KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, April 29, 2012

JAMAMANI TUTOE MAONI ,PLEASE INSERT YOUR COMMENT


SHUKURANI KWA KUTEMBELEA BLOG YANGU

Jambo ambalo napenda kulitoa kwanza ni shukurani zangu za dhati kuona watu wanao soma blog hii ni wengi natoa pongezi kwenu nyote nasema asanteni sana.

Hebu niingie kwenye mada yangu ndugu zangu kusoma ninjia moja yakujiongezea Elimu kujua nini kinaendelea nchini mwetu Tanzania na hapa songea, wewe unaye soma unatakiwa kutoa maoni yako nini nifanye nini niongeze lipi nimesahau watanzania wengi wanamwono wa mbali lakini wana shindwa kutoa mawazo yao wapi watoe sasa na kukaribisha katika blog YALIYO JIRI MKOANI RUVUMA Kwa kuingia www.songeahabari.blogspot.com


Wewe unanapo fungua mtandao huu uta ona mahali pameandikwa COMMENT au kwalugha yetu TOA MAONI eneo hilo unabonyeza kita tokea kisanduku anandika maoni yakohapo halafu peleka mshale palipo andikwa SEND huo ujumbe wako utanifika nawashukuru wote kwa ushirikiano

Saturday, April 28, 2012

MTOTO WA AJABU AZALIWA SONGEA SEHEMU ZA SIRI ZIKIWA KICHWANI



Adam nindi Songea

Mtoto wa ajabu amezaliwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akiwa na sehemu nne za siri za kike na za kiume mbili zikiwa kichwani na mbili zikiwa katika hali ya kawaida.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Mathayo Chanangula amesema Mzazi wa Mama huyo ajulikanaye kwa Jina la Situmai Hausi na Mume wake Said Abdalah wameweza kubahatika kuzaa mara tatu na huyu ni mtoto wa nne .

Mganga Msaidizi Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Mathew Chanangula amesema kuzaliwa kwa Mtoto huyo kuwa katika maumbile hayo yanaweza kutokana na kutumia Madawa Makali wakati akiwa Mjamzito.

Mathew Chanangula amesema waja wazito wengi huharibu mimba kwa kutumia madawa makali wakati mwingine watoto huzaliwa wakiwa na mdomo wa sungura hiyo yote hutokana na kutumia madawa yasiyo ruhusiwa na dakitari.

Mzazi wa mtoto aliyezaliwa katika Maumbile ya ajabu Said Abdalah amewaomba Wataalamu kuweza kumfanyia upasuaji ili mtoto sura yake iwe ya kawaida ,ameomba kuwa hali ya upasuaji silazima ifanyike hapa watalamu wowote wanao ona wana weza kumusaidia mtoto wake wamsaidie ..

Mama Mzazi wa Mtoto wa Kike amesema kinachotakiwa ni kupokea Mapenzi ya Mungu, Nao wuuguzi wa Wodi ya watoto wamesema kutokana na Maajabu ya Mtoto huyo wameamua kumuweka katika Wodi Maalumu ili kupunguza Wimbi la watu kumshangaa Mtoto huyo wauguzi hao wameomba jamii kutoa ushirikiano kwa mzazi wa mtoto huyo kuona hicho ni kitu cha kawaida.

Watu mbalimbali waliofika katika Hospitali ya Mkoa wameomba jamii kujitolea kwa hali na mali ili kumwezesha mtoto huyo kurudi katika hali ya kawaida aidha wame shirikiana na wazazi wa mtoto kuiomba serekari kurudisha hali ya mtoto kuwa ya kawaida .

