Katibu wa Baraza la Madiwani
ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Dkt Oscer Mbyuzi amesema Baraza limeamua
kumfukuza Afisa Utumishi Maiko Alex
Mbunda kwa kukiuka maadili ya Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa amesema
Halmashauri ya wilaya ya Nyasa imeweka mikakati mbalimbali kwa kushirikiana na madiwani wa Halmashauri hiyo ili kuinua kiwango cha
Elimu na kurudisha hali ya zamani ya ufaulu ambapo huko nyuma Halmashauri ya Nyasa iliweza kutoa wasomi wengi na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa.
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wakiwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya kwanza katika mwaka 2017/2018 ulioanza july - october 2017 katika ukumbi wa Capten Komba Mbamba Bay wilayani Nyasa.
Wajumbe wa Baraza wakizungumza kuhusu kushuka kwa Elimu wamesema ili Elimu ipande kunahitajika ushirikiano baina ya wazazi, walimu wana siasa na jamii nzima kila mmoja akitimiza wajibu wake heshima ya halmashauri ya wilaya ya Nyasa kutoa wasomi wengi itarejea.
Wajumbe wakiendelea kuchangia juu ya suala la Elimu wamesema inasikitisha kuona wazazi wamekuwa wakiwa wepesi kunyooshea vidole walimu pindi matokeo yanapokuwa hayaridhishi bila kujiuliza wao kama wazazi wanawajibika vipi kushirikiana na walimu katika kupandisha kiwango cha Elimu kwa watoto wilaya ya Nyasa.
Wilaya ya Nyasa katika Matokeo ya Mtihani wa darasa la saba 2017 imekuwa ya 171
mwaka jana ilikuwa nafasi ya 139kitaifa.
Katika kikao hicho pia Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Nyasa limeweka mikakati ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kusogeza huduma kwa wananchi katika sekta ya Maji Kilimo na Uvuvi.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wakipitia Agenda za Kikao wakati mwenyekiti wa Halmashauri Alto Komba akiongoza Kikao.
No comments:
Post a Comment