KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, November 29, 2011

WAUGUZI WATAKIWA WAWE NA MOYO WA HURUMA KWA WAGONJWA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Saidi Thabit Mwambungu amewataka wauguzi kuwa na moyo wa Hururuma kwa wagonjwa kwani dawa kamili ya mgonjwa ni kauli mzuri ,Dawa ya pili ni kuwa karibu na wagonjwa, Jambo la Tatu kutunza siri za wagonjwa .Namnukuru "Mnamwona Mgonjwa yule hana siku za kuishi ana UKIMWI " Mwisho wa kunukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akikagua vifaa vilivyoko Maabara ya Hospitari ya Mkoa Songea akiwa na mganga mkuu Dr. Daniel Mlalekela


Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Said Thabit Mwambungu akieleza kuhusu juhudi zilizo fanywa na serekari kuhusu ulipaji wa Mahindi ya wakulima yapayo Tani 24,000 yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 10Wauguzi wa Mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza mkuu wa mkoa jinsi serekari inavyo fanya juhudi ya kutatua kero zao ikiwa na pamoja na kutafuta jinsi ya kulipa malipo ya kujikimu yanayo tokana na madhara yanayo wapata wakiwa kazini

Sunday, November 27, 2011

MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO JENISTA MHAGAMA AMWAGA MTOTO WAKE BAADA YA KUPATA JIKO

Wabunge kutoka Nzanzibabar ,Tanzania Bara walikuja kumunga mkono mwenzao katika kumwaga mtoto wake kipenzi Ledina Mhama hapo wanaonyesha wakicheza kwa furaha zote.

Jambo la pekee linalo furahisha familia ni pale unapo ona umeweza kumsomesha mtoto wako na mtoto akapata mchumba na wewe mzazi upo. Picha ya juu ni Mama Pinda ambaye alikuja kushuhudi mtoto wa Mwenyekiti la Bunge la Tanzania Mh.Jenista Mhagama alipo kuwa akimwaga mtoto wake baada ya kupata mchumba

Mila na Desituri zina faa kuzingatiwa kwa mila za kingoni huwezi kuchukua zawadi kwenye vyombo vya kichina hapo mh. Jenista Mhagama anaonyesha jinsi anavyo heshimu mila na desturi kwa kuchukua zawadi na kuweka kwenye Jamanda akimzawadia mtoto wake Ledina Mhagama

Binti ledina Mhagama akiwa katika nyuso ya Huzuni kuona ana achana na familia aliyo izoea na kwenda kuanza maisha mapya na mchumba wake baada ya Ndoa


Kwenye sherehe huongozwa na chereko hoi hoi na vigelegele hapo Mama Pinda mke wa wawaziri mkuu Mh.Mizendo pinda akipiga makofi baada ya mshenezi kutoa mistari yenye kusisimua

Sherehe haikosi chereko Vijana wanao onekana ni kikundi cha mganda kikitumbuiza kumwaga Ledina Mhagama huku mama yake mzazi Jenista Mhagama naye akicheza ngoma hiyo kwa furaha zote


Mwanamziki wa zamani Makasi kutoka zaire aliimba furaha ipo aina mbili kucheka na kulia hapo juu ni Mke wa Mheshiwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh. Tomasi Sabaya akiwa analia haijulikani ni uchungu au furaha

Viongozi walijitoa kwenda kumfariji Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama huyo anaye toa nasaha ni Mke wa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Said Thabiti Mwambungu akimwasa mtoto akaishi vizuri na mchumba wake baada ya kufunga pingu za maisha

Mama Mwambungu akitoa zawadi kwa Ledina Mhagama aliye kuwa kulia ,zawadi ya Sufuria ili akaweze kumpikia mumewe na kama atabahatika akapikie uji kwa mtoto atakaye zaa

Ndugu za Ledina Mhagama wakiwa wame zunguka meza wakiendelea kumpa nasaha za maisha mema

Saturday, November 26, 2011

MRATIBU WA VIJANA SINGIDA AKUTWA NA MIUJIZA AMBAYO HATA ISAHAU MILELE

Mmoja wa washiriki kutoka singida kutoka kikundi cha YOUTH MOVEMENT FOR CHANGE YMC Fideriko Yunde akiwa amevuliwa koti na binti aliye jifunga kamba. miujiza iliyo mpata mulize mwenye . dunia hii kama hujafa huja umbika .ikiwa unataka kujua zaidi wasiliana naye kwa namba zifuatazo akueleze mujiza ulio mkuta 0755516482

wasanii wa kitanzania wakitumbuiza katika tamasaha la 9 katika utoaji wa tuzo kwa Azaki zilizo fanya vizuri