Friday, April 27, 2012

MTOTO WA AJABU AZALIWA SONGEA SEHEMU ZA SIRI ZIKIWA KICHWANI

Mtoto wa Ajabu aliye zaliwa katika Hospitali ya Songea Mkoani Ruvuma akiwa na sehemu za kike na za kiume Kichwani
Angalia kwa makini kitu unacho kiona kime simama hapo kichwani ni sehemu za siri za Mwanaume
Sehemu za Kawaida nazo zipo katika sehemu mbili za kike na zakiume angalia kwa makini
Unayo ona hapo mbele ni sehemu ya siri ya mwanamke ikiwa ime kaa katika paji la uso
Sasa una weza kuona Vizuri unacho ona kama kidole ni sehemu ya siri ya mwanaume na juu ya Paja la Uso ni Sehemu ya Siri ya Mwana mke mambo hayo yote yametokea katika Hospitatari ya Songea siku mbili zilizo pita, Hivi sasa watu wana miminika kwenda kuona mtoto huyo wa ajabu katika hospitali ya Songea Mkoani Ruvuma

Tuesday, April 24, 2012

SHUKURANI ZIWAENDEE TGNP KWA KUTOA ELIMU MKOANI RUVUMA MATUNDA NI HAYO HAPO CHINI

Kikao kilicho tukuka kikijadili jinsi ya kuweza kutokomeza mauaji mkoani Ruvuma dhidi ya Wanawake

wajumbe mbalimbali kutoka wilaya tano za mkoa wa Ruvuma wakijadili kwa kina changamoto zinazo sababisha mauaji dhidi ya watoto wakike walio chini ya miaka 20Mafundi walio piga bati jengo la police wanawake mkoani Ruvuma wakisalimiana na Mhamasishaji wamichango wa jengo hilo chini ya maelekezo ya TGNP


Juma Nyumayo akielekeza jinsi ya kupiga bati katika jengo la Police Wanawake jijini Songea Mkoani Ruvuma

Mwonekano wa jengo la police wanawake baada ya kuanza kuezeka sehemu ya mbele


WP Mfaume akiwa katika ofisi za Star Tv kuchukua uzoefu dhidi ya kutafuti maswala ya unyanyasaji kijinsia dhidi ya wanawake Mkoani Ruvuma


Wakongwe wa Mtandao wa police wanawake wakipeana mawazo jinsi mkoa wa Ruvuma unavyo ongezeka katika maswala ya vitendo vya kikatili dhidi ya wanake hapo wapo makao makuu ya Police Mkoani Ruvuma

MAENDELEO YA JENGO LA POLICE MKOANI RUVUMA

Ujenzi wa jengo la police wanawake mkoani Ruvuma hivi sasa umekamilika na vihi karibuni jiwe la msingi lina tegemewa kuwekwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu

Mwenyekiti wa Mtandao wa Police wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo akitoa nasaha kwa Police wanawake mkoani Ruvuma


kundi zima la Police wanawake kutoka mkoa wa Ruvuma baada ya kikao katika makao makuu ya Police Mkoani Ruvuma

Mafundi wakiendelea kujenga jengo hilo kwa kumimina bimu

Police wanawake wakiwa katika kikao cha kutathimini ujenzi wa Jengo la Police Wanawake

Jengo la Police Wanawake likiwa lime anza kupanda baada ya usimamizi wa Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda akishirikiana na wadau wa TGNP Mkoa wa Ruvuma Adamu Nindi na Juma Nyumayo

Msingi wa Jengo la Police ukiwa ume anza kujengwa huku mafundi wakisuka nondo kwa ajili ya nguzo

Jengo la Police Wanawake likianza kupimwa huku kamanda wa police Michael Kamhanda akikagua Msingi huo katika eneo la kituo kikuu cha police


Mwanzo wa ujenzi wa Jengo la Police Wanawake mkoani Ruvuma Hapo mafundi wakianza kupima jengo la police wanawake

Monday, April 23, 2012

TANZANIA YA PATA ZAIDI YA DOLA 614 ZA KIMAREKANI KWA AJILI YA USHURU WA TUMBAKU

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma SaidThabit Mwambungu alipo kuwa akifungua semina na Mkutano Mkuu wa Bodi ya Wataalamu Nchini Tanzania Mkutano ulio fanyika Mkoani Ruvuma



