Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe Anatory Choya
amewataka watu wanaotoa huduma ya Msaada wa kisheria kutumia taaluma yao kwa kutoonyesha
mgogoro katika Jamii bali wajikite katika kutatua Migogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mkoani njombe ametoa Agizo hilo
baada ya kuona kazi zilizofanywa na wasaidizi wa Kisheria kupitia Shirika
Mashirika ya PADI na SOPCE kwa kutoa Elimu kwa Wananchi 59,876 na kutoa Mafunzo
kwa Watoa huduma ya msaada wa kisheria 75 waliopo wilaya za Ludewa, Makete na
Uwanging`ombe Mkoani Njombe.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Edward
Haule amewaomba watoa Elimu ya kisheria kwa jamii kuwa na mawasiliano ya karibu
na Ofisi ya Mwenyekiti wa halmashauri ya Ludewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa ili
wanapotaka msaada waweze kupewa badala ya kulalamika mitaani.
Katika Tathmini ya katikati ya mradi katika kipindi cha miezi 15 iliyolenga kujua Mafanikio yaliyopatikana katika
muhula wa kwanza, changamoto kubwa iliyojitokeza ni vitendea kazi katika
Ofisi za wasaidizi wa kisheria kama Meza, Viti na vyombo vya usafiri
ingawa Mradi umetoa viti vinne na meza moja kila ofisi ya wilaya pamoja na
matumizi ya Stationaries Shilingi 20,000 kwa kila mwezi katika kipindi cha utekelezaji wa mradi.
Akiongelea Mafanikio ya Utoaji wa Msaada wa Kisheria Mkurugenzi wa Shirika la PADI amesema, Wanawake ambao walikuwa wakinyanyaswa kijinsia sasa wamepata Elimu ya
kujitambua ikiwemo na mambo ya Ndoa na masuala ya migogoro ya mashamba.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa amesema Wilaya ya Ludewa ni wilaya
ambayo kijiografia imekaa kwa kuzungukwa na Milima, hivyo kwa jinsi mazingira hayo siyo rahisi Serikali kuwafikia wananchi wote lakini kwa kushirikiaana na
Shirika la PADI na SOPCE kwa kuwatumia watu wa msaada wa kisheria wameweza kupunguza
masuala madogo madogo ambayo yalitakiwa kutatuliwa na mabaraza ya Kata,
Mahakama za Mwanzo na Ofisi ya Mkuu wa wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya
Ludewa kutoa ushirikiano kwa watu wanaotoa huduma ya msaada wa Kisheria katika
Wilaya ya Ludewa kwa kuwapa Ofisi, kusaidia usafiri wanapokwenda vijijini
kikazi pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na wasaidizi wa kisheria na wananchi
kwa ujumla.
Wadau wa Masuala ya kisheria wamepongeza uwepo wa wasaidizi wa kisheria katika ngazi za chini kutokana na kukithiri kwa kesi za masuala ya ndoa, mirathi unyanyasaji wa kijinsia na masuala ya Ardhi ambazo wananchi walikosa fursa za kuyafikia mabaraza ya kata kutokana na kutojua sheria ama kwa kukosa fedha za kufungulia jalada mahakamani au kwenye mabaraza.
Katika Mila za wakinga na wabena wilaya ya Makete Mwanamke akijifungua hakuruhusiwa
kulala juu ya kitanda pia hatakiwi kushiriki na Jamii chakula anachokula Mama
aliyejifungua kikibaki ni lazima kimwagwe, kikiliwa kitaweza kuleta nuksi.
Jambo jingine Mama aliyejifungua haruhusiwi
kulala Kitandani bali anatakiwa kulala juu ya nyasi ndogo ndogo na zitandikwe
chini. Lakini hayo yote baada ya kupata Elimu ya msaada wa kisheria yametoweka ambapo Wilaya ya Ludewa wananchi 23496 wamefikiwa na elimu hiyo.Wasaidizi wa msaada wa kisheria wameomba watendaji kuwapa ushirikiano pindi wanapokuwa vijijini wakitoa Elimu ya kisheria au kusuluhisha migogoro katika jamii.
Changamoto zingine zinazowakabili wasaidizi wa kisheria ni kukosa ushirikiano wa watendaji, kesi
zote za migogoro ya Ardhi, Ndoa na misaada mingine hutatuliwa bure na watu wa
msaada wa kisheria tofauti na Mabaraza ya Kata na watendaji ambao huomba
chochote kwa wanaowatolea huduma.
Mratibu wa Mradi wa msaada wa Kisheria Wilaya za ludewa,
Uwanging`ombe na Makete Mkoani Njombe Recho Steven amesema changamoto
wanazokutana nazo wasaidizi wa kisheria ni pamoja na umbali wa maeneo ya kutoa
msaada, mara zote hulazimika kutembea umbali wa kilomita hadi 30 kwa mguu.
Changamoto zingine ni kukosa ushirikiano wa watendaji, kesi
zote za migogoro ya Ardhi, Ndoa na misaada mingine hutatuliwa bure na watu wa
msaada wa kisheria tofauti na Mabaraza ya Kata na watendaji ambao huomba
chochote kwa wanaowatolea huduma.
Jambo ambalo linaloongeza chuki na watendaji kuona sasa
hawapati kesi za migogoro ya Ndoa, Mashamba na Mirathi baada ya wasaidizi wa
kisheria kutoa Elimu ya kisheria na Jamii kujua huduma za kisheria ni bure.
Kutokana na Elimu inayoendelea kutolewa na wasaidizi wa kisheria katika wilaya za Makete, Ludewa na Uwanging`ombe migogoro ya Ardhi na kesi za ndoa zimepungua baada ya wananchi kufahamu haki zao na uelewa juu ya masuala ya kisheria.
Mratibu wa mradi wa kutoa Elimu ya Msaada wa Kisheria
amesema watoa msaada kisheria walikuwa 75 lakini kutokana na changamoto za
kujitolea watu wane walishindwa kuendelea na Mafunzo ya siku 25 yaliyotolewa na
Shirika la PADI kwa kushirikiana na Shirika la SOPCE kwa ufadhili wa LPF.
No comments:
Post a Comment