Serikali Mkoani Ruvuma imelishukuru serekari ya Italia
na Dhehebu la Kanisa Katoliki Jimbo Kuu
la Songea kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuondoa Umaskini miongoni mwa wanawake
wazee na Vijana.
Balozi wa Italia Nchini
Tanzania Roberto Mengoni amesema ana
tegemea mradi wa maziwa uuzaji wake utaweza kufikiahadi mikubwa kama Dar es salaam
Mhashamu Asikofu Mkuu wa
Jimbo la Songea Damian Daluamewshukuru
kwa serekari ya italia kwa kuweza kuwa fanzili wa fugaji katika Nyanja za Ufugaji Ng`ombe, Kuku, Nyuki na Kilimo na kuwafanya waweze kufikia uchumi
wa kati.
Wadau waliokuja kushuhudia ghafula ya uzinduzi wa Maabara ya Mifugo na zoezi la kuhitimisha wafugaji na wakulima walionufaika na mafunzo ya kilimo na mifugo kupitia ufadhili wa Serikali ya Italia
Mradi wa FARE katika Chuo cha
Mifugo Mahinya wilayani Namtumbo toka
ulipoanza umeshawafikia wakulima 3000 pia baadhi ya wanufaika wame weza
kupewa vitendea kazi.
Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo katoliki la Songea Askofu Damian Dalu kushoto amesema wananapata faraja wao kama kanisa kuona wanapata wadau wa maendeleo wanaounga mkono jitihada za kanisa katika kushirikiana na Serikali kuinua Elimu ya jamii ya Watanzania kwa kuwasaidia kuwaongezea maarifa ya ujuzi na kufanya usatawi wa jamii uimarike.Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Damin Dalu amesema lengo la kanisa kuinua watu katika nyanja za elimu na kuondokana na umaskini elimu wanayoitoa ni ile inayoanzia ngazi ya chini ya awali ili kujenga msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binith Saatano Mahenge ameyasema
hayo katika Hafla ya kufunga mafunzo ya Kilimo na Mifugo kwa wafugaji 59 kutoka
katika Vijiji vya Mkoa wa Ruvuma ufungaji ulio
ambatana na uzinduzi wa maabara ya
mifugo katika chuo cha Mafunzo Mahinya wilaya ya namtumbo mkoa wa Ruvuma ,Mkuu wa Mkoa ameishukuru nchi ya Italia kwa
kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania
Afisa Mifugo wa Mkoa wa Ruvuma Dr Ramadhani Mwaiganju akitoa ufafanuzi wa Matumizi ya vifaa vya kufanyia kazi kwa wahitimu 58 wa Mafunzo ya Mifugo kupitia mradi wa FARE wakishirikiana na shirika la COPE kwa ufadhili wa Serikali ya Italia katika Kituo cha Mahinya Kata ya Msindo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Mgeni Rasmi katikaghafla ya kufunga mafunzo kwa wafugaji na wakulima wa Mkoa wa Ruvuma Balozi wa Italia Nchini Tanzania Robertor Mengoni akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge wakikabidhi vyeti na vitendea kazi kwa wahitimu wa mafunzo ya kilimo na mifugo yaliyowezeshwa na Serikali Itali kupitia Mradi wa FARE (Fair Agro - Zootechnical Reginal Empowermrnt) Mkoani Ruvuma.
Mradi wa FARE ni mradi wa miaka miwili mkoani Ruvuma wenye lengo la kujengea uwezo wananchi wa vijijini wenye kipato cha chini na kuwawezesha kujiiniua kiuchumi kutoka kwenye hali ya chini hadi uchumi wa kati wa viwanda vidogovidogo.
Wahitimu wa Mafunzo ya Ujasiliamali Kilimo na Mifugo kutoka Vijiji vya wilaya 3 za Mkoa wa Ruvuma wameshukuru kwa kupata mafunzo ya kuwawezesha kufuga kisasa na kilimo cha biashara wameomba kuendelea kupewa mafunzo endelevu ili kuwajengea uwezo zaidi pia wameomba serikali ya mkoa wa Ruvuma kuwawezesha Mikopo ya Ng`ombe na Fedha ili iwasaidie kupata mitaji ya kuendesha shughuli za kiuchumi zinazoendana na mafunzo waliyoyapata.
Wahitimu walionufaika na Mradi wa FARE wameiomba Serikali kutatua changamoto ya kukosekana kwa umeme wa uhakika katika eneo la mradi katika Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji endelevu Mahinya ili kurahisisha utoaji wa mafunzo kwa vitendo na hasa katika Maabara ya Mifugo ambayo imezinduliwa itakayosaidia kuchunguza afya ya Mifugo mkoani Ruvuma.
Viongozi wa Serikali ya wilaya ya Namtumbo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr binilith Satano Mahenge, Balozi wa Italia Nchini Tanzania Robertor Mangoni, Mhasham Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Askofu Damian Dalu na Mkurugenzi wa Taasisi ya AICS kutoka Italia wafadhili wa Mradi wakiwa katika picha ya pamoja katika chuo cha Mafunzo ya Mifugo Mahinya.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Mahenge kushoto ameagiza shirika la umeme TANESCO wilaya ya Namtumbo na Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma wahakikishe wanafikisha umeme kwa haraka katika chuo cha Mifugo Mahinya ili kuwezesha vifaa vilivyopo katika Maabara ya Mifugo kufanya kazi ya utafiti wa magonjwa ya mifugo na tiba.
Mhandisi Dr Binilith Saatano Mahenge Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiwa na Balozi wa Italia Nchini Tanzania Robertor Mengoni wakipokea taarifa ya kazi za Maabara ya Mifugo iliyopo Chuo cha Mifugo Mahinya wilayani Namtumbo muda mfupi kabla ya kuzindua.
Mkurugenzi wa Shirika la COPE
Nchini Tanzania Valentina Quaranta
amesema shirika lake limeweza kutoa Mafunzo ya Ufugaji kwa wakulima 200 shabaha
ni kuendeleza viwanda vya uzalishaji maziwa hasa kwa kuwainua Wanawake.
Mkurugenzi wa Chuo cha Mahinya Zakayo Mwampagatwe akitoa ufafanuzi mbele ya wageni wa Heshima katika ghafla ya kuhitimisha wakulima 58 waliopata mafunzo ya Ufugaji endelevu, Kilimo bora na ujasiliamali.
No comments:
Post a Comment