Kaya 144 zimekosa
mahali pakuishi katika Kijiji cha
Ngadinda Kata ya Gumbilo wilaya ya Songea vijijini baada ya nyumba 51 kubomoka
na nyumba 91 kutetereka baada ya mvua kali kunyesha mfululizo muda wa siku tatu mfululizo
Mkuu wa wilaya ya
songea Bensoni Mpesya amesema licha ya nyumba kubomoka mvua pia imeathiri
mashamba yapatayo hekari 102 za nafaka
mbalimbali zikiwemo mahindi mpunga na maharage
Kufikia maeneo yenye maafa kunataka moyo hapo Gari la Mkuu wa wilaya ya Songea Bensoni Mpesya likiwa lime kwama na kusababisha mkuu huyo kutembea kwa mguu kukagua maeneneo yaliyo athirika katika kata ya Gumbiro
Mkuu wa wilaya ya Songea Bensoni Mpesya amesema maafa yaliyo
tokea yametokea baada ya mto Hanga kufurika na kusababisha hasara kubwa lakini
kamati ya maafa ya wilaya imejipanga kusaidia familia hizo katika ujenzi,
chakula kipo cha kutosha
Mkuu wa wilaya ya songea Benson Mpesya amewaomba wananchi wa
Songea ili kuepukana na majanga ya kubomokewa na nyumba wajaribu kufuata
ushauri wa wahandisi wakati wa ujenzi, nyumba nyingi hubomoka kwa kukosa misingi
imara
No comments:
Post a Comment