Mkuu wa mkoa akiongea na wandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa bodi ya Tumbaku nchini Tanzania

wajumbe wakitasimini jinsi ya kumwinia Mkulima katika zao la Tumbaku


Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Nchini Tanzania Vitta Kawaw a akiongea na Wandishi wa Habari

Wajumbe wa mkutano mkuu wa nchini Tanzania wakiwa katika mkutano mkuu wa kutasimini mafanikio ya zao la Tumbaku ulio fanyika mkoani Ruvuma


Adam Nindi Songea

Zao la tumbaku nchini tanzania limeweza kuingizia serekari kiasi cha dola za kimarekani 614.8 kutokana na ushuru unao tolewa baada ya mauzo ya Tumbaku

Mwenyekiti wa bodi ya tumbaku Nchini Tanzania Mh .Vita Kawawa ameyasema hayo wakati akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu katika semina na Mkutano wa watalamu wa Bodi ya tumbaku kutoka Tanzania Nzima mkutano unao fanyika mkoani Ruvuma kujadili mafanikio na changa moto ya zao la Tumbaku.

Mwenyekiti wa bodi ya Tumbaku Nchini Tanzania Vtta kawawa amese zao la tumbaku ni mkombozi kwa mwananchi wa Tanzania katika kuondokana na umasikini ,hata halmashauri za wilaya zina ongeza kipato kutokana na uuzaji wa tumbaklu kwa miaka miwili mfululizo hali shauri zime weza kupata zaidi bilionni 26 kwa fedha za kitanzania

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akifungua Mkutano huo amesema mkutano huo uelekeze nguvu zake kuwa komboa wananchi wa m,koa wa Ruvuma kufaidi kwa kupata ajira kutokana na kiwanda cha kusindika tumbaku ambacho mpaka sasa kime kaa bila kufanya kazi zaidi ya miaka 10

Wadau wengine wameomba ili kumkomboa mkulima bei ya tumbaku ipande ili iweze kulingana na soko la dunia

Lengo kuu la mkutano huo ni kupandisha kiwango cha uzalishaji kutoka tani 50.000 kwa mwaka 2009 hadi kufikia tani 100,000 kwa. Mwaka 2010 jambo ambalo lime fikiwa kwa kuzalisha tani 126 sawa na asilimia 103 jumula ya watu 187 wamehudhulia mkutano huo wakiwemo wanunuzi na wana chama wa bodi ya tumbaku

Saturday, April 21, 2012

HALIMASHAURI ITAKAYO PATA HATI CHAFU VIONGOZI WAAJIBIKE

PICHA HIZO HAPO CHINI NI PICHA ZA KIKAO CHA AZAKI ZISIZO ZA KISEREKARI KILICHO FANYIKA DODOMA KUJADILI KUHUSU MAFANIKIO YA MKUKUKUTA TWO NA JINSI WANANCHI WAVYO SHIRIKI UANDAAJI WA BAJETI Wajumbe wa Azaki kutoka maeneo mbalimbali kutoka Tanzania Bara wakiwa katika tahtimini ya mafanikio ya Mkukuta TWO na kuangalia jinsi wanchi anavyo husishwa katika bajeti serekari za mtaa
Meneja Mradi wa TANGO Zaa Twalangeti akirabitu maswala ya Mkukuta two na mpango wa Bajeti
Mwana harakati kutoka TGNP Badi akiwa tayari kuwakilisha mada kuhusu mwanachi anavyo takiwa kushirikikuanda bajeti pamoja na kulinda rasilimali za serekari
wana Azaki wakiwa jijini Dodoma waki peruzi mambo mbali mbali yaliyo fanikishwa katika mkukuta two na yale ambayo hayaja fanikiwa

Vikundi mbalimbali vya wana Azaki waki pitia michakato mbali mbali ya kuweza kuisaidia serekari ili iweze kufikisha huduma kwa wananchi

