MKUU WA MKOA WA RUVUMA AMEFANYA ZIARA
YA KUSHTUKIZA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA RUVUMA NA KUBAINI CHANGAMOTO
MBALIMBALI IKIWEMO UKOSEFU VIFAA TIBA IKIWEMO GLOVES, NYUZI NA DAWA ZA KUTULIZA
MAUMIVU.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith
Satano Mahenge ameutaka Uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kuwajengea Jiko wauguzi wa Nje na kutatua
Changamoto ya ukosefu wa nyuzi za
kushunea kwenye upasuaji.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge
ameyasema hayo katika ziara ya kushitukiza katika Hospitali ya Mkoa na kukuta
kuna choo kimoja tu kinachotumiwa na watu wasiopungua 250 .
Wauguzi wa
wagonjwa wameulalamikia Uongozi wa Hospitali ya Rufaa kwa kukosa vitu
vidogovidogo na kuwalazimu kwenda kununua nje, pamoja na kukosa sehemu ya
kupikia, wamesema kwa sasa wanapikia nje.
wauguzi kutoka maeneo mbalimbali katika mkoa wa ruvuma |
Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma Dr. Binilith Satano Mahenge amesema changamoto ndogo ndogo za kukosa
vyoo, ukosefu wa Gloves na nyuzi katika hospitali kunaweza kuifanya Serikali
iliyopo Madarakani ikashindwa kuaminika
na wananchi Ni juu ya Uongozi wa Hospitali kufanya Ziara katika vitengo
mbalimbali kubaini changamoto za
Hospitali.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma Dr
Philis Nyimbi amesema ukosefu wa Vifaa katika Hospitali hiyo inatokana na msongamano
wa wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali
Katika Ziara hiyo ya kushtukiza Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Dr. Mahenge amebaini ukosefu wa
sehemu ya kupikia, ukosefu wa dawa za
Maumivu na uharibifu wa Mashine za Utra Saund ambazo mpaka sasa zinatimiza miaka 2 bila kutengenezwa.
Mkuu wa Mkoa Dr Binilith Satano Mahenga akitoa agizo la kuwa jengea banda la kupikia kwa wauguzi wa nje
Msafara wa waganga wakiwa katika ziara ya kusutukiza ya mkuu wa mkoa ambayo ziara hiyo ili baini changamoto za kuto kuwa na vyoo.dawa za m,aumivu na baadhi ya Mashine kuharibika
Wafanyakazi wa Hospitali wakisikiliza kwa makini maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuhusu jinsi ya kuweza kutatua matatizo ya Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Damas Kayera akipokea Maagizo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Satano Mahenge juu ya ujenzi wa vyoo vya wauguzi wa nje pamoja na kujenga banda la kupikia
katibu wa hospitali akieleza kuhusu damu ya akiba katika hosipatali ya Mkoa wa Ruvuma na kusema damu ya akiba iliyopo ni yuniti kumi tu ukilinganisha na mahitaji yanayo takiwa Hospitali ya Mkoa kwa siku hutumia yuniti kumi za Damu
No comments:
Post a Comment