KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, October 12, 2015

HALI YA UKATILI NA MAUAJI KWA WAZEE WA TANZANIA INASADIKIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 5 WAZEE ZAIDI YA 2866 WAMEUWAWA KWA IMANI ZA USHIRIKINA

Waandishi mbalimbali kutoka mikoa yote Tanzania wakihudhulia Mkutano Malumu unao jadili jinsi ya kurekebisha na kuwapa ulinzi wazee ili wasuwe kinyama kama wanavyo tendewa
Wandishi wakisikiliza kwa makini hoja zinazo tolewa kuhusu unyanyaswaji waq wazee katika mikoa mbalimbali ya Tanzania
 Mkurugenzi Msaidizi wa shirika la Help Age InternationalSmart Daniel akifungua mkutano waandishi wa Habari kutoka mikoa mbali mbali nchini Tanzania ,kujadili jinsi ya kuweza kuokoa maisha ya Wazee katika hali tete inayo wa kabili kwa Mwaka 2012 na 2013 mauaji ya wazee kwa imani za kishirikina yalikuwa 630 na 765 wengi wao wakiwa wazee wanawake
Jopo la waandishi wa habari kutoka Tanzania Bara na kisiwani wakisikiliza maada mbambali zilizokuwazina tolewa ukumbi wa ubungo plaza jijini Dar -es -salaam

Mambo mhimu yanayojadiliwa katika mkutano wawaandishi wa habari ni pamoja na kuangalia hali tete inayo wakuta wazee walemavu. hapo mzee mlemavu akitumia baikeli kwa kuweza kurahisisha katika kutembea
Joseph Mbasha meneja mradi wa shirika la HelpAge akiwakilisha mada kuhusu wazee wanavyo kabiliwa na matatizo mbambali hiyo yote ina tokana na kuto pitisha sera ya wazee ambayo toka mwaka 2003 haijulikani hatima yake kutokana na hilo wazee bado wapo hatarini kwa kipindi cha miezi sita kwa mwaka 2014 jumula ya wazee 320 waliuwawqa kwa imani za kishirikina

Waandishi wa habari wakiwa kazini kuchukua hutuba ya kaimu msaidizi wa HelpAge Smart Daniel akieleza kuhusu vifo vilivyo tokea toka mwaka 2013 mpaka 2014 zaidi ya wazee 2896 wamepoteza maisha kwa kukosa huduma mhimu ikiwemo na vifo vinavyo tokana na kudhaniwa kuwa ni Wachawi
                     Waandishi wa habari wakiwa na wadau mbalimbali wanao hudumia wazee
                                                            wandishi wa Habari

                         Edita Karo mwandishi wa Mtanzania akiingia ukumbi wa Ubungo Plaza
                                    Mwandishi wa habari Wilison Elisha  akiwa anatuma habari StarTv
Kaimu Msaidizi wa HelpAge Smart Daniel akitoa msisitizo jinsi Waandishi wanavyo takiwa kukabiliana na mauaji ya wazee yanayo tokea kutokana na imani za ushirikina
Moja ya waandishi wa Habari walio hudhuria mkutano wa kujadili hatima ya wazee nchini tanzani

Wednesday, October 7, 2015

KATIKA NCHI 96 ULIMWENGUNI TANZANIA NIYA 92 KWA KUKOSA ULINZI KWA WAZEE


Mauaji ya Wazee katika Maeneo mbalimbali yanatokana na Serikali kutotunga Sheria ambayo ita walinda Wazee, katika kuishi kwakuweka kinga ya usalama wao.


Mauaji ya Wazee katika Maeneo mbalimbali yanatokana na Serikali kutotunga Sheria ambayo ita walinda Wazee, katika kuishi kwakuweka kinga ya usalama wao.
Mkurugenzi wa Shirika linalohudumia wazee la PAD Issaka Msigwa, amesema katika Nchi 96, Tanzania imeonyesha kushika nafasi ya          Nne kutoka mwisho kwa hali hatarishi ya Maisha ya Wazee, hiyo inatokana na Jamii kutoshirikishwa katika kulinda Maisha ya Wazee.
Mkurugenzi wa Shirika linalohudumia wazee la PAD Issaka Msigwa  amesema Shirika la Kimataifa la Help Age  Duniani katika utafiti wake umeonyesha ukatili kwa Wazee kwa, mauaji na vitendo vingine vya unyanyasaji Tanzania inachukua nafasi ya 92 katika Nchi 96, mwaka 2013 ilikuwa ya mwisho katika Nchi 96.

