Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea mkoani Ruvuma kitu kilicho mvutia ni kusikia kuwa tuna Makaa ya Mawe kiasi cha tani milioni 400 na pia makaa hayo yana uwezo wa kuzalisha umeme MG 400 umeme ambao una weza kupunguza tatizo la umeme Tanzani pia Makamu wa Rais Mohamed Bilali aliambiwa mkoa wa Ruvuma unaweza kupata Umeme MG 120 muda wowote bora idhini itolewe na Tanesco jee nani akumbushe swala hili wakati Makamu alisha kubali
Mkurugenzi wa NDC aliye hapo juu alisha fanya jitihada za kuonana na uongozi wa Tanesco lakini alipiga chini sasa baada ya kukubaliwa na Makamu wa Rais kinacho takiwa ni kumpa nguvu ya kuanza kufanya mipango yakinifu ili umeme uingie Songea
Mwekezaji huyo kutoka kampumni ya TANCOAL amesema yeye anacho ngoja ni serekari ya Tanzania kutia saini maombi ya kusambaza umeme ili wao waweze kupata fedha na kuanza kujenga njia za umeme,
Hapo ni viongozi wawili wa kubwa katika mkoa wa Ruvuma wakibadilishana mawazo ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Said Mwambungu na Mbunge wa jimbo la songea Mh.Emanuel John Nchimbi sasa hatujui kama wana zungumuza kuhusu umeme au...............
Wawekezaji wa kampuni ya TANCOAL akiwepo Emanuel Consitatino akibadilishana mawazo na Greison Msigwa wa TBC Songea wakiwa Ngaka wilayani Mbinga
Makamu wa Rais Mohamed Bilali alipo tembelea Machimbo ya Makaa ya Mawe katika kijiji cha Ngaka wilayani Mbinga hapo ana salimiana na viongozi wa TANCOAL
Makamu wa Rais akiendelea kusalimiana na Viongozi wa TANCOAL Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma
Kupata umeme ni swala la kawaida hebu ona makaa yanayo chimbuliwa tuna uuwezo hata wa kutengeneza simenti hata mbolea kwa kutumia mali gafi tuliyo nayo kilicho baki ni watalamu kujituma.
Msomaji Makaa hayo ni bora kuliko yote hapa Africa .hakuna Makaa kama haya hapa Africa ni juu ya viongozi kuajibika kuya fanyia kazi ,Hebu ni kupe siri Makaa yaliyopo kijiji cha ngaka yalikuwa ya kiungua kwa moto kwa kipindi cha miaka mitatu lakini mimi Adamu Mzuza Nindi nilipiga kelele kwenye vyombo mbali mbali vya Habari mpaka serekari ili zima moto huo kwa gharama ya shilingi milioni 59 sasa zamu ni yako wewe
No comments:
Post a Comment