Kamanda wa kikosi cha kuzuia Rushwa mkoa wa Ruvuma Yunisitina Chagala amesema jumula ya tarifa 82 zimewakilishwa katika ofisi yake zikiwa na malalamiko mbalimbali yakiwemo migogoro ya Aridhi, Afya,miradi ya miundo mbinu .Amesema kise moja iliyo kuwa ikihusu baraza la kata Namtumbo mwenyekiti na katibu wake wa baraza la kata Namtumbo ametiwa hatiani
kamanda wa TAKUKURU amesema changamoto zinazo patikana kushindwa kutekeleza majukumu ni kutokana na wananchi kuto toa ushirikiano pale panapo hitajika ushahidi ameomba waandishi wa habari kusaidia kutoa tarifa zinazo husiana na Rushwa
Waandishi wahabari wameambiwa waache kupaka matope wafanyakazi wa TAKUKURU kuhusika na Rushwa bila kuwa na uthibitisho wa swala hilo endapo kuna Mwandishi anajua kuna Rushwa ina tendeka basi atoe tarifa mara moja kwa wahusika
waandishi waqliuliza kuhusu kesi zinaqzo husu vigogo kwanini hazi fikii mwisho na baadala yake kufanyiwa upeleleze zaidi ya miaka 7 .Mkuu wa TAKUKURU amesema kuna kesi ambazo zina takiwa maamuzi ya kutoka juu ndiyo jambo linalo leta usumbufu
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma akijibu swali la mwandishi kutoka mbinga nini hatima ya gari la taka lililo nunuliwa na Halimashauri ya Mbinga amesema uchunguzi una fanywa ili kujua tenda ya manunuzi ili fanyika kwa kufuata sheria majibu sahihi yata tolewa baada ya kumalizika kwa uchunguzi
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa ruvuma amesema wilaya inayo ongoza katika maswala ya rushwa ni wilaya ya mbinga ambayo yana husu zaidi swala la Manunuzi
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yusitina Chagaka amesema kwa muda wa miezi mitatu sasa ofisi yake imesha toa elimu kwa wananchi wapatao 4300
waandishi waq habari mkoa wa Ruvuma wameiomba tasisi ya kuzuia Rushwa kupitia habari zinazo tolewa na waandishi wa habari ili ziwe chazo cha kubaini kufuka kwa rushwa
Katika kikao hicho waandishi wa habari wameomba kufanyike semina ya kuzuia Rushwa kwa Mikoa ya Nyanda za juu kusimi ikiwepo mikoa ya Mbeya,Njombe,Iringa,na Ruvuma
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma amesema Rushwa ni swala gumu kulibaini Mwananchi wa kawaida endapo ata toa ushirikiano basi Rushwa ita weza kufikia kikomo. Ameomba wananchi pamoja na waandishi wa Habari kuwa kitu kimoja ili kuweza kuisaidia TAKUKURU kukamata wale wote wanao husika na Rushwa na kuwapeleka Mahakamani
No comments:
Post a Comment