                               Umati katika Sherehe za Wazee Duniani Mkoani Ruvuma
 Wazee wanawake walio hudhuria sherehe za Wazee Duniani zilizo fanyika katika viwanja vya H/ya Songea
 Wananchi walio hudhulia katika sherehe za wazee Duniani zilizo fadhiliwa na shirika lisilo la kiserekari la PAD la Mkoa wa Ruvuma
                            Orodha ya Nchi mbalimbali zinavyo weza kuhudumia Wazee

Viongozi wa Dini wa Madhehebu ya Kikristo na Kiislamu wamemuaomba Mwenyezi Mungu kulinda Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Okatoba mwaka huu.

                                     Wazee wakilisakata Rumba kukumbuka Enzi za ujana wao
                                         Wageni walikwa kwenye sherehe za Wazee DFuniani
             Dr Ngaiza akiwa kwenye viwanja vya Manspaa ya Songea kushiriki Siku ya Wazee Duniani

Nao Viongozi wa Vyama vya Siasa wamesema endapo wataingia Madarakani watahakikisha hali za wazee zinazingatiwa ikiwa ni pamoja na kutunga Sheria ya Wazee pamoja na kuimarisha Uchumi wa Wazee.

 Makamu Mwenyekiti  wa Baraza la Wazee Sofia Hasara akiwa kwenye Sherehe Za wazee

 Wazee walio shiriki siku ya wazee duniani AQnna Tembo Afisa Upelelezi wilaya ya Songea Akisalimia Wazee

Nao Viongozi wa Vyama vya Siasa wamesema endapo wataingia Madarakani watahakikisha hali za wazee zinazingatiwa ikiwa ni pamoja na kutunga Sheria ya Wazee pamoja na kuimarisha Uchumi wa Wazee.

 Katibu wa wazee aqliye vaa suti ya Blue Daudi Mpangala akijiandaa kusoma Risala
 Orodha hii ina onyesha jinsi Tanzani inavyo shika nafasi ya 91 katika nchi 96 katika kuwa hudumia wazee
 Akina mama wa Manspaa ya Songea Wakiwa wana sikiliza Jinsi viongozi mbalimbali wanavyo ahidi kuwa tumikia Wazee
Mwandishi wa Fikira Pevu Judith Lugoye akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Songea  Gama kupitia Chama cha Mapinduzi

JENISTA NA MRADI WA MAJI JIMBO LA PERAMIHO SONGEA VIJIJINI ATUMIA SHILINGI MILIONI MIA MOJA THEMANINI


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Peramiho kupitia Chama cha Mapinduzi Jenista Johakimu Mhagama ameomba kuchaguliwa tena ili aweze kumaliza Miradi ya Maji na Miundo mbinu ya Barabara aliyoianza.


Mheshimiwa Jenista Johakimu Mhagama mpaka sasa kwa mradi wa Maji ameshatumia kiasi cha Shilingi Milioni 180 kwa kutandaza Mabomba na kujenga matangi ya Maji.

Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Jenista Mhagama amesema kazi iliyobaki kwa Upande wa Maji ni kuingiza Maji kwenye Tanki na kusafisha Mabomba ili maji yaweze kuanza kutumika
 Watanzania Mwaka huu wamekuwa makini na kampeni wana sikiliza kwa makini ili October wasifanye makosa

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amewaomba wagombea wote wa vyama vya upinzani kufanya kampeni kwa Amani na Utulivu pia kuachana na kuweka mabango katika sehemu hatarishi kama kwenye nguzo za umeme

 Wananchi wakisikiliza sera mbalimbali kutoka kwa wagombea katika kijiji cha Matimila songea vijijini

Mwenyekiti wa kampeni Jimbo la Peramiho Jumanne Nyingo amewaomba Wananchi kuacha kujiingiza kwenye vyama vinavyoendeshwa kiundugu.Naye Mgombea Udiwani kata ya Matimila Menasi Komba ameainisha shuguli zilizo fanyika na na ccm

Wapiga kampeni wa Mgombea Uchaguzi Jimbo la Peramiho wakipiga Baragumu ya Pembe3 ya Ng'ombe wakati wa Kampeni

Tuesday, October 6, 2015



 Wafiwa na wafasi wa UKAWA wakiwa na simanzi kwa kupoteza mwenzao ERASMO NYINDI
 Mh Wiloni akiwa na Viongozi wa Kanda wa UKAWA katika Msiba wa Mhamasishaji Erasmo Nyindi uliotokea Mkoani Ruvuma
 Wafuasi wa Ukawa Wakitoa heshima zao za Mwisho kwa Mpendwa wao Erasmo Nyindi katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mbeya.
 Wanachama wa Mkoa wa Ruvuma wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Erasmo kiongozi wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
 Waombolezaji wakimlilia mpendwa wao
 Maandalizi ya Safari ya Mwisho ya Marehemu Erasmo yakifanywa na viongozi m,balimbali wa UKAWA katika Eneo la Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.
 Gari iliyosafirisha mwili wa Marehemu Erasmo Nyindi kutoka Songea mkoani Ruvuma kuelekea Mbeya.
 Mwili wa Marehemu Erasmo ukitolewa kwenye Chumba cha kuhifadhi Maiti kupeleka kwenye gari tayari kwa kuanza msafara wa kuusindikiza nyumbani kwao mbea.


