Pamoja na kushiriki kikao cha Halashauri kuu ya CCM wilaya Mhandisi Manyanya amewataka wazazi kushirikiana na Serikali katika kuinua kiwango cha Elimu kwa Watoto kwa kuhakikisha watoto wanakwenda shule na kuwaboreshea mahitaji yao ya msingi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa chakula cha mchana mashuleni, Amesema ni fedhea kubwa kuona Jimbo lake linakuwa na kiwango cha chini cha Elimu.
Katika Kikao hicho cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Nyasa Makatibu wa Kata wameomba kufikiriwa kuongezwa posho wanazolipwa kwa mwezi ili iwasaidie kutekeleza majukumu kwa wakati pale wanapohitajika kupeleka taarifa CCM Wilaya kwa kuwa Jiografia ya Wilaya ya nyasa baadhi ya kata ziko mbali na makao makuu ya chama zaidi ya km 100 kwa posho ya sh 10,000 kwa mwezi ni kiasi kidogo.
Wamesema inapotokea kuna taarifa zinatakiwa kuziwasilisha Ofisi za chama wilaya Makatibu wanaanza kufikiria jinsi ya kuzifikisha kwa kuwa wanaitaji nauli zaidi ya sh 20,000 kwa kila safari na ni lazima watumie siku mbili jambo ambalo huwapelekea wakati mwingine kutuma taarifa hizo kwa njia ya simu.
Aidha Makatibu na wenyeviti wa Kata Vijiji na Matawi wametakiwa kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya chama na siyo viongozi kuanza kulalamika.
Mhandisi Stella Martini Manyanya anaona fahari kuthamini tamaduni za asili ikiwa ni pamoja na chakula cha asili, Pichani ni Naibu Waziri wa Elimu akichukua chakula cha Ugali wa Muhogo kwa dagaa Nyasa kilichoandaliwa katika Hoteli ya kiasili ya Bio Camp iliyopo wilayani Nyasa, kushoto ni waandishi wa Habari wa Chanel Ten na TBC wakiwa wameambatana na Naibu waziri wa Elimu.
Akioongea kuhusu usalama wa majini kwa wananchi wa wilaya ya Nyasa Mhandisi Manyanya amesema anatamani kuona ulinzi wa watu wanaotumia ziwa Nyasa kusafiri au shughuli za uvuvi ukiimarishwa kwa kutumia njia wanayoitumia wataalamu wa Umeme katika kukabiliana na hitilafu zinapojitokeza kwa kutega baadhi ya maeneo na wataalamu kufuatilia watu wanaopanda kwenye mitambo kwa kutumia mawasilikano ambayo hutegwa ktk vituo mbalimbali ili kufuatilia usalama wa watumiaji wa umeme na mafundi.
Mhandisi Stella Manyanya anasema ni vema tuwe na tabia ya kuvithamini vya kwetu, ameomba wazawa wa Mwambao wa Ziwa Nyasa kuwekeza katika rasilimali zetu kuliko za kigeni ziko fursa nyingi zilizopo wilaya ya Nyasa ambazo maeneo mengine hazipatikani vikitumika vizuri vitasaidia katika kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya ya Nyasa na Tanzania kwa ujumla .
Mtanzania anayeishi Ujerumani mzaliwa wa wilaya ya Nyasa ambaye ameamua kuendeleza nyumbani Mr Chengula amewaasa wananchi wa Tanzania kufanya shughuli za Maendeleo kwa kutumia fursa zilizopo Nchini na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada za kuhakikisha Tanzania inakuwa Nchi yenye uchumi wa kati kwa kufanya kazi. Pia amesema Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania wasisahau kuthamini nyumbani kama ambavyo yeye anafanya ingawa amekuwa Ujerumani kwa miaka 25 lakini anaona fahari kuwekeza nyumbani.hamasisha maendeleo kupitia sera yake ya Hapa Kazi tu amesema wenzetu wanathamini kufanya kazi.
Mhandisi Stella Manyanya akiwa katika ufukwe wa Ziwa Nyasa na Mwenyeji wake Mr Chengula ambaye anaishi Ujerumani. Mhandisi Manyanya amemuomba anapokuwa Ujerumani kutangaza fursa zinazopatikana mwambao wa Ziwa Nyasa na Tanzania kwa ujumla, pia kukitangaza Kiswahili ili kiwe no moja kuliko kuenzi lugha za kigeni na kusahau nyumbani.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho amewataka wanachaa wa Chaa cha mapinduzi kuzingatia Matumizi ya Mali za Chama. Amesema kwa yeyote atakayebainika kuharibu mali za chama ama kuzitumia kwa kujinufaisha chama hakitasita kumchukulia hatua.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho na Mwandishi wa Chanel Ten Marietha Msembele juu ya kuimarisha Jumuia za Chama katika wilaya ya Nyasa ili ziweze kujitegemea.
Mhandisi Manyanya amesema sasa ni wakati wa kuhakikisha kila kata inakuwa na mradi wa Chama ambao utasimamiwa ipasavyo na kuwezesha chama kujiendesha badala ya kusubiri wakati wa chaguzi.
Mwandishi wa habari Marietha Msembele akiongea na Naibu waziri wa Elimu kukuhu Mikakati iliyopo katika kuendeleza Elimu wilaya ya Nyasa. Naibu Waziri amesema kwa sasa wanaikuza Shule ya Mbamba Bay High School ili iwe shule ya Mfano nyumbani kwa Naibu waziri wa Elimu ambayo inaboreshewa miundo mbinu na vitabu vya kutosha na mazingira bora ya kujisomea wakati jitihada za kuendeleza shule zingine zikiendelea.
Wilaya ya Nyasa yenye vijiji 84 ina fursa nyingi ambazo zinahitaji uwekezaji
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba ameomba ushirikiano kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa katika kujiletea Maendeleo.
Fursa zilizopo wilaya ya Nyasa ni pamoja na ufukwe nzuri kaa inavyoonekana pichani.
Hizo ni nyumba zinazopatikana katika Hoteli ya Bio Camp ambayo ni ya asili iliyopo wilaya ya Nyasa koani Ruvuma. Ni ufukweni mwa Ziwa Nyasa pana upepo mwanana na hali nzuri ya hewa ukihitaji kutembelea mazingira ya ziwani usafiri wa Boti unapatikana pia vinywaji na chakula cha asili vinapatikana BIO CAMP.
Madiwani na Viongozi wa CCM Kata za Wilaya ya Nyasa wakiwa katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Nyasa.