UTOAJI WA TUZO KWA AZAKI ZILIZO FANYA VIZURI KWA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI WASHIO PEMBEZONI

Kuishi jiji la Dar - es - salaam kuna hitaji imani hebu ona msululu huu wa magari ikiwa unaenda mahali unahitaji kuweka mda waziada zaidi ya saa moja vinginevyo unaweza kuonekana mwongo, jambo lingine linalo kera DSM ni joto na msongamano wawatu na magari DSM inataka moyo

Mkoa wa Ruvuma ulikuwa mshindi wa Pili kwa Tanzania Nzima kwa kutoa huduma bora kwa wazee,Kwa kuweza kutoa fedha za matibabu kwa wazee walioko Mkoa wa Ruvuma kupitiaPADI Hapo ni Mkurugenzi wa PADI Iskaka Msigwa akipokea tuzo kwa Devota Likokola Mbunge wa Viti malumu kutoka Ruvuma

Mama likokola Mbunge wa Viti malumu akitoa Tuzo kwa akina mama walio fanya Vizuri katika mpango wa Vicoba Nchini Tanzania




Mlemavu kutoka Tanga akipokea Tuzo la kuweza kutoa huduma bora kwa Walemavu wazee Mkoani Tanga

Msanii Mrisho Mpoki akitoa Misitari kwa washiriki wa Tamasha la 9 katika jumba la Ubungo Plaza jijini Dar - es - salaam


Washiriki wa Tamasha la 9 wakishuhudia Mikoa ya Ruvuma,kilombelo,Tanga,Zanzibar Azaki zilizo pata Tuzo kwa kuweza kutoa huduma mnzuri kwa wananchi


Hii ni sehemu ambayo Serekari imekuwa ikifanyia mikutano yake Jengo hili liko Ubungo jijini Dar - es - salaam linauwezo wakuchukua watu zaidi ya I000

UBORA WA UTENDAJI KIHABARI KARINE YA UTANDAWAZI

Kazi kubwa ya wandishi wa Habari ni kuwakilisha kero zinazo wakabili watu wanao ishi pembezoni hapo Adamu Nindi akiwakilisha kilio cha wakulima wa Mkoa wa Ruvuma baada ya Serekali kusitisha ununuzi katika mkoa wa Ruvuma na wananchi kubaki na mahindi ambayo yana hitaji fedha zaidi ya shilingi Bilioni 8 ,Hapo ni katika Tamasha la 9 lililo andaliwa na The Foundation kutasimini na kuangali changa moto zinazo wakabili Watanzania katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru.

Vyombo vya Habari Hivi sasa vimeboreshwa katika kufanikisha kupata habari kwa njia ya Video Camera hapo mpiga picha akichukua picha bila kutumia nguvu kwa kutumia mtambo wa kisasa .Vyombo mbali mbali Nchini Tanzania vinajitahidi kuelimsha wanachi kwa njia ya Televisheni hapo ni kituo cha Abood TV Mkoani Mrorogoro kikitoa habari kwa wananchi wa kanda ya kati, Hapo Mhariri wa Habari wa Abood Media Juma Kapalatu akihakikisha kila kitu kinaenda sawaHicho ni kituo cha Radio cha Abood FM katika mkoa wa Mrorogoro hapo ni wasomaji wa Tarifa ya Habari Wakisoma Tarifa ya Habari

Studio za Abood FM ziko makini katika urushaji wa Habari hapo wanangoja mwongozaji tayari kwa kuwa burudisha watanzania wanao ishi mikoa ya Morogoro,DSM,Iringa,Dodoma

Tuesday, November 22, 2011

MKURUGENZI WA THE FOUNDATION AZITAKA AZAKI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

Mkurugenzi wa The Foundation John Ulanga akieleza mafanikio yaliyo letwa na The Foundation nchini Tanzania ,ameziomba Azaki kufanya kazi kwa uadilifu kuwa kimbia wa kaguzi wanapo kuja kukagua miradi ni moja ya uzaifu wa Azaki.

Washiriki katika Tamasha la 9 linalo fanyika jijini Dar - es - salaam wakimsikiliza Mkurugenzi wa The Foundation akitoa maelezo kuhusu Ruzuku zitakazo endelea kutolewa na The Foundation kuwa kuanzia sasa hakuta kuwa na Ruzuku za kusajili asasi.

viongozi wa Andamizi wa The Foundation wakiwa tayari kujibu changamoto zinazo zikabili Azaki

MAONYESHO YA TAMASHA LA 9 JIJINI DAE -ES - SALAAM

Marukus akielezea hasara zinazo patikana kutokana na nchi kukopa na kua tia wanchi katika umasini , umasikini umeongezeka kutokana na mikopo inayo ombwa

Washiriki wa Tamasha la 9 wakiwa jijini Dar - es - salaam kujadili mafanikio na maendeleo katika nchi ya Tanzania ,Ambao wamebaini kuwa jambo linalo ikumba Tanzania na kuingiza katika umasikini ni kutegemea misaada

