Mchakato wa kupata Katiba mpya Nchini Tanzania.
Tunaposema kupata Katiba Mpya Nchini Tanzania tuna maana gaini: Tuseme Katiba tuliyonayo haifai au Katiba tuliyonayo haieleweki kwa Watanzania, au tuseme Katiba iliyopo haikidhi Matakwa ya wale wanaotaka vyao viwe vyao na vya wenzao viwe vyao.
La muhimu ni kuangalia katika Nchi za Kiafrika ni Nchi ngapi ambazo zimekuwa na Katiba mpya baada ya kutawaliwa na wakoloni na Nchi zao sasa zimekuwa na Uhuru wa ukweli.
Tanzania imekuwa na Muungano toka Mwaka 1964 kabla ya hapo kulikuwa na Tanzania Bara yani Tanganyika na Tanzania Kisiwani yani Zanzibar. Marais wawili Rais Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Zanzibar Amani Abedi Karume waliona Uhuru walio nao hautakuwa Uhuru mpaka Nchi hizi mbili ziungane na ziwe Nchi moja na Katiba moja. Ambayo ilisomeka .
Kwa hiyo basi Katiba hii imetungwa na Bunge maalumu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga Jamii kama hiyo na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuatilia misingi ya Demokrasia, Ujamaa na isiyokuwa na Dini.
Katika sura ya kwanza ya Katiba ambayo ilitungwa mwaka 1977 Sura ya kwanza kipengere cha tatu kinasema.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi ya Kidemokrasia na ya Kijamaa isiyokuwa na dini yenye kufuata Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa.
Katika kipengere hiki kimegusa mambo ya Dini, kuwa Nchi ya Tanzania haitaongozwa kwa udini bali Wananchi wake hawakatazwi kufuata Dini yoyote ile bora wasivunje Sheria (Sura ya pili kifungu cha 39 kifungu kidogo cha 2)
Msingi mzima wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitaki Nchi iingie katika Udini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akihutubia katika Sherehe za Sikukuu ya Iddi Mwaka 2011Septemba Mkoani Dodoma alitoa kauli nzito kuwa Katiba ya Nchi iwe Katiba ya Nchi na sheria za Dini zibaki kuwa Sheria za Dini, Viongozi wa Dini wasiingize suala lolote linalohusu Dini. Katiba mpya inayotarajiwa kujadiliwa , hivyo Watanzania wawe macho na Hilo.
Watanzania katika kuangalia upya Katiba wanatakiwa wajikite zaidi katika mambo ya Afya, Uchumi, Elimu na Utawala Bora, waangalie ni dawa gani ambayo imetumika katika miaka 50 ambayo imeifanya Tanzania iwe Nchi ya amani. Dawa hiyo hiyo iingie kwenye Mchakato wa kupata Katiba mpya .
Sasa hebu tuangalie Katiba inasema nini kuhusu Uchumi wa Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sheria ya Madini haimpi ruhusa Mwananchi ambaye ana miliki ardhi, endapo kutakuwa na Madini chini ya Ardhi yake Sheria inasema Madini hayo ni mali ya Serikali.
Katiba haijagusa nani anatakiwa amiliki Madini yaliyo chini ya Ardhi ya Mwananchi. Kumetokea hali ya kutoelewana kati ya Wawekezaji katika Madini na Wananchi wakaazi katika eneo husika, Mwekezaji akipata hati ya kumiliki eneo lenye Madini yeye anachojali ni kuchimba Madini na siyo Mali ya Mwananchi anayeishi hapo.
Wananchi wamekuwa hawana haki kwanza kwa kutojua Sheria ya Ardhi, pili kutojua wawapo Kijijini wanalindwa na vipi na Sheria za Nchi.
Hebu tuone kuhusu Sheria ya Madini Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inasemaje.
Sura ya pili kipengere cha 30 kifungu kidogo cha 2b kinasema “Kuhakikisha Mipango ya Maendeleo ya Miji na Vijiji, Ukuzaji na Matumizi ya Madini au ukuzaji na uendelezaji wa Mali au Maslahi mengineyo kwa nia ya kukuza Manufaa ya Umma”.