Friday, April 20, 2012

DIWANI KASIMU NTARA ACHUKULIWE HATUA ZA KISEREKARI KWA KUMJAZA MIMBA MWANAFUNZI

Diwani Kasimu Ntara wa kata ya Hanga anaye Tuhumiwa Kumpa mimba mtoto wa mwenyekitti Saidi Kupata huko mliayoyo Namtumbo vijijini


Mwenyekiti wa kijiji cha Mageuzi Saidi Kupata akitoa malalamiko yake kwenye mkutano wa Hadhara alivyo fanyiwa na Diwani Kasimu Ntara

Serikali ya Chama cha mapinduzi Sera zake Mikakati Mikakati yake na kuinua kipato cha Mwananchi wa chini mipango ambayo ikiwa na Usimamizi nzuri haina lawama. Hivi sasa katika Chaguzi zilizopita Baadhi ya Viti vya udiwani na Ubunge vimechukuliwa na Wapinzani.

Jambo hilo haimaanishi Wananchi wamechoka na Chama la ni kuwa Wananchi wamechoka na Viongozi wasio Waadilifu. Mipango mingi inayo panga Seriakali ina makusudi ya kuongeza Utendaji katika Sekta fulani kwa mfano Sera ya Chama cha mapinduzi imeazimia Kila Kata iwe na Sekondari jambo hilo limefanikiwa,

kazi kubwa ipo kwa wasimamizi kuona kama Maswala hayo yana yana patiwa Vitendea Kaz. Nimesema hapo awali kuwa Wananchi hawajachoka na na Chama cha Mapinduzi bali wamechoka na Watendaji, hebu nitoe mfano wa hivi karibuni Seriakali inahimiza Elimu,

Anatokea Kiongozi anampa Mimba Mwanafunzi wa kidato cha Pili katika Kata yake huyo Diwani badala ya kuonywa na kukanywa badala yake anapandishwa cheo na kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri. Jee hapo ukipitishwa Uchaguzi hali inakuwaje.

Diwani huyo ajulikanaye kwa jina la Kasimu Ntara ndiye anayetuhumiwa kufanya Vitendo hivyo ni wazi amezalilisha Mkoa wa Ruvuma na Mbunge wa Jimbo hilo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha mageuzi Said Kapata sasa watu kama hawa wakisha jua wananchi hawawapendi hukimbiliakujiunga na chama fulani ili kuficha maovu yao lamuhimu kama diwani kampa mimba mwanafunzi anaye achukuliwe hatua za kiserekarisasa .

Hebu ona aibu anayo ipata mwenyekiti wa serekari ya mtaa mliayoyo Saidi Kapata baada ya mwanaye kupewa mimba wananchi wanahoji kama mwenyekiti kashindwa kumshitaki diwa Kasimu Ntara mtu mwingine anaweza CCM Tafadhali ondoeni viongozi wachafu ili wananchi warudishe imani kwa serekari na amani iendelee

KITABU CHA USALAMA BARABARANI KAMA KINAVYO ONEKANA

Ndugu msomaji wa blog hii tumesema Jeshi la Police lihakiki kitabu hiki kwa kuwa katika ukurasa huu utaona ikieleza kuwa kamanda wa police Ruvuma ni Mshana wakati kamanda ni Michael Kamhanda

kitabu cha safiri salama nikitabu ambacho kimekuwa mkombozi kwa wasafiri Dereva akizidisha sipidi kulikuwa na uwezekano wa kupiga kwa Kamanda wa Police na Asikari wa usama barabarani walio mbele huweza kumsimamisha Dereva na kupewa onyo lakini sasa ukipiga asikari wengi wame stahafu

JESHI LA POLICE LINATAKIWA KUHAKIKI KITABU CHA USALAMA BARABARANI

Jeshi la police nchini tanzania lina takiwa kuhakiki vitabu wanavyo wapa wanachi kwa ajili ya usalama wao wakiwa safarini. Kwanza nalipongeza jeshi la Police kwa kuweza kujali hali za wananchi wa Tanzania kwa kusambaza vitabu vya usalama zikiwa na majina ya wakuu wa Police mikoa yote pamoja na wakuu wa upelelezi mikoa yote.

