Mratibu wa Mradi wa msaada wa Kisheria Wilaya za ludewa,
Uwanging`ombe na Makete Mkoani Njombe Recho Stiven amesema changamoto
wanazokutana nazo wasaidizi wa kisheria ni pamoja na umbali wa maeneo ya kutoa
msaada, mara zote hulazimika kutembea umbali wa kilomita hadi 30 kwa mguu.
Mratibu wa mradi wa kutoa Elimu ya Msaada wa Kisheria
amesema watoa msaada kisheria walikuwa 75 lakini kutokana na changamoto za
kujitolea watu wane walishindwa kuendelea na Mafunzo ya siku 25 yaliyotolewa na
Shirika la PADI kwa kushirikiana na Shirika la SOPCE kwa ufadhili wa LPF.
Shirika la PADI kwa kushirikiana na Shirika la SOPCE wamewezesha kuwafikia watu zaidi ya 4000 kupata elimu ya sheriria kupitia wasaidizi wa kisheria 22 waliopata Elimu ya msaada wa kisheria kutoka wilaya ya Uwanging`ombe katika masuala ya miradhi ya ndoa na masuala ya Ardhi ambayo wasaidizi wa kisheria wamekuwa wakisuluhisha na kupunguza migogoro katika jamii.
Mkufunzi wa Elimu ya Kisheria kutoka shirika la Songea Paraligal Center (SOPCE) Fatuma Misango amesema Mradi umeweza kufadhili kutoa Elimu kwa watoa huduma ya kisheria kwa lengo la kusaidia kujengea uwezo wa kujisimamia jamii inapopata migogoro ili kujua haki zao kinachotakiwa wadau kuunga mkono juhudi za mashirika yanayowawezesha wananchi kwenye maeneo yao.
Watoa huduma ya kisheria Wilaya ya Uwanging`ombe wamewezeshwa kupata chumba cha Ofisi ya wilaya katika Kijiji cha Igwachanya ambayo mradi unagharamia ukarabati, changamoto wanayoipata katika utendaji kazi ni kukosa usafiri wa kuwatoa toka eneo moja kwenda nyingine kutoa Elimu ya kujenga uelewa wa kisheria.
Changamoto nyingine ni kukosa muda wa kutosha wa kutoa Elimu kwa wananchi kwa kuwa mikutano wanayotumia kutoa Elimu ya sheria huandaliwa na uongozi wa Serikali ambapo wao hupewa nafasi ya dakika tano mpaka kumi kutoa elimu jambo ambalo huwalazimu kuelezea juu juu ikizingatia masuala ya sheria yanahitaji muda wa kutosha kuelimisha jamii mpaka ielewe.
Changamoto nyingine hujitokeza pindi wanapopita vijijini kutoa Elimu ya sheria baadhi ya maeneo hudaiwa vitambulisho pamoja na kuwa walishajitambulisha kwenye maeneo yao, hivyo wameomba Mradi au Serikali kuangalia uwezekano wa kuwapa vitambulisho ili waweze kuafanya kazi kwa uhuru.
Mkurugenzi wa PADI Iskaka Msigwa amesema kazi zote
zinazofanywa na watu wa msaada wa kisheria ni kazi za kujitolea ambazo zilitakiwa kufanywa na Serikali lakini Shirika limesaidia kupunguza majukumu ya Serikali, hivyo wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Serikali washirikiane kuweza kuwasaidia vitendea kazi kwenye maeneo yao ili waweze kufanikisha shughulia zao.
Pamoja na changamoto mbalimbali kujitokeza watoa huduma ya msaada wa kisheria wamefanikiwa kutatua migogoro ya Mashamba na ya kifamilia kwa njia ya usuluhishi ambapo baadhi ya kesi zilifika katika mabaraza ya kata na hazikupata suluhu lakini kwa kutumia wasaidizi wa kisheria wameweza kusuluhisha kwa kutoa Elimu ya sheria na kila mmoja kutambua kosa lake.
Mkurugenzi wa PADI Iskaka Msigwa amesema ni muhimu kuwatumia wasaidizi wa kisheria kwa kuwa wanatoa Elimu ya jinsi gani sheria inataka na jamii ikipata Elimu inabadilika na migogoro inapungua katika maeneo yao tofauti na kupeleka Mahakamani ambako hakuna nafasi ya kutoa Elimu bali Mahakama hutafsiri sheria.
Shirika la PADI linafanya kazi katika Wilaya za Ludewa, Makete, Uwanging`ombe na Njombe Mkoani Njombe na wilaya za Songea Vijijini Namtumbo na Songea Mjini Mkoani Ruvuma, Wema Sanga ni Miongoni mwa watendaji wa Shirika la PADI Ofisi ya Njombe akiratibu shughuli za Mradi wa Elimu ya Msaada wa Kisheria kwa wilaya za Ludewa na Uwanging`ombe.
Wadau wa Msaada wa kisheria wamesema wamenufaika na uwepo wa wasaidizi wa kisheria kwenye maeneo yao kwa kuwa kabla ya uwepo wao migogoro yote imekuwa ikisuluhishwa na watendaji, wenyeviti na mabalozi ambao hutatua pasipo kuelimisha kisheria bali hutumia mamlaka yao lakini kwa sasa balozi anapopata suala linalohitaji ufafanuzi wa kisheria huwatumia watoa huduma ya msaada wa kisheria kutoa elimu ya sheria kabla ya kuamua.
Watoa huduma ya msaada wa kisheria wilaya ya Uwanging`ombe wakiwa katika picha ya pamoja na wadau na watendaji wa Shirika la PADI na SOPCE wilayani Uwanging`ombe.
Katika Tathmini ya Mradi wa Elimu ya Msaada wa Kisheria kumekuwa na mafanikio makubwa ambapo uelewa wa jamii umeongezeka juu ya masuala ya kisheria ambapo zaidi ya kesi 50 zimeamuliwa kwa wilaya zote za mradi pamoja na kuwa wasaidizi baadhi ya maeneo wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kutopata ushirikiano nzuri kutoka kwa wadau.
Changamoto kubwa iliyojitokeza ni kukosa vitendea kazi katika Ofisi kama Meza, Viti na usafiri ingawa Mradi umetoa viti vinne na meza moja kila ofisi ya wilaya pamoja na matumizi ya Stationaries Shilingi 20,000 kila mwezi, kwani huduma hii inatolewa kwenye kila Kata.
Wadau wameazimia kuendelea kuwapa ushirikiano wasaidizi wa kisheria kwa kuwasaidia usafiri wanapokuwa na shuhuli za kufuatilia miradi ya maendeleo vijijini kuwachukua na watoa huduma ya kisheria wakatoe Elimu kinachotakiwa ni wao kuwa na mawasailiano ya karibu na Viongozi wa Halmashauri kwenye maeneo yao.
Elimu ya Masuala ya kisheria imeweza kuwafikia watu wengi kwenye eneo la Mradi kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya adhara kwenye mikusanyiko ya dini na kupitia Redio za Kitulo FM, Green FM na Kings FM ambapo watoa huduma ya msaada wa kisheria wameweza kutoa elimu ya sheria ya Aridhi, Mirathi, Sheria ya Ndoa na Haki za watoto na Wanawake.
Wilaya za Makete, Ludewa na Uwanging`ombe mara kwa mara zimekuwa zikikabiliwa na kesi za Masuala ya kugombania Ardhi (Mashamba), Ukatili wa Kijinsia na unyan yasaji wa watoto na masuala ya mirathi kutokana na Mila na desturi za maeneo hayo. Hivyo kufikiwa kwa Elimu ya Kisheria itasaidia kugeuza mtazamo wa wanajamii waliokuwa wakikosa haki zao kwa kutojua sheria.
Wadau wa masuala ya kisheria wakiwa katika kikao cha Tahmini ya mradi wa utoaji Elimu ya Msaada wa kisheria kwa wasaidizi wa kisheria wilayani Uwanging`ombe kilichofanyika katika ukumbi wa Parokia kijiji cha Igwachanya wilayani Uwanging`ombe Mkoani Njombe.
Mradi wa Utoaji wa Elimu ya Kisheria unatarajia kukamilika mwezi Disemba 2016 katika wilaya za Makete, Ludewa na Uwanging`ombe ambapo wasaidizi wa kisheria watakuwa wamepatiwa usajili kama Asasi ambazo zitajitegemea na kuendelea kutoa huduma za Msaada wa Kisheria katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment