Katibu wa Naibu waziri wa Elimu sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Yonafika Mzungu akishuhudia uzuri wa Ziwa Nyasa na maajabu yake ikiwemo na vivutio vyenye mandhari nzuri alipokuwa ziara katika Ziwa Nyasa na Naibu waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya.
Naibu waziri wa
elimu,sayansi,Teknolojia, na Mafunzo ya ufundi Mhandisi Stella Manyanya amewaomba watanzania kushiriki katika
maadhimisho ya utalii yatakayo fanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu. Pichani ni watalii wa ndani wakiongozwa na Naibu waziri wa Elimu wakiwa katika Boti kutembelea visiwa mbalimba vinavyopatikana katika Ziwa Nyasa.
Mhandisi Stella Manyanya amesema ukitembelea mwambao wa ziwa Nyasa utaweza kufaidi vivutio vilivyoko katika ziwa nyasa na kupata vyakula vya asili ikiwemo samaki wanaopatikana katika Ziwa hilo wenye ladha safi ya asili.
Miongoi mwa vivutio vilivyopo katika visiwa vya ziwa nyasa ni pamoja na mawe mazuri na maeneo ambayo wavuvi hupata hifadhi pindi ziwa linapochafuka. Hicho ni kisiwa cha Lundo kilichopo Mbamba Baye kilomita chahe kutoka Nchi kavu.
Katibu Yonafika Mzungu kutoka Ofisi ya Naibu waziri wa Elimu akichukua kumbukumbu ya mambo yanayopatikana katika kisiwa cha Lundo Mbambabay wilayani Nyasa.
Pamoja na mazuri mengi yanayopatikana Ziwa Nyasa pia kuna dagaa wenye stata ya aina yake almaarufu Dagaa Nyasa kama wanavyoonekana pichani wakiwa wameandaliwa katika mitungo tayari kwa kukaushwa ili waliwe ukiwapata wakiwa wametengenezwa utapenda uwatumie mara kwa mara. kulia ni Naibu waziri Mhandisi Manyanya akishuhudia utajiri wa Mwambao wa Ziwa Nyasa.
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia, na Mafunzo ya
ufundi Mhandisi Stella Manyanya amesema
kuvijua vivutio vya mwambao wa ziwa nyasa ni fursa kwa wananchi kuzitambua rasilimali ambazo zinaweza kuwaingizia kipato.
Mhandisi Manyanya amesema utalii wa ndani
una faida na fahari kwa kuwea utaweza kujifunza mambo mbali mbali ya Historia ya Ziwa Nyasa ambayo yakitangazwa ipasavyo ni faida kwa wakazi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa, Mkoa na taifa kwa ujumla. Piachani ni Msafara wa Naibu Waziri wa Elimu wakielekea katika kisiwa cha Lundo kwa usafiri wa Boti.Ziara ya Naibu waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya katika kutembelea vivutio vilivyopo katika Ziwa nyasa ilipiga kambi katika Kisiwa cha Lundo kupata historia ya kisiwa hicho ambacho kilitumika kama makazi ya wagonjwa wa ukoma baada ya kutengwa na familia zao kutokana na ugonjwa.
Naibu waziri wa elimu,sayansi,Teknolojia, na Mafunzo ya
ufundi Mhandisi Stella Manyanya akielezea
kuhusu kisiwa cha lundo kilichopo wilaya ya nyasa amesema kisiwa hicho kinaitwa kisiwa cha lundo Mkombozi kutokana na kuwa kimbilio kwa wavuvi wanapopatwa na dhoruba wakiwa katika shughuli za uvuvi Ziwa linapochafuka
hujificha kisiwani hapo na kusalimika.
Hayo ni mawe ya aina yake yenye kuvutia ambayo unayapata katika Kisiwa cha Lundo katika ziwa Nyasa ambapo utaweza kupafikia kwa kutembea kwenye maji umbali usiopungua mwendo wa nusu saa kwa usafiri wa Boti au Mtumbwi kutoka Nchikavu . Ni mawe yenye nakshi ya rangi nyeupe pembeni utadhani yamepakwa rangi.
Naibu waziri wa
elimu,Sayansi,Teknolojia, na Mafunzo ya ufundi Mhandisi Stella Manyanya akiwa katika ziwa nyasa
kujionea vivutio vilivyopo kwenye ziwa hilo ikiwepo ufukwe, kisiwa cha lundo
ambacho wakati wa ukoloni kilitumika kama kambi ya wagonjwa ukoma.
Kutoka kushoto mwenye life jaket ni Meneja wa TANSCO Kanda ya Kusini Joyce Ngahyoma, katikati Mhandisi Stella Manyanya na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba wakifurahia mandhari nzuri ya Mwambao wa Ziwa Nyasa na hali safi ya hewa walipotembelea kisiwa cha Lundo katika Ziara ya Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na taknolojia Mh Manyanya.