sasa kinacho watatiza wananchi kila wanapo piga namba zilizopo inaonyesha kuwa wakuu wengi walikuwa katika kitabu hicho wame sitahafu  tungeomba kwakua kitabu hicho ni mhimu tungeomba kitabu hicho kitengenezwe tena upya
PICHA HIYO HAPO CHINI NI DIWANI ANAYE TUHUMIWA KUMPA MIMBI MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI KATIKA SECONDARI YA MAGEUZI Serikali ya Chama cha Mapinduzi, Sera zake, Mikakati yake ya kuinua kipato cha Mwananchi wa chini ni mipango ambayo ikiwa na usimamizi Mzuri haina lawama.

Hivi sasa katika chaguzi zilizopita Baadhi ya Viti vya Udiwani na Ubunge vimechukuliwa na Wapinzani.

Jambo hilo haimaanishi Wananchi wamechoka na chama la ni kuwa Wananchi wamechoka na Viongozi wasio waadilifu.
Mipango mingi inayopanga Serikali ina makusudi ya kuongeza Utendaji katika sekta fulani kwa mfano sera ya chama cha Mapinduzi imeazimia kila kata iwe na Sekondari jambo hilo limefanikiwa, kazi kubwa ipo kwa wasimamizi kuona kama maswala hayo yanapatiwa vitendea kazi.

Nimesema hapo awali kuwa wananchi hawajachoka na Chama cha Mapinduzi bali wamechoka na Watendaji, hebu nitoe mfano wa hivi karibuni, Serikali ina himiza Elimu anatokea Kiongozi anampa Mimba Mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Kata yake huyo ni Diwani badala ya kuonywa na kukanywa badala yake anapandishwa cheo na kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri.

Jee hapo ukipitishwa Uchaguzi hali inakuwaje.

Diwani huyo ajulikanaye kwa jina la Kasimu Ntara ndiye anayetuhumiwa kufanya Vitendo hivyo ni wazi amedhalilisha Mkoa na Mbunge wa Jimbo hili Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mageuzi Said Kapata.

Sunday, April 15, 2012

Makamu wa Rais Mh.Mohamed Bilali akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia jenereta wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma , Jee hali hii ya kufungua majenereta ita isha lini ?



Adam Nindi, Songea
Tanzania kila wakati imekuwa katika swala la kukabiliwa na Matatizo ya Umeme.

Jambo hilo lilisababisha mpaka kipenzi cha Watanzania ajihudhulu Uwaziri Mkuu ili kuwa ridhisha Watanzania ni Ushujaa huo hakuna ambaye anaweza kujihudhuru kwa Maslahi ya Watanzania.

Swala la Umeme limekuwa Tatizo kwa Watanzania, Viongozi wamesikika wakisema kuwa tutamaliza Tatizo la Umeme kwa kutumia Nishati ya Gesi.

Tunajua kuwa hayo yote ni Juhudi za kumkomboa Mtanzania, Jee sisi Watanzania hutuna Rasilimali ambazo zinaweza kusaidia kupata Umeme.?

Hebu tuone wenzetu wana pata Umeme kwa kutumia Victorfall sasa sisi hapa Mkoani Ruvuma tuna Maporomoko ya Maji Nakatuta njia ya kwenda Msumbiji Muhukuru Songea Vijijini.

Tuna Madini ya Urenium Namtumbo Mkoani Ruvuma , Pia tuna Makaa ya Mawe yaliyoko Kata ya Rwanda Kijiji cha Ngaka Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma.

Nini kinatufanya tushindwe kutatua Mgogoro wa Tatizo la Umeme ndugu msomaji hapo nimezungumzia mkoa mmoja tu wa Ruvuma baki ya Mikoa mingine 23 iliyobaki.