Kutokana na Kipengere hiki cha Katiba kinasisitiza kuhakikisha kuwa Ulinzi na Usalama wa Jamii amani katika Jamii Maadili katika Jamii yanalindwa. Jee Haki ya Kumiliki Madini Mwananchi wa kawaida inamlinda vipi?
Kama Usalama wake kiulinzi ungekuwepo Wawekezaji wasinge kuwa na kiburi kwa Wananchi.
Kama Maadili yangefuatwa Wananchi wasingefukuzwa katika Maeneo ya Madini.
Sasa wananchi ili kuacha kulalamika kuhusu suala la Madini tunatakiwa tuchangie nini kifanyike kuhusu umilikaji wa Madini kwa Mwananchi wa kawaida.
Baada ya kuangalia suala la Uchumi hebu tuangalie suala la Elimu.
Katika sura ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 11 kifungu kidogo cha 2 kinasema.
“Kila Mtu anayo haki ya kujielimisha na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na Stahili na Uwezo wake”.
Kipengere hiki kinasema kila mtu ana uwezo wa kupata elimu; lakini kuna makundi ambayo hayapati Elimu Makundi hayo ni ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi wapo katika Majalala toka wanapozaliwa hadi wanapo fikisha miaka 18. Baada ya hapo wanakuwa Majambazi na kazi kuachiwa Polisi. Jee Katiba inawasaidia vipi hawa watoto.
Inaelezwa Mtu anatakiwa kuchagua Elimu anayo itaka, asilimia 80% ya Watanzania wanaishi Vijijini. Jee kutokana na Utandawazi watapataje elimu wanayo itaka. Katiba isemaje kuhusu hilo ili litekelezwe kwa Vitendo.
Baada ya kuangalia suala la Uchumi na Elimu sasa tuangalie suala la Afya ya Watanzania.
Hivi karibuni tulikuwa tukisikiliza kuhusu Matibabu ya Wabunge, Mawaziri na Rais, ipo Sheria maalumu inayoruhusu hawa Viongozi kwenda kutibiwa Nje.
Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna kipengere kinacho husu Afya ya Jamii kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za Afya, Sura ya pili kipengere cha 30 kifungu kidogo cha pili b.
Wananchi wenyewe wamekuwa Mashahidi kuhusu huduma zinazotolewa katika Hospitali za Serikali. Sheria inasema Wajawazito, Watoto walio chini ya miaka 5 na Wazee wana ruhusiwa kutibiwa bure. Hiyo imekuwa kinyume watoto asilimia 80% hupata huduma ya Afya kwa kunuliwa Dawa na Wazazi wao.
Asilimia 20% waliobaki muda fulani hupata dawa na katika asilimia hiyohiyohupoteza maisha kwa kukosa dawa. Jee Watanzania tuseme nini kuhusu suala la Matibabu haya.
Jee kama Viongozi wanatibiwa Nje wanaweza kuona Changamoto wanazo pata Wananchi wao.
Ni juu ya wananchi kuangalia kwa Makini kuhusu huu Mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Sura ya 2 Kipengere cha 11 kinafafanua kuhusu jinsi ya kupata Haki ya Matibabu, Elimu na Afya.
Utawala Bora.
Kumekuwa na Msemo wa kutenganisha kati ya Wanawake na Wanaume, kwa kusema kuna Upendeleo wa Viti Maalumu na Viti vya Kuchaguliwa.
Kwa Mtazamo wangu inaonyesha kuwa Wagombea wa Viti Maalumu kutoka kwenye Vyama vya Siasa kuna Uchaguzi Mgumu kama unavyofanywa katika Chaguzi nyingine, wanaochaguliwa kwenye Viti Maalumu huchukua watu wengi katika Uchaguzi unaoshirikisha Wanaume na Wanawake. Kusema Wanawake wa Viti Maalumu ni kuendeleza Mfumo Dume. Uchaguzi uwe mmoja bila kujali Wanawake au Wanaume. Hiyo itakuwa ndio Utawala Bora.
Mpaka Hapo Natoa Nafasi Ya Maoni Kabla Ya Kuendelea Na Srura Zingine Za Katiba Katiba Ina Sura 10 Na Kurasa 130
No comments:
Post a Comment