PICHA HIYO HAPO CHINI NI DIWANI ANAYE TUHUMIWA KUMPA MIMBI MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI KATIKA SECONDARI YA MAGEUZI Serikali ya Chama cha Mapinduzi, Sera zake, Mikakati yake ya kuinua kipato cha Mwananchi wa chini ni mipango ambayo ikiwa na usimamizi Mzuri haina lawama.
Hivi sasa katika chaguzi zilizopita Baadhi ya Viti vya Udiwani na Ubunge vimechukuliwa na Wapinzani.
Jambo hilo haimaanishi Wananchi wamechoka na chama la ni kuwa Wananchi wamechoka na Viongozi wasio waadilifu.
Mipango mingi inayopanga Serikali ina makusudi ya kuongeza Utendaji katika sekta fulani kwa mfano sera ya chama cha Mapinduzi imeazimia kila kata iwe na Sekondari jambo hilo limefanikiwa, kazi kubwa ipo kwa wasimamizi kuona kama maswala hayo yanapatiwa vitendea kazi.
Nimesema hapo awali kuwa wananchi hawajachoka na Chama cha Mapinduzi bali wamechoka na Watendaji, hebu nitoe mfano wa hivi karibuni, Serikali ina himiza Elimu anatokea Kiongozi anampa Mimba Mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Kata yake huyo ni Diwani badala ya kuonywa na kukanywa badala yake anapandishwa cheo na kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri.
Jee hapo ukipitishwa Uchaguzi hali inakuwaje.
Diwani huyo ajulikanaye kwa jina la Kasimu Ntara ndiye anayetuhumiwa kufanya Vitendo hivyo ni wazi amedhalilisha Mkoa na Mbunge wa Jimbo hili Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mageuzi Said Kapata.
No comments:
Post a Comment