Watanzani pale tulipo tusiwe na kawaida ya kulaumu bali tuishauri serekari na kupaze sauti zetu ili serekari itafute njia mubadala ya kumaliza swala la umeme kwa kutumia rasilimali tulizo nazo

SWALA LA UMEME LIME KUWA KITENDAWILE HAPA TANZANIA HEBU TUONE NIKWELI HAKUNA UWEZEKANO WA KUPATA UMEME WA UHAKIKA ?

Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea mkoani Ruvuma kitu kilicho mvutia ni kusikia kuwa tuna Makaa ya Mawe kiasi cha tani milioni 400 na pia makaa hayo yana uwezo wa kuzalisha umeme MG 400 umeme ambao una weza kupunguza tatizo la umeme Tanzani pia Makamu wa Rais Mohamed Bilali aliambiwa mkoa wa Ruvuma unaweza kupata Umeme MG 120 muda wowote bora idhini itolewe na Tanesco jee nani akumbushe swala hili wakati Makamu alisha kubali


Mkurugenzi wa NDC aliye hapo juu alisha fanya jitihada za kuonana na uongozi wa Tanesco lakini alipiga chini sasa baada ya kukubaliwa na Makamu wa Rais kinacho takiwa ni kumpa nguvu ya kuanza kufanya mipango yakinifu ili umeme uingie Songea

Mwekezaji huyo kutoka kampumni ya TANCOAL amesema yeye anacho ngoja ni serekari ya Tanzania kutia saini maombi ya kusambaza umeme ili wao waweze kupata fedha na kuanza kujenga njia za umeme,


Hapo ni viongozi wawili wa kubwa katika mkoa wa Ruvuma wakibadilishana mawazo ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Said Mwambungu na Mbunge wa jimbo la songea Mh.Emanuel John Nchimbi sasa hatujui kama wana zungumuza kuhusu umeme au............... Wawekezaji wa kampuni ya TANCOAL akiwepo Emanuel Consitatino akibadilishana mawazo na Greison Msigwa wa TBC Songea wakiwa Ngaka wilayani Mbinga


Makamu wa Rais Mohamed Bilali alipo tembelea Machimbo ya Makaa ya Mawe katika kijiji cha Ngaka wilayani Mbinga hapo ana salimiana na viongozi wa TANCOAL Makamu wa Rais akiendelea kusalimiana na Viongozi wa TANCOAL Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma



Kupata umeme ni swala la kawaida hebu ona makaa yanayo chimbuliwa tuna uuwezo hata wa kutengeneza simenti hata mbolea kwa kutumia mali gafi tuliyo nayo kilicho baki ni watalamu kujituma.
Msomaji Makaa hayo ni bora kuliko yote hapa Africa .hakuna Makaa kama haya hapa Africa ni juu ya viongozi kuajibika kuya fanyia kazi ,Hebu ni kupe siri Makaa yaliyopo kijiji cha ngaka yalikuwa ya kiungua kwa moto kwa kipindi cha miaka mitatu lakini mimi Adamu Mzuza Nindi nilipiga kelele kwenye vyombo mbali mbali vya Habari mpaka serekari ili zima moto huo kwa gharama ya shilingi milioni 59 sasa zamu ni yako wewe

Saturday, April 14, 2012

MAWAZIRI WAKUU WAZURU KABURI LA KIPENZI CHA WATANIA HAYATI MORINGE SOIKOINE



Moja ya kukumbuka kazi za Viongozi walio tangulia mbele za haki ni kuwaombea na kudhuru makabuli yao Hapo waziri msitahafu Edward Luwasa akiwa Morogoro kwa ajili maombi malumu ya Hayati waziri mkuu Edward Moringe Sokoine

Waziri mstahafu Edward Luwasa akiendelea kutoa baraka zake kwa waziri Mkuu aliye mwachia madaraka Mh. Mizengo Pinda walipo kuwa waki mkumbuka Hayati waziri mkuu kipenzi cha watu Edward Moringe Sokoine ambaye alifaniwa ibada marumu na askofu Tekphor Mkude