Wanachama wa Sacoss
ya Walimu Manispaa ya Songea yenye Wanachama 320 imeweza kuwakopesha wanachama
kiasi cha Shilingi Bilioni 3,931,780,000/
Mwenyekiti wa Sacoss ya Walimu Manispaa ya Songea Antony Mahundi amesema Saccos ya Walimu imeweza kupata faida kutokana na Wanachama wake kukopa na kurudisha mikopo kwa wakati. Jumla ya Shilingi Milioni 14 na laki 6 imepatikana na kuweza kuendesha Mkutano Mkuu bila kukopa mahali
Mgeni rasmi
Godrey Majuto akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea katika mkutano huo
wa chama cha kuweka na kukopa cha manispaa ya songea amewataka viongozi kutoa
elimu kwa wanachama wapya ili kuongeza Idadi ya wanachama na huduma za kiuchumi
ambazo zitawawezesha kujikwamua katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Mwenyekiti wa
Chama cha Akiba na Mikopo Sacos ya Walimu wa Manispaa ya Songea Antony Mahundi
amesema katik kutafuta washindi waliongoza kurejesha mikopo kwa wakati jumla ya
wanachama 7 waliweza kurejesha mikopo kwa wakati ambao walishindanishwa na
kupatikana washindi watatu walifanya vizuri zaidi.
Katibu wa
Chama cha kuweka na kukopa cha walimu wa Manispaa ya Songea Gebhard Nyoni akielezea
hali ya mapato na matumizi yaliyopatikana katika chama hicho kwa mwaka
2016 amesema katika kipindi cha January hadi Oktoba Chama kimeweza
kukusanya kiasi cha Tsh. 60,886,811.38 na kutumia kiasi cha shilingi 46,642,959.10
Amesema
Makusanyo hayo yamepatikana kutokana na faida ya mikopo shilingi 46,684,692.64,
viingilio vya Wanachama 100,000.00,makusanyo toka uwekezaji Tsh, 13,816,800.00
na Mapato mengine ikiwa ni Tsh 285,318.00.
Wanachama
waliokopeshwa na kuweza kurudisha kwa wakati ambao walioshindanishwa na
kushinda 3 wamesema mikopo imeweza kuwasaidia kusomesha watoto hadi chuo kikuu
. Sacoss ya Walimu wa Manispaa ya Songea pia imeweza kutoa rambirambi kwa
wafiwa kiasi cha shilingi Milioni 6,300,000 kati ya shilingi 24,678,328.50 zilizotengwa.
No comments:
Post a Comment