Bweni la
wanafunzi wavulana katika shule ya sekondari Nandembo limeungua moto na
kuteketea kwa Mali zote za wanafunzi zilizokuwamo, wakati wanafunzi wakiwa
katika nyumba ya ibada.
Akiyoa
taarifa ya moto kaimu afisa Elimu W Mwalimu Habiba mfaume alisema taarifa za
kuzuka kwa moto walizipata majira ya saa moja na nusu jioni kutoka kwa uongozi
Wa shule ya sekondari Nandembo za kutokea kwa moto na kuunguza bweni la
wavulana.
Ukosefu
Wa kikosi cha Zima moto katika wilaya ya Tunduru umesababisha mali za wanafunzi
kuteketea kwa ni walitumia tu njia za asili kama mchanga na mitungu ya gesi ya
Fire extinguisher iliyopo katika maeneo ya hostel kwa kushirikiana na majirani
Wa shule.
Alisema
bweni hilo walikua wanakaa wanafunzi 72 ambao vitu vyao vimeteketea kwa moto na
ikiwa ni pamoja na magodoro, vitanda, madaftari na vifaa vingine vyote
vilivyokuwamo ndani ya bweni hilo.
No comments:
Post a Comment