KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, November 18, 2011

KAMANDA WA POLICE MKOAWA RUVUMA AMEWATAKA WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO KUWA WALINZI WA ROHO ZA WATU WAWAPO BARABARANI

Mkurugenzi kutoka nyanda za juu kusini wa VETA Monica Mbele akimkabidhi kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda vyeti tayari kwa kuwa kabidhi wa hitimu wa mafunzo ya pikipiki katika bonde la Agati Langilo Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma


Mkuu wa VETA Mkoa wa Ruvuma Gidioni Olle Lalumbe akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa nyanda za juu kusini Monica Mbele wakiwa katika viwanja vya Langiro Bonde la Agati Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma

Wahitimu wa mafunzo ya pikipiki katika bonde la Agati Mbinga wakiwa na Pikipiki zao mara baada ya kumaliza mafunzo na kukabidhiwa vyeti na Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda


Adam Nindi – Songea

Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda amewataka Vijana wanao endesha vyombo vya moto kuwa makini wawapo barabarani, ulinzi waroho za watu upo mikononi I mwao.

Kamanda wa Jeshi la Police Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamuhanda ameyasema hayo wakati akigawa vyeti kwa wahitimu katika Mafunzo ya Uendeshaji wa Pikipiki uliojumuisha Vijana 90 akiwemo Mwanamke mmoja katika bonde la agati langilo wilayani mbinga mkoani Ruvuma.

Kamanda wa Polisi Kamuhanda amesema Ajali nyingi ambazo zimesababishwa na vyombo vya moto zikiwemo Pikipiki Mkoani hapa zimetokana na Uzembe pamoja na kutozingatia alama za Usalama Barabarani.

Kamanda amesema Vijana wakijiunga na Veta itasaidia kuwaongezea ujuzi wa kuweza kutunza vyombo vya Moto na kuweza kujipatia ridhiki, amewataka waliohitimu kuwa walinzi kwa wezao ambao wanaenda mwendo wa kasi, kupakiza abiria zaidi ya mmoja, wakiona vitendo hivyo waarifu Polisi.

Mkurugenzi wa Veta Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Monika Mbele amesema shabaha ya Serikali kuanzisha VETA ilikuwa kuongeza ufanisi katika kuboresha Ujuzi wa utengenezaji vipuli, kutoa elimu ya ufundi kwa Wananchi juu ya kuboresha biashara ya Usafirishaji na kulinda Vyombo vya Moto. Hivyo ni juu ya Wazazi kuleta vijana wao kujiunga na Veta bila kujali ni Mwanamke au Mwanaume.

Mkuu wa Chuo cha VETA Songea Gideon Olle Lailumbe amesema Mkoa wa Ruvuma una nafasi nyingi za wanafunzi kujifunza, wazazi wasifikiri VETA inapokea wanafunzi waliofeli bali inachukua wanafunzi kuanzia darasa la saba, kidato cha nne hadi kidato cha sita hata chuo kikuu.

No comments:

Post a Comment