Mkuu wa Wilaya ya Makete Mkoani Njombe Veronica Kessi amewaomba Wananchi
ili kuepukana na dhuluma inayofanywa na Jamii kwa kupora Mali za wajane na
wagane suluhu yake ni kushirikiana vitendo vinavyotoa Msaada wa Kisheria kwa
Wananachi ambao hawana Elimu hiyo, Pamoja na kutoa habari zao za kudhulumiwa
kwenye vyombo vya habari.
Mkuu wa Wilaya ya Makete ameyasema hayo baada ya Wagane na Wajane 80 kupata msaada wa kisheria na kuweza kurudishiwa mali walizoporwa.
Mkuu wa Wilaya ya Makete Veronica Kessi amesema wilaya ya Makete ina Kata
23 na katika Kata hizo kata 22 zina wasaidizi wa kisheria ambao wamekuwa msaada
kwa wasiojua sheria wakishirikiana na vyombo vya habari za kitaifa pamoja na vyombo vya wilaya
ikiwemo Green FM na Kituro FM
Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amesema anashukuru vyombo vya habari kwa kuwa wameweza kusaidiana na wananchi katika kupunguza migogoro mbalimbali inayowakabili wananchi kwa kutangaza hatua zinazochukuliwa na Serikali baada ya kuona wajane na Wagane wakitaka kudhulumiwa mali zao.
Mkuu wa wilaya ya Makete amesema kuwa na wasaidizi wa
kisheria kwa Kata 22 za wilaya ya Makete kumeleta mwanga kwa wasiojua
sheria kusaidiwa na kupata haki zao
ikiwemo kurudishiwa mali zao.
Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amelipongeza Shirika lisilokuwa la kiserikali la PADI likishirikiana na shirika la Msaada wa Kisheria SOPSE kutoa Elimu kwa wasaidizi wa kisheria na kuweza kufuzu vizuri katika utetezi huo, amesema wilaya itaendelea kusaidia Asasi zinazounga mkono shughuli za Maendeleo ikiwemo PADI
Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa amesema wafadhili baada ya kuona PADI ilivyofanya vizuri katika mwaka mmoja uliopita wameongezewa ufadhili kwa miaka mi nne na kuongeza wigo wa utoaji huduma kutoka wilaya moja ya Makete hadi kufikia wilaya tano za Mkoa wa Njombe.
Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa amesema vitendo vya kudhulumu wajane na wagane katika wilaya ya Makete vilikuwa vingi mno kiasi cha kuwaacha watoto waliofiwa na wazazi wote wawili kuishi kwa matatizo jambo lililosababisha ongezeko la watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi.
Shirika la PADI limeweza kufikisha Elimu kupitia vitengo vya
kisheria na kuweza kusaidia watu 80 waliopatwa na majanga ya Mirathi, ndoa na
masuala ya kumiliki Ardhi.
Mkurugenzi wa PADI ameomba pamoja na washauri wa kisheria wameweza kufanikiwa katika kazi hiyo lakini msaada wa vyombo vya habari kama inavyofanya Radio Free Africa , Green FM na Kitulo Fkujitolea kutangaza matukio yanayowapata Wagane na wajane kwa kutangaza bure, na vyombo vingine viige tabia hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji Halimashauri ya Makete Gregory Emanuel amesema katika kupata kituo hicho sasa suala la
Maendeleo liko mbele kwani migogoro ya Ardhi sasa imepungua , kwa kiasi kikubwa
sasa wananchi wanashiriki kazi za
Maendeleo. Migogoro inashughulikiwa na wasaidizi wa kisheria kwa njia ya
upatanishi.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Makete Felex Mbwiro amesema kazi ya
Afisa Maendeleo ni kuhakikisha hakuna Mwananchi anayekosa Maendeleo kwa ajili
ya kunyanyaswa kwa kudhulumiwa mali zake, akiungwa mkono na Afisa Idara ya maji
jinsi vitengo vya kisheria vinavyosaidia wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessi amewaomba wananchi na Viongozi wa Serikali kutofumbia macho vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa wananchi kwa kudhulumiwa mali zao na familia za wajane na wagane baada ya mme au mke wa marehemu kufariki. Na kuwataka waache kudhulumu mali za familia ya marehemu aliyefariki badala yake wawe wasimamizi kuhakikisha hakuna anayeingia na kudhulumu mali hizo.
No comments:
Post a Comment