Katibu Mkuu wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma Daktari Lauren Ndumbaro amesema shabaha ya
Serikali kuendesha Zoezi hili ni kutaka kuwadhibiti wale ambao wanapokea
mishahara bila kufanya kazi na kujenga Muundo bora wa uongozi katika Serikali
hii ya awamu ya tano.
Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma Daktari Lauren Ndumbaro amewatoa wasiwasi
watumishi kuwa kufanyika kwa mazoezi hili si kwamba watumishi watapoteza haki zao laa,
baada ya uhakiki kukamilika mambo yatarudi kama
kawaida.
Serikali imeamua kuhairisha Ajira Mpya, Ajira mbadala,
Upandishaji wa Vyeo pamoja na Marekebisho ya nyongeza za Mishahara mpaka zoezi
la Uhakiki wa Watumishi hewa litakapokamilika.
Katibu Mkuu wa Utawala
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Daktari
Lauren Ndumbaro ameyasema hayo wakati akizungumza na Watusmishi wa Halmashauri
tatu za wilaya ya Songea kuhusu zoezi la uhakiki wa watumishi Hewa.
Watumishi wa Umma katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wameomba Serikali kuangalia Upya kwani wapo watumishi ambao wanafanya kazi
Serikalini wanafikia miaka miwili bila kupata mishahara na wengine wanafikia
mwaka hawajapandishwa vyeo wala kuongezwa mishahara baada ya kusoma.
Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma Daktari Lauren
Ndumbaro amewataka watumishi wote wanaoidai Serikali katika nyanja mbalimbali
kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiendelea
kufanyia kazi Masuala yao.
No comments:
Post a Comment