Banda la The FOUNDATION lilioko katika jengo la Ubungo Plaza wakiwa wame weka maonyesho na kuwaeleza washiriki kuwa The Foundation civill imeweza kuwa wezesha Azaki 2500 kwa kuweza kuwapa ruzuku ya shilingi bilioni 37 na kutoa mafunzo kwa wanchi 400 toka The Foundation ilipo anza

wasiriki wa tamasha la Azaki kutoka Tanzania bara na Tanzania kisiwani wakiwa kwenye majadiliano

VIONGOZI WA TTCL WAMEKUWA WAKIAJIBIKA KWA KUSOGEZA HUDUMA ZA TTCL KARIBU NA WANCHI KAMA WALIVYO FANYA UBUNGO PLAZA

Ndugu John Hamisi akiwa ofini Ubungo Plaza akihudumia wateja wa TTCL wateja wenyewe kutoka mikoa mbalimbali walio kuja kushiriki Tamasha la 9 la azaki zilizo kuwa za kiserekali kutoka Tanzania Mzima


Jengo la TTCL ambalo limo ndani ya Jumba la UBUNGO PLAZA Jijini Dar - es - salaam linavyo onekana kwa ndani



Banda la maonyesho la the Foundation civvil likiwa ndani ya jengo la Ubungo Plaza jijini Dar - es -salaam

Saturday, November 19, 2011

WAHITIMU WA MAFUNZO YA UDEREVA WA ASWA KUTOKUCHUKUA ABIRIA WENYE MADAWA YA KULEVYA

Kamanda Police Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda amewaasa Madereva kuwa macho na abilia wanao wasafirisha wasikubali kupokea mzigo wasio ujua endapo dereva ata kamatwa na mzigo katika gari lake iwe nyara za serekari au madawa ya kulevya kesi niya dereva aliye kamatwa,pia amewaomba kujiepusha na mwendo wa kasi unasababisha ajali barabarani

Mkuu wa chuo cha VETA Mkoa wa Ruvuma Gidion Olle Lalumbe akitangaza lengo la Veta na kusema lengo la veta kabla ya mwaka huu kumalizika ni kutoa mafunzo kwa madereva wapatao 3000

Mkuu wa usalama barabarani Cerestini Mtaki akiwa kanya madereva walio hitimu kuachana na kutoa rushwa kwa asikari wa usalama barabarani endapo mtu anatoa rushwa basi ajue ana makosa

viongozi wa mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na kamanda wa Police mkoa wa Ruvuma kuliya aliye mbele ni mkuu wa VETA Mkoa wa Ruvuma Gidion Olle Lalumbe mama aliye katikati ni afisa usafiri, na aliye vaa suti ya kanga ni kamanda wa TAKURU Mkoa wa Ruvuma aliye kushoto ni kamanda wa mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda

Mwenyekiti wa Madereva Karimu Hamis Manzi akipokea cheti cha kuhitimu udereva kutoka kwa kamanda wa police mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda

wahitimu wa mafunzo ya udereva Mkoa wa Ruvuma wapatao 67 wakiwa wame piga picha ya pamoja na mgeni rasimi kamanda wa Police Mmkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda

Niwahitimu wapatao 67 ambao wamefanya mtihani wa Udereva katika chuo cha veta Songea hapo wakifikilia jee tuta faulu au la,

Wahitimu wa mafunzo ya udereva katika chuo cha veta wakisikiliza nasaha za mgeni rasimi ambaye alikuwa kamanda wa Police Maiko Kamhanda

SKILL PATH SCHOOL [GREEN VISION KATIKA MAAFALI YA WATOTO WA AWALI KATIKA ENEO LA MSAMALA

Umwonaye hapo juu ni mtoto wa mwandishi wa habari Gereison Msigwa ajulikanaye kwa jina la Wayne Msigwa ambaye katika matokeo ya mtihani wa kufungia shule amekuwa mtu wa pili .mshindi wa kwanza ni Vaileth Nchimbi

Watoto wa Skill Path School wakipokea vyeti vya kuhitimu shule ya awali , skill Path School ina fundisha kwa kutumia kingereza

Mwalimu mkuu wa Skill Path aliye vaa shati la blue omary Hakimu Foum akiwa na Mgeni Rasimi Adam Mbega kutoka Voda Com aliwasihi wazazi kuachana na mambo ya anasa badala yake wasomeshe watoto wao

picha ya chini na picha ya juu ni wahitimu wa shule ya Skill Path wakiwa katika mavazi ya kuhimu masomo ya awali

wanafunzi wa shule ya Skill Path wakiwa na furaha baada ya kuhitimu mafunzo ya shule ya awali

SKILL PATH SCHOOL

Ndugu msomaji wa http://www.songeahabari.blogspot.com/ utaona picha za watoto zina rudia rudia hiyo ni kumpa kila mtoto aliye kuwepo katika maafali aonekane nikimwacha mmoja basi ujue mimi mwandishi nitafute njia ya kupita una wajua watoto wadogo msomaji.