KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, November 16, 2015

NFRA MKOA WA RUVUMA YA ELEMEWA NA MZIGO WA MAHINDI ,WALIO PEWA VIBALI WAOMBA KUJA KUCHUKUA MAHINDI HARAKA



Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu ameiomba Mikoa ambayo imepata kibali cha kuchukua Mahindi katika Hifadhi ya Chakula NFRA  Mkoa wa        Ruvuma waje haraka ili kupunguza wingi wa Mrundikano wa Mahindi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema Hifadhi ya Chakula ya Mkoa wa Ruvuma ina Tani zaidi ya Laki Moja, kutokana na hali ya Masika inayokuja Mahindi yanaweza kuharibika.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amesema kutokana na Mlundikano uliopo wa Mahindi katika ghala la kuhifadhia mahindi  NFRA kuwa mengi. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameiomba Mikoa iliyo pata kibali cha kuja kuchukua Mahindi waje haraka ili  kutoa nafasi ya kuweza kupokea Mahindi mengine kutoka kwa wakulima
Mkuu wa Mkoa amesema Mwaka huu serekari haikopi mahindi ya Mkulima ina nunua kwa Fedha Tasilimu


Wakulima kuuziwa Pembejeo feki kwa kuwekewa Chumvi na Simenti ni njia moja wapo ya kurudisha maendeleo ya wakulima ukizingatia Mkulima wa Tanzania hana Bima hata akikosa Mazao Shambani hilo lina kuwa swala lake Mwenyewe

 Vijana wakijitahidi kupakia Mahindi ili kupeleka Sehemu ambako hakuna Chakula lakini hata Hivyo haionekane palipo chukuliwa Mahindi

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amewaonya wale wote wanaouza Pembejeo  feki kwa kuwadanganya wakulima  kuwa ni Mbolea kumbe wametia Chumvi au simenti, Watu hao wakikamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

 Meneja wa NFRA Mogani akiongoza msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akionyesha hali halisi ya Mlundikano wa Mahindi katika Ghala la NFRA
Kama unavyo ona mahindi yalivyo Rundikana yana hitaji kuondolewa ili nafasi ya kuweka mahindi mengine, kuna zaidi ya tani laki moja hivyo Mikoa yenye njaa au iliyo pewa kibali ije kuchukua Mahindi

Thursday, November 12, 2015

BARAZA LA WANAWAKE WA CHADEMA (BAWACHA) MKOA WA RUVUMA WAMEMUOMBA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA KUTENGUA UTAUZI WA ZUBEDA HASSAN SAKURU KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA RUVUMA


 Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Ruvuma wamesema wanapinga vikali kuteuliwa Zubeda Hassan Sakuru kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.
 Wanachama wa BAWACHA Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma wametoa Tamko la pamoja, wapo tayari kutoka CHADEMA endapo uteuzi huo hautabatilishwa  wamesema Zubeda Hassan Sakuru siyo mkaazi wa Mkoa wa Ruvuma hata wilaya waliyo sema ana toka Tunduru  hakuna hata mmoja anaye mjua . Jambo waliyo baini nikuona chama kipo mkononi mwa mtu mmoja.
 Wajumbe wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Ruvuma (BAWACHA) wakiwa ndani ya Ofisi za CHADEMA wilaya walipokutana kwa ajili ya kutoa tamko la kupinga Uteuzi wa Mbunge wa Viti Maalum atakayewakilisha Mkoa wa Ruvuma uliofanywa na Uongozi wa CHADEMA Taifa.
 Wanawake wa CHADEMA kutoka wilaya za Tunduru, Nyasa, Mbinga, Namtumbo, Songea Vijijini na Songea Manispaa walipokutana katika Ofisi za CHADEMA wilaya ya Songea kutoa TAMKO hilo.
 wanachama wa Chadema wakiwa nje ya Ofisi za CHADEMA wilaya Matarawe Manispaa ya Songea mara baada ya kutoa Tamko la Kupinga Uteuzi huo wa Mbunnge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.

Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma (BAWACHA) wamemuomba Mwenyekiti wao wa CHADEMA Taifa Filiman Mbowe kubadilisha uteuzi alioufanya kumteua mtu ambaye hayuko katika Mkoa wa Ruvuma anaye tokea Tanga na kumteua kama mkazi wa Mkoa wa Ruvuma.
 Wajumbe wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma wameshangaa kuona hata Uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma hawakuonekana katika kikao kilicho andaliwa rasimi kupinga uteuzi wa Zubeda Sakuru na kudai uteuzi huo wa kumfanya Mbunge wa mkoa wa Ruvuma wamedai umetumika kulipa fadhila zinazo tiliwa mashaka.
 Wanachama wa BAWACHA  nje ya Ofisi za CHADEMA wilaya ya Songea Mjini.
Wajumbe wa BAWACHA kutoka wilaya za Mkoa wa Ruvuma.

Saturday, November 7, 2015

SWALA LA KUWAKOMBOA WAZEE KAQTIKA KUPATA HAKI ZAO UPO MIKONONI MWA WAANDISHI WA HABARI


Nchi ya Tanzania ni nchi ya 91 kati ya Nchi 96 Duniani kwa Wazee kuwa katika hali hatarishi kwa maisha ya wazee kwa kukosa mahitaji muhimu ikiwemo afya, Elimu Chakula na Malazi.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa ameyasema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma katika kutafuta njia ya kuwakwamua wazee waweze kutokana na hali hiyo.


Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wameazimia kuifahamisha Serikali kujua kuwa haki ya Kuishi pamoja na huduma nyingine ni wajibu wa Serikali kuwatekelezea Wazee.


Mkurugenzi wa shirika la PADI linalohudumia wazee Nchini Tanzania Iskaka Msigwa amesema Tanzania ina wazee wapatao milioni 2.5, wanawake wakiwa milioni 1.3 na wanaume milioni 1.2. Idadi hiyo ya wazee ndiyo inayohudumia Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na kupelekea wazee hao kuambukizwa magonjwa ya kuambukizwa ikiwemo Ugonjwa wa UKIMWI.

 Waqandishi wa Habari wakijadili jinsi ya kunusuru Maisha ya Wazee kuhusiana na Changamoto zinazo wakabili

Aidha Wazee wanatakiwa wapewe kipaombele kama ilivyo kwa Wanawake kuwa na Wawakilishi katika viti Maalumu vya Ubunge na Udiwani, vivyo hivyoi na Wazee wanatakiwa wawe na Viti Maalumu vinavyowakilisha wazee.

 Moja ya Wazee ambao wana tegemea kinga kutoka kwa jamii jinsi yakupata kinga ya tuhuma mbalimbali kutoka kwa watu wenye imani potofu.Wazee wanalia na Pesheni ya kuweza kupata fedha ingawa kidogo tu

Katika Kikao hicho imebainika kuwa huduma za Wazee zinashindwa kutekelezawa kutokana na kutokuwa na wawakilishi katika Vyombo vya Maamuzi kama

Friday, November 6, 2015

JEE MCHAKATO WA UCHAGUZI ULIKUWAJE KATIKA TANZANIA ?

