu pasipo na maadilik mazuri matokeo yake tunazalisha viongozi wasio na hofu ya mungu wenye kujilimbikizia mali, ufisadi na mambo mengine ambayo ni kinyume na hnaki.
Ndugu msomaji tunapaswa kujifunza kuwa kila jambo linatokana na mungu kinachotakiwa ni kujiamini na kumtegemea Mungu awe kiongozi wa Maisha yetu ya Dunia.
No comments:
Post a Comment