 Waombolezaji wakiomboleza msiba wa Erasmo Nyindi katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma iliyopo Manispaa ya Songea.

Viongozi wa Chadema wana fanya Taratibu za kusafirisha Mwili wa Marehemu Mhamasishaji Erasmo Nyindi  kwenda nyumbani kwao mkoa wa Mbeya kwa mazishi bwana ametoa na bwana ame twaa jina lake lihimidiwe, amina.



 Baadhi ya Viongozi waandamizi wa CHADEMA wakibadilishana mawazo juu ya Tanzia ya msiba walioupata.
 Viongozi a CHADEMA wakiwa katika hali ya majonzi na kushindwa kuamini kilichotokea kwa mpenda wao.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi amesema kifo hicho kimetokana na Ajali ya Gari lenye namba za usajili T. 501 BBX aina ya Noah iliyotokea katika eneo kijiji cha Chunya wilayani Mbinga, na uchunguzi bado unaendelea.

 Waombolezaji na wafuasi wa UKAWA Mkoani Ruvuma wakiwa viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambako mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa.
 Wanachama na Viongozi wa UKAWA waliokusanyika nje ya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ili kufanikisha mipango ya kusafirisha mwili wa Mpendwa wao Erasmo Nyindi aliyefariki dunia wilayani Nyasa kwa ajali ya Gari iliyotokea usiku wa tar 2/10/2015
 Wanachama wa CHEDEMA wakiingiza kwenye Gari Jeneza la Erasmo Nyindi tayari kwa kuanza safari ya kuelekea Mkoani Mbeya kwa Mazishi.
 Baadhi ya Wafuasi wa UKAWA waliokuwapo Katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kuuaga mwili wa Marehemu Erasmo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mbozi Mkoani Mbeya kwenye Makazi yake ya Milele.
 Waombolezaji wakiwa katika hali ya mshangao na majonzi kwa kuondokewa na kada wao.
 Waombolezaji ambao pia ni wanachama wa CHADEMA wakiomboleza katika Msiba wa kada wao Erasmo Nyindi katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO)
 Waombolezaji wakimwimbia nyimbo za buriani Marehemu Erasmo Nyindi.
 Jeneza la mpambanaji na mhamasishaji wa Kampeni za Uchaguzi kupitia UKAWA kanda ya Nyanda za juu Kusini Erasmo Nyindi likiingizwa kwenye Gari tayari kwa kuanza safari ya kuelekea Nyumbani kwao Mkoani Mbeya.
 Wafuasi wa UKAWA wamesema wamepata pigo kubwa kwa kumpoteza mtu wao muhimu katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu. Wamesema amekufa kishujaa akiwa kazini kutekeleza majukumu yake ya kupigania ushindi wa Ukawa Daima atakumbukwa kwa kazi zake na mchango wake ndani ya chama.

Mtendaji Mkuu wa Kampeni za Ukawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Rajabu Kaluwa amesema ajali hiyo ilisababishwa na watu walioshika tochi nyakati za usiku wakiwa na silaha kutaka kuteka nyara msafara wa Mgombea Ubunge katika Jimbo la Nyasa Bw. Cathbet Saule almaarufu kwa jina la Ngwata (32)


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia Ukawa Kanda ya Nyanda za Juu kusini wamepata pigo baada ya kumpoteza kada wao Mhamasishaji Erasmo Nyindi     ambaye amepata ajali katika Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma akiwa katika ziara ya kazi .



Mtendaji Mkuu wa kanda ya Nyanda za Juu Kusini Rajabu Kaluwa amesema baada ya kumulikwa taa na watu wenye silaha, Dereva alishindwa kuliongoza Gari na kusababisha Ajali iliyoua mtu mmoja Mhamasishaji Erasmo Nyindi na majeruhi watatu akiwemo mgombea Ubunge kupitia ukawa na watu wawili ambao hali zao ni mbaya wako Hospitali ya Litembo wakipatiwa matibabu.