Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medard Kalemani amesema
nyumba nyingi zinazoungua kwa ajili ya Umeme ni makosa yanayotumika kwa kutumia
Mafundi Vishoka, kutandaza nyaya za
umeme pasipo na ujuzi.
Mkurugenzi wa TANESCO Kanda ya Kusini Joyce Ngahyoma akiwa katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Naibu Waziri amewaomba Wananchi kuacha kutumia Mafundi umeme
wasio na sifa, wakandarasi wote wanaohusika na ufungaji umeme majina yao yabandikwe katika mbao za
matangazo ili mwananchi aweze kujua fundi kamili ni nani.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini akiwa ziara wilayani Nyasa amewaambia wananchi wa wilaya ya Nysa kuwa REA awamu ya tatu inaanza kwa kasi ambapo vijiji vyote ambavyo havina umeme vinatakiwa kufungiwa umeme
ikiwemo na vijiji vya wilaya ya Nyasa.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medard Kalemani amesema ili kuharakisha zoezi la kufunga
umeme linafanyika kwa wakati Viongozi wa
TANESCO wanatakiwa kuweka vituo katika Kata na vijiji ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kurahisisha kupokea
malipo kwa wateja wanaounganishwa badala ya wananchi kufuata
huduma Mbamba Bay.
Wananchi wa mwambao wa ziwa nyasa wameishukuru Serikali kuleta umeme wa Rea wamesema itasaidia kupata mwanga vijijini pia katika biashara ya samaki na dagaa wanavuliwa Ziwa Nyasa wataweza kuhifadhi katka majokofu
na kusafirisha salama pindi wanapokwenda kuuza nje ya wilaya pamoja na kukuza uchumi kwa kufanya shughuli zinazohitaji umeme.
Meneja wa TANESCO wilaya ya Nyasa akifuatilia kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini katika kutekeleza Mradi wa REA awamu ya tatu wilayani humo.
Afisa tawala wa wilaya ya nyasa Richard Mbambe akimweleza
naibu waziri wa Nishati na Mdini amesema kati ya vijiji 94 vya wilaya ya nyasa
ni vijiji 7 tu ndivyo vilivyo na umeme wa Rea hivyo juhudi zina takiwa
kuvifikia vijiji vilivyo baki
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr. Medard Kaleman amesema katika Mkoa wa Ruvuma watu ambao hawajafungiwa Umeme wa REA wanafikia zaidi ya 3000 na ifikapo 2018 kila Kijiji kitakuwa umeme. Naibu waziri wa Nishati ametoa angalizo kwa kiongozi yeyote wa Shirika la TANESCO atakayeshindwa kumfuata Mwananchi basi atakuwa amejiondoa mwenyewe kazini
No comments:
Post a Comment