Maafisa Wanyamapori wa Pori la Akiba Kanda ya Kusini Kituo cha Kalulu wakiwa katika ukakamavu ikiwa ni kiashiria kuwa wako imara kwa ulinzi.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera alipotembelea Kituo cha Hifadhi ya Seluu Kanda ya Kusini Ikolojia ya Kalulu na kusalimiana na wanyama pori mara baada ya kuangalia ashamba yaliyovamiwa na Tembo wa hifadhi hiyo na kuharibu Mazao ya Wananchi wa Kijiji cha Rahaleo.
Askari wa Wanyama Pori ikolojia ya Kalulu wameseama changamoto inayowakabili katika kuwadhibiti Tembo wasivamie mashamba na Makazi ya watu ni pamoja na wananchi kutotoa taarifa mapema pindi Tembo wanapovamia katika maeneo yao badala yake hutoa taarifa wakati tayari uharibifu mkubwa umetokea.
Hilo ni Moja kati ya Mashamba yaliyovamiwa na Tembo na kula mazao ya shamba katika Kijiji cha Rahaleo. kutokana na uvamizi huo uliopelekea hasara kuharibu kwa mazao ya mahindi, mbaazi, vitunguu na mihogo kwenye mashamba tofauti ulimsukua Mkuu wa wilaya ya Tunduru kutembelea eneo la tukio na kuona hali halisi wakati taratibu za uthamini wa malipo ya kifuta jasho ukiendelea.
Katika Ziara hiyo Pia Mkuu wa Wilaya aliweza kutebelea Mradi wa Ufyatuzi wa Tofari kwa ajili ya Benki tofari zitakazosaidia ujenzi wa Madarasa na Vyoo vya Shule katika Shule ya Msingi Kalulu na kukuta nguvu kazi ikiwa ndogo ambapo aliweza kubaini wanaofyatua tofari hizo ni vibarua jambo amb alo hakuridhika nalo na kutilia shaka kama zoezi hilo litakamilika ndani ya mwezi mmoja kadiri ya agizo la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Pamoja na changamoto ya wanyama wa Tembo kuvamia mashamba pia wananchi wamemuomba mkuu wa wilaya kufuatilia upatikanaji wa kifuta machozi kwa wananchi watatu ambao waliuwawa na Tembo licha ya kuwa hatua zote zilizoelekezwa na Serikali kuzifuata zilifuatwa lakini mpaka leo ndugu hawafahamu hatima yake.
Afisa wanyamapori wa wilaya ya Tunduru Peter Chrispin aesema changaoto inayowakuta ni jiografia ya Eneo la Kalulu imekaa vibaya wananchi wanalima katika Mabonde ambamo napakana na Misitu minene hivyo Askari wanapofukuza Tembo wanaingia msituni lakini kadiri wanavyotembea hujikuta wameingia tena kwenye mashamba ya wananchi na kula mazao. Pia amesema wananchi wanapaswa kushirikiana na Askari wanyama pori katika ulinzi kwa kua Wanyama ni maliasili ya Taifa na si wa Askari kama wananchi wanavyotafsiri.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kalulu walipotembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru wamemmuomba kusimamia ujenzi wa madarasa mawili ambayo yanapungua kwa idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hapo.
Waalimu wa Shule ya Msingi Rahaleo wamemueleza Mkuu wa wilaya ya Tunduru kuwa wanakabiliwa na upungufu wa waalimu 5 waesema ahitaji ni walimu 13 waliopo ni 8.
Mkuu wa Wilaya ya
Tunduru Juma Homera amewataka Wananchi wa Kijiji cha Rahaleo Kata ya Kalulu wilaya
ya Tunduru kuwa na subira wakati
Serikali ikifanya Taratibu za kifuta machozi kwa wananchi waliopatwa na maafa
kwa kuharibiwa mazao yao na Tembo.
Wananchi wa Kijiji cha Rahaleo wamesema Janga lililowakumba kwa sasa wamekosa chakula na watashindwa kutoa huduma za kibinadamu ikiwa
ni pamoja na kuwasomesha watoto
Wanachi wameiomba Serikali kubuni mbinu zingine za kuwafukuza Tembo kwa kuwa Tembo hao sasa hata wakisikia milio ya Risasi hawaogopi.
Wananchi wa Kijiji cha Rahaleo wilayani Tunduru wameiomba
Serikali kuwadhibiti Tembo Kwa kuongeza
Asikari wa wanyama Pori idadi iliyopo inaonyesha kuwa ni ndogo kuliko mahitaji .
Mkuu wa Kanda ya Kusini Pori la Akiba la SELUU Ikolojia ya Kalulu Izack Boizai amesema changamoto inayowakabili katika kanda yao ni upungufu wa watuishi mahitaji ni watumishi 80 waliopo ni watumishi 64 katika eneo lenye ukubwa wa Km 6019, Amesema licha ya uchache wao wanajitahidi kufanya kazi usiku na mchana ya kulinda raia na mali zao dhidi ya Tembo licha ya hatari ya kufanya kazi usiku wa maanane.
Wanafunzi wa shule ya msingi Rahaleo wakifuraia ujio wa kuu wa wilaya ya Tunduru
Licha ya changamoto ya Maafa yaliyotokana na Uharibifu wa Tembo Wananchi wa Kijiji cha Rahaleo wamesema wanakabiliwa na changamoto ya wahudumu wa afya katika zahanati yao.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru pia amepiga marufuku wanafunzi kupewa kazi ya kuuza mbogamboga ama kukata kuni badala yake wasome na shughuli za kazi za nje zifanywe na wazazi.
No comments:
Post a Comment