 Una weza kuona matokeo ya Uchaguzi wa Urais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania yalivyo ushindani ulikuwa mkubwa ndiyo maana Rais Mteule wa Jamuhuri ya Mungano Tanzania Dr John Pombe Magufuli  alisema alikuwa na washindani na siyo vyama vya siasa. Hii ni kuonyesha kuwa watanzania wa sasa sio wale wazamani Watanzania sasa wameamuka. Hii ni dalili mzuri ya kufikia Maendeleo Tuombe ushirikiano walio onyesha wa tanzani katika uchaguzi hali hiyo hiyo ihamie kwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wote walio chaguliwa
 Unapo sherekea Amani katika uchaguzi Mkuu nilazima ujue kuna watu walikesha kuombea Amani Miongoni Mwao ni Mkurugenzi wa PAD Shirika linalo hudumia wazee Issaca Msigwa hapo akionekana akitoa Elimu Mkoani Njombe kuwa omba watu wote Wachungaji Wazazi na Viongozi mbalimbali kuwa elimisha vijana kujiepusha na Vurugu
 Mkurugenzi wa PAD akiwa na Wanasheria Mkoani Njombe ambao walikuja kutoa Elimu ya Kisheria kuzingatia amani na Hasara ya kuto kuwepo kwa Amanmi
 Wafanyakazi wa Shirika la PAD Mkoani Njombe wakihudumia Watu walio shiriki kopngamano la Amani Mkoani Njombe
 Mwandishi Judith Lugoye aliye kuwa akikusanya mambo mbvali mbali yaliyo husiana na utengamavu wa Amani katika Uchaguzi Mkuu
 Pasipo kumkumbuka Mungu Amani haiwezi kupatikana waimbaji mwa kanisa la  New Good Singer kutoka kanisa la EGT
 Waimbaji Hawa waliwakonga Watu walio hudhuria Kongamano la Amani katika uimbaji wao huku wakitoa mifano mbalimbali juu ya kupotea Amani
                                                                                 ETAG
                                                                           Good senger
 Watu walio hudhulia kongamano la Amani wakijadili mambo ambayo yanaweza kuleta Amani kipindi chote cha uchaguzi ,ikiwa na pomoja na kukaa na vi9jana wao katika kuwa elimisha maana kamili ya uchaguzi
 picha ya pamoja waliyo piga katika mdahalo wa amani kila mmoja akiwa ameahidi kufikisha ujumbe wa amani kwaq watu mia moja
                             katibu wa Jukwaa la Amani kabla ya uchaguzi na Baada ya uchaguzi
 wajumbe wa jukwaa la Amani kabla ya uchaguzi na Bada ya uchaguzi wakiratibu mambo mhimu ya kulitoa taifa letu katika Amani
 Matunda yaliyo onyeshwa baada ya Elimu kutolewa wanchi wakipiga kura kwaq Amani na Utulivu
 Uikiwa Mwandishi wa Habari unatakiwa uwe wakwanza katika kufuata tarati sheria na kanuni za Nchi hapo Adamu Mzuza bNindi akipiga kura katika kituo cha Mkombozi Mjimwema Manspaa ya Songea kumchagua kiongozi bora na siyo bora kiongozi
 upigaji wa kura ulikuwa wa siri hapo Adamu Mzuza Nindi akiwa amejificha katika banda la kupigia kura na kutumia haki yake ya kidemokurasia ya kumchagua kiongozim anaye mtaka
 Mchakato wa uchaguzi ulikuwa ukifuata taratibu zote za uchaguzi hapo ndugu Adamu Mzuza Nindi akimalizia taratibu ya mwisho ya kutumbukiza kura yake kwenye masanduku ya Rais,Mbunge na Diwani ndiyo maana watanzania walioshiriki zoezi la upigaji kura, wanashangaa pale utakapo sema uchaguzi ulikuwa sio wa haki, Haki ipi inayo tafutwa kuliko hii tunayo iona
 Kila aliyestahili kupiga kura aliangalia jina lake kwenye ubao, watu waliwasili katika vituo vya kupigia kura kuanzia saa kumi na moja alfajili ili wapige kura na kurudi kufanya shuguli zingine
 Wananchi wa Manispaa ya Songea wakitekeleza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 25, 2015.
 Wasimamizi wa Uchaguzi katika Kituo cha Mahenge wakiwa na nyuso za furaha bila hofu yoyote kutokana na uwepo wa Amani ambayo ni tunu ya Taifa letu inayoifanya jamii ya watanzania kuendelea kuilinda na kuitunza katika kipindi chote cha hatua mbalimbali zinazolenga kusukuma maendeleo ya Taifa la Tanzania.
 Mkusanyiko mkubwa wa wananchi wazalendo wa Tanzania wakifuatilia matukio ya uchaguzi ambayo yamefanyika kwa amani na uhuru kuanzia wakati wa Kampeni  mpaka upigaji wa kura na hatimaye kuwapata Viongozi kwa haki na Amani. Pichani wananchi wakielekea kupiga kura na wengine wakifuatilia orodha za wapiga kura. Hayo yote yameendelea kwa utulivu kutokana na Amani iliyotawala katika kipindi chote cha zoezi la kufanikisha Uchaguzi Mkuu.
 Zoezi la kupiga kura Tanzania Bara lilifanyika kwa utuvu mkubwa kwa kudumisha amani kupitia maombi mbalimbali ya wananchi na Viongozi wa Dini kuliombea Taifa la Tanzania liendelee kuwa kisiwa cha amani, kama inavyoonekana pichani wananchi wakielekea kupiga kura pasipo shaka yoyote.
Kama unanvyoona watu walikubali kukaa muda wowote ili mradi wahakikishe haki yao ya msingi wanaipata ya kupiga kura.