Mkuu wa
Wilaya ya Songe amepiga marufuku kwa Wananchi kufanya shughuli za kibinadamu
katika Eneo lililopimwa kwa ajili ya Hifadhi ya Milima ya Matogoro lenye Ukubwa
wa Hekta 6755.
Mkuu wa
Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ameyasema
hayo baada ya Wananchi wa Kijiji cha Kikunja kukataa kuweka Mipaka ya hifadhi
ya Misitu kwa madai kuwa Hifadhi ikipimwa Wananchi wananyanyaswa na Maliasili
kwa kupigwa na kukatazwa kusogea katika Mipaka hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akikagua Hifadhi ya Milima ya Matogoro Kusini ametoa Agizo kwa Mtu yeyote atakayeonekana akifanya Shughuli za kibinadamu katika Hifadhi hiyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani
kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Songea ikiongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Songea Mgema wakiw katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wa kijiji cha kikunja na uongozi wa kata ya Matimila pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu katika Kijiji cha Kikunja Songea Vijijini
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kikunja katikati Teodat Ansgar Kwanji akipokea Agizo toka kwa Mkuu wa Wilaya juu ya kusimamia ulinzi wa vyanzo vya maji katika hifadhi ya misitu kwenye eneo lake ambalo wananchi walizuia wakala wa misitu kuweka mipaka ya hifadhi hiyo kisheria
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kikunja Teodat Ansgar Kwanji amemuomba Mkuu wa wilaya
kuitisha mkutano wa hadhara kwa Wananchi ili kutoa Elimu juu ya Mipaka kwa kuwa Wananchi hawana Mihutasari inayoainisha uwepo wa Mipaka.
Eneo la Hifadhi katika safu ya Milima ya Matogoro Magharibi
Sehemu ya eneo la Msitu wa Matogoro ambalo ni chanzo kikubwa cha maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea
Wananchi wa Kijiji cha Chikunja Kata ya Matimila Tarafa ya Muhukulu
Wananchi wa Kata ya Kilagano waliokuwa wanafanya shughuli za Kilimo katika eneo la Hifadhi ya misitu
Sehemu ya eneo la hifadhi Kata ya Kilagano lililoingiliwa na wakulima kufanya shughuli za Kilimo
Afisa Mtendaji kata ya Matimila Emmanuel Njogopa akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Wilaya jitihada walizozichukua katika kusimamia eneo la hifadhi ya misitu.
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu wilaya ya Songea Manyisye Mpokigwa akiratibu sheria za uhifadhi na nini wananchi wanruhusiwa kukifanya eneo la Hifadhi amesema ni kosa kufanya shughuli za kilimo na kukata miti mibichi.
Wananchi wa Vijiji vya Kihagala, Muungano Zomba na Kilagano wamesema eneo wanalolima walirithi kwa mababu toka zamani wameomba Serikali kuwafikiria kwa kuwa hawana maeneo mengine ya kulima wamesema wapo tayari kushirikiana na Serikali kwa kupanda miti na kuilinda.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema katikati akibadilishana mawazo na viongozi wengine juu ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na wananchi kuingilia hifadhi ambazo ni vyanzo vya maji yanayotumiwa na wakaazi wa Wolaya ya Songea. Kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Songea Pendo Daniel
Viongozi wa Kata ya Kilagano wakiratibu maelekezo toka kwa Mkuu wa wilaya ya Songea namna wanavyopaswa kusimamia sheria katika kuhifadhi misitu na vyanzo vya maji kwenye maeneo yao.
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Songea Manyisye Mpokigwa ameainisha shuguli zinazopaswa kufanyika katika eneo la hifadhi ambazo haziathiri vyanzo vya maji na uharibifu wa Mazingira.
Eneo la
Hifadhi ambalo halijapimwa lenye ukubwa wa Hekta 3208 ni miongoni mwa maeneo ya
Vyanzo vya Maji ambavyo ni tegemeo kwa wakazi wa Manispaa ya Songea.
No comments:
Post a Comment