
Kazi kubwa ya wandishi wa Habari ni kuwakilisha kero zinazo wakabili watu wanao ishi pembezoni hapo Adamu Nindi akiwakilisha kilio cha wakulima wa Mkoa wa Ruvuma baada ya Serekali kusitisha ununuzi katika mkoa wa Ruvuma na wananchi kubaki na mahindi ambayo yana hitaji fedha zaidi ya shilingi Bilioni 8 ,Hapo ni katika Tamasha la 9 lililo andaliwa na The Foundation kutasimini na kuangali changa moto zinazo wakabili Watanzania katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru.

Vyombo vya Habari Hivi sasa vimeboreshwa katika kufanikisha kupata habari kwa njia ya Video Camera hapo mpiga picha akichukua picha bila kutumia nguvu kwa kutumia mtambo wa kisasa .

Vyombo mbali mbali Nchini Tanzania vinajitahidi kuelimsha wanachi kwa njia ya Televisheni hapo ni kituo cha Abood TV Mkoani Mrorogoro kikitoa habari kwa wananchi wa kanda ya kati, Hapo Mhariri wa Habari wa Abood Media Juma Kapalatu akihakikisha kila kitu kinaenda sawa

Hicho ni kituo cha Radio cha Abood FM katika mkoa wa Mrorogoro hapo ni wasomaji wa Tarifa ya Habari Wakisoma Tarifa ya Habari

Studio za Abood FM ziko makini katika urushaji wa Habari hapo wanangoja mwongozaji tayari kwa kuwa burudisha watanzania wanao ishi mikoa ya Morogoro,DSM,Iringa,Dodoma
No comments:
Post a Comment