Hivyo ndivyo wakaazi wanaozunguka ziwa Nyasa wanavyoona fahari kutumia Rasilimali Hadhimu ya Ziwa Nyasa wakiwa katika mtumbwi kuelekea kutafuta ridhiki katika ziwa lao hakika ni fahari kuwa na tunu ya aina hiyo.
Mwonekano wa Ziwa Nyasa na Maji ya kupendeza pembeni kukiwa na uoto wa asili.
Uzuri wa Ziwa Nyasa unaambatana na Visiwa vyenye mvuta na historia ya aina yake hicho kinachoonekana kwa mbali ni kisiwa cha Lundo ambacho kina historia ya aina yake kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Unapofika Ziwa Nyasa huna hofu ya kukuwezesha kufika katika kisiwa chochote kujionea uzuri wa Ziwa hilo na yanayopatikana katika fukwe na visiwa vinavyovutia kuvitembelea kuna usafiri wa boti kama unavyoiona pichani na manahodha wenye ujuzi wa kuziendesha pia kuna mitumbwi kwa ajili ya kusafirisha watu.kwenda upande wowote wa ziwa hilo.
Boti la kisasa linalotumika kusafirisha Abiria wa Majini katika pande zote za ziwa Nyasa kama unavyoona wataalamu wakiliendesha kuelekea maeneo ya visiwa vilivyopo Ziwani.
Meneja wa TANESCO Kanda ya Kusini Joyce Ngahyoma akiwa katika ziwa Nyasa kujionea usuri wa Ziwa hilo maarufu Duniani lenye utajiri wa vivutio ambavyo maeneo mengine havipatikani.
Maji ya Ziwa Nyasa ni Maangavu yenye kuvutia ambayo ukiangaza unaweza kuona vitu vilivyo chini kama inavyoonekana katika picha.
Ukifika Ziwa Nyasa utakutana na nakshi ya mawe tofauti tofauti yenye kuvutia kama inavyoonekana pichani hapo ji kandokando ya kisiwa cha Lundo hakika ni nadhifu. |
Watalii wa ndani waliokuwa katika Ziara na Naibu Waziri wa elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Manyanya wakiwa katika piacha ya pamoja kando kando mwa Ziwa Nyasa katika Kisiwa cha Lundo Mbamba Bay wilayani Nyasa.
Nahodha Emmanuel Mguhi akihakikisha usafiri wa boti kama uko sawa tayari kwa kusafirisha Abiria wanaotoka Nchi kavu kwenda ziwani na katika visiwa vilivyopo katika Ziwa Nyasa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Nyasa hakuwa nyuma katika Ziara ya Naibu waziri wa Elimu kuhakikisha Usalama unakuwepo hata katika Maji aliongoza msafara wa Naibu waziri katika Visiwa na fukwe mbalimbali alizotembelea.
Mkuu wa vilaya ya Nyasa amesema kisiwa cha lundo kina vitu
vingi vya kujivunia yakiwemo mapambo ya maganda ya konokono ambayo yanaweza kutumika kama
mkufu, pia kuna samaki wa mapambo na mawe ya kuweza kupumzika. Mkuu wa wilaya
amesema wilaya ya Nyasa ina wasomi wengi wanaotoka mwambao wa ziwa Nyasa ni juu yao kushirikiana kwapamoja
kuenzi na kutangaza kuhusu utalii wa ziwa Nyasa
Mhandisi Stella Manyanya amewaomba watanzania na wazawa wa Ziwa Nyasa kuja kushuhudia visiwa vilivyoko katika ziwa nyasa ikiwemo pomonda visiwa vilivyo tumika kwa watu kujificha wakati wa vita vya pili vya dunia, pia kuona mawe mawili Jike na Dume yanayo tumika kutambikia wakati wa shida. Hayo Maji ya kuvutia yenye rangi nzuri kama yanavyoonekana pia yanapatikana Ziwa Nyasa .
Mawe yanayopatikana katika ziwa Nyasa yakiwa na naksh asili ya rangi ya kijani.
Naibu waziri wa elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya
ufundi Mhandisi Stella Manyanya amewaomba
wazawa na watanzania wote kushiriki katika sherehe zitakazofanyika Desember 30 mwaka huu. wa shida
Yonafika mzungu Katibu wa Naibu waziri wa Elimu Mahandisi Manyanya akifaidi uzuri wa fukwe za Ziwa Nyasa alipokuwa Ziara ya kikazi Wilayani Nyasa.
Mkuu wa Kituo cha Maliasili Utalii na Ufugaji Geofrey Sakala akiwa na Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya wakitafakari jinsi ya kuboresha vivutio vilivyopo katika mwambao wa Ziwa Nyasa ambavyo ni vya asili na utamaduni.
No comments:
Post a Comment