
Hayo ni makaburi ya watakatifu yaliyoko katika eneo la Peramiho katika misheni ya peramiho songea vijijini Makaburi hayo la juu la sister Benedeta na la chini la sister Camilla kwa imani za watu kila siku hufukuliwa udongo wake nawale wenye kuchukua udongo huo hufanikiwa katika shida zao

Mtazamaji unaweza kuona makaburi hayo yanavyo chukuliwa udongo kila siku ya mungu inayo pita kwenye vyupa unavyo viona kuna jazwa maji lakini kila wakati maji huisha ni hivi karibuni sister Benedeta na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wali tangazwa na kanisa katoric kuwa ni wenye heri

Waombelezaji kutoka kila pembe ya Tanzania wakija kuomba kutatuliwa shida zao walizo kuwa nazo kwenye makaburi ya sister Camila na Sister Benedeta Mwenyeheri .

Hilo hapo juu ni kanisa lililo jengwa Peramiho na Wamisionari wa kikatolic miaka mia moja iliyo pita lakini mpaka leo halijanyiwa ukarabati wowote ,pamoja na kanisa hilo ipo saa ambayo nayo ina chukua miaka 100 bila kutengenzwa wala kurekebishwa

Waumini ambao wanaamini kuwa udongo wa makaburi ya Sister Camilla na Sister Benedeta yaliyoko Peramiho yanaweza kusaidia katika matatizo yao hapo wanaonekana wakichukua udongo katika makaburi

Mwandishi mwandamizi mzee Ndimala akiwa mkoani Ruvuma Maeneo ya Peramiho akifaidi matunda yenye radha halisi ya machungwa yaliyo pandwa kiutalamu na wamishenari kutoka Ujerumani
No comments:
Post a Comment