Afisa tarafa wa Tarafa ya Muhukuru
Salma Mapunda akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Songea katika zoezi la kuteketeza bangi iliyooteshwa shambani amesema shamba lenye ukubwa wa ekari 2 linaloteketezwa
lilibainika baada ya wananchi wenye kuchukia biashara ya Madawa ya kulevya kwa
kushirikiana na Serikali ya Kijiji kutoa taarifa za uwepo wa shamba hilo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma
limefanikiwa kuteketeza Shamba hilo la Bangi lenye ukubwa wa ekari 2 katika Kijiji
cha Manyamba Kata ya Muhukulu barabarani Songea Vijijini.
Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa imara katika mapambano dhidi ya Vita hii ya Madawa ya Kulevya ambayo ni tishio kwa Vijana.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Manyamba akishiriki katika zoezi la kuteketeza Bangi amesema yeye kama kiongozi wa Serikali ataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na Viongozi wengine katika Mapambano dhidi ya Zao la Bangi amesema tatizo lililopo wakulima wa bangi wanahamia kinyemela katika vijiji kwa kutafuta maeneo mazuri ya kulima wanapopata wanaamua kulima Bangi badala ya kulima mazao ya chakula
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Manyamba anasema, inakuwa vigumu kuyabaini mashamba hayo wanapoanza kilimo kwa kuwa hawaripoti katika Uongozi wa Vijiji husika wao huchukua maeneo kupitia kufuata wenzao na baadaye inabainika bangi ikiwa imeoteshwa na pengine imeshakuwa kupitia doria za msako wa mashamba yanayolimwa bangi hizo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Manyamba anasema vijana watambue kuendelea kulima Bangi hawatakuwa salama kwa kuwa Serikali ina mkono mrefu badala yake wanaweza kulima Maharege, Ufuta na mahindi mazao ambayo wakilima hawana shida ya kukimbizana na Serikali.
Mwanasheria wa Serikali akiwa katika Oparesheni hiyo ya Kuteketeza Bangi katika shamba lililopo Msitu wa Kijiji cha Manyamba Muhukuru Songea Vijijini amesema sheria ya sasa hivi iko wazi na endapo mtuhumiwa anabainika na vielelezo vikitimia adhabu yake haina mbadala hivyo ni vyema wananchi wakaacha kabisa kujishughulisha na kilimo cha bangi badala yake watafute kazi zingine.
Mwanasheria wa Serikali akishiriