Hayo yamebainika wakati Naibu Waziri wa Elimu Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akisomewa
taarifa ya chakula kilichotolewa Mkoani Ruvuma kusaidia mikoa mingine yenye
uhaba wa chakula Tanzania.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi
Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa
katika hifadhi ya chakula Songea kununua Tani 5 za Mahindi kwa ajili ya wananchi wake
waliopata Maafa ya Mafuriko katika Jimbo la Nyasa.
Meneja wa Kitengo cha hifadhi ya Chakula (NFRA) Songea Amos Mtafya akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Elimu amesema katika kipindi cha 2015 – 2016 Hifadhi ya Chakula Songea imeweza kusafirisha Tani 88,000 kwa mikoa ya Tanzania bara yenye Upungufu wa chakula na Tani 10,000 kwa Shirika la chakula Duniani (Word Food Program– WFP) na Tani 8,000 kuhamishiwa katika Hifadhi ya Dodoma na Tani 5 kununuliwa kwa ajili ya watu waliopatwa na maafa jimbo la Nyasa na kitengo kimebakiwa na tani 11,000
Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya amesema miundombinu ya barabara na usafiri wa majini Serikali imeweza kusaini Mkataba wa kutengeneza Barabara ya Kitahi - Lituhi na Mbinga hadi Mbamba bay kwa kiwango cha lami.(Picha Gari ya Naibu Waziri ikiwa imenasa katika Tope akiwa ziarani Jimbo la Nyasa)
Nao wananchi wanaoishi vijijini wametakiwa kufuatilia kwa
ukaribu Miradi inayofadhiliwa na Serikali, Miradi inayofanyika vijijini
inatakiwa kuwa imara kusiwe na visingizio vya kujenga miradi chini ya kiwango
kwa kudai ni miradi ya vijijini.
Mhandisi Stella Manyanya ameyasema hayo baada ya kuona Mradi wa ukarabati wa Kituo cha Afya cha kata ya Linga Wilayani Nyasa uliogharimu shilingi Milioni 27 simenti ya sakafu ikionyesha imepasuka kabla ya kumaliza mwaka mmoja.
Mhandisi Stella Manyanya
amesema hakuna kisingizio cha kukarabati ovyoovyo miradi ya Vijijini na
kusingizia miradi ya vijijini inatakiwa kulipua Wananchi wawe macho katika
kusimamia miradi hiyo.(Pichani Mhandisi Stella Manyanya akikagua ukarabati wa Kituo cha Afya Litumba Kuhamba Kata ya Linga.)
Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya amesema
katika Jimbo la Nyasa kutakuwa na mashindano ya ufaulu kubaini shule gani
imefaulisha vizuri, mwalimu atakayeshindwa kufaulisha vizuri wanafunzi itambidi
apishe nafasi hiyo ichukuliwe na wenzake watakaoweza kufundisha vizuri.Mh
mhandisi Stela Manyanya ametoa agizo kiloa shule iwe na shamba darasa kwa ajili
ya somo la kilimo
Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya akizungumza kuhusu Sekta ya Elimu amesema katika Tanzania kuna vyuo vikuu zaidi ya 50 na chuo kingine cha Madaktari bingwa wa Moyo na Mishipa ya Damu kinajengwa Mlogazila Dar Es Salaam ambacho kitachukua wanafunzi 15,000 wa fani ya Udaktar
Mhandisi Stella Manyanya amesema Serikali katika kuinua
uchumi wa Watu wanaoishi Mwambao wa Ziwa Nyasa tayari mkataba wa kutengeneza
Barabara ya Mbinga
MbaMba Bay
umeshatiwa sahihi kwa ujenzi wa kiwango cha lami.
Naibu Waziri wa Elimu amewahimiza Wazazi kutoa ushirikiano
kwa Serikali kwa kuboresha Elimu katika mambo yanayowahusu wazazi , kama kutoa chakula kwa watoto, Madawati pamoja na kuboresha
eneo la kusomea.
Wananchi wa Maeneo yaliyopatwa na Maafa ya Mafuriko wamemshukuru
Mweshimiwa Mbunge kwa kuweza kukimbia Jimboni na kutoa pole kutokana na Maafa
yaliyowapata.
Akiongea na Wananchi wa Jimbo la Nyasa Mh. Naibu Waziri wa
Elimu amesema ili uweze kuingia katika Vyuo hivyo unahitajika kufaulu vizuri
kwa kupata Daraja la kwanza (Division One).
Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu amesema pamoja na
kurahisisha mawasiliano ya usafiri katika Ziwa Nyasa, pia ujenzi wa Bandari ya
Ndumbi unaendelea, na meli tatu
zinaundwa, mbili zikiwa za mizigo na moja ya Abiria ambazo zitasaidia
kusafirisha mizigo na Abiria kutoka Mbeya hadi Mbamba Bay.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi Mhandisi Manyanya amesema wako watu wachache ambao wanawakatisha tamaa
wenzao kuhusu Elimu, lakini watu hao ni wa kuwapuuza jambo muhimu kwa wazazi ni
kutoa ushirikiano kwa Walimu kwa kuboresha Mazingira kwa kujenga Nyumba nzuri
za walimu.
Mheshimiwa Stella Manyanya alikuwa katika Ziara ya siku mbili
katika Jimbo la Nyasa kwa ajili ya kutoa pole kwa wananchi waliopatwa na Maafa
ya kukumbwa na Mafuriko.
No comments:
Post a Comment