Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Madaba Prosper
Luambano amewataka wakulima wa Halmashauri ya Madaba kujiunga kwenye vikundi
ili waweze kukopa nyenzo za kulimia ikiwemo Matrekta.
Kaimu Mkurugenzi ameyasema hayo baada ya kupokea
taarifa kwa NMB kuwa waliweza kukopeshwa shilingi Milioni 113 na kuweza kulima
kitaalamu Hekari zisizopungua Hekari 522 za Mahindi.
wakulima wa Halimashauli ya Madaba wakisikiliza watalamu wa kilimo njia za kuweza kuendelea kwa kutegemea kilimo
Akina mama Madaba wamekiri kuwa kilimo kinaweza kuwa komboa baada ya kuvuna gunia 30 kwa ekari moja
Pamoja na hayo wananchi wa madaba wameomba elimu ya kilimo ianze kufundishwa toka shule za awali ili mtoto aondoe dhana ya kusema masikini ndio wanao sitahili kulima
Nao Wakulima wamesema wameshindwa kupuliza dawa ya magugu
kutokana na upungufu wa Vitendea kazi kama
Mabomba ya kupulizia dawa, Wakulima wa madaba wamesema ili kilimo kiwe na tija
wange weza kukopeswa mikopo ya muda mrefu kutegemea na zao unalo lilima
WAKULIMA HALMASHAURI YA MADABA WAMETAKIWA KUJIUNGA
KATIKA VIKUNDI ILI WAWEZE KUNUFAIKA NA FURSA ZA MIKOPO YA PEMBEJEO NA KUWEZA KULIMA
KILIMO CHENYE TIJA.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Prosper Luambano amesema ikiwa wakulima
wataanza kulima kwa kutumia Trekta hali ya uchumi itaongezeka, amewaomba wakulima
wa Halmashauri ya Madaba kulima pia zao la Tangawizi ambalo kwa Ardhi ya Madaba
inakubali. Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba amewaomba wawekezaji wanaotaka
kuwekeza kwenye Kilimo waweze Madaba.
Wataalamu wa Kilimo wamewataka Wakulima wanapolima waangalie mbegu za kupanda ili wanapovuna wapate kujiwekea chakula na kupata kipato baada ya kuuza mazao yao watalamu hao wamewaomba wakulima kutumia dawa ya kuua magugu kwa kuwa ina punguza garama ya palizi
Mkoa wa ruvuma kwa msimu wa Mwaka 2015 - 2016 wanatarajia kuvuka lengo la mwaka
jana la kuvuna Tani million 1.8 na kuweza kufikia Tani Milioni 2
kutokana wakulima kuelimika baada ya kupata elimu kutoka kwa watalamu wa Mashirika ya RUDI na ACTN kupitia Makampuni
ya SEEDCO, SYNGENTA na YARA. Kwa mwavuli wa Green Luvolation
No comments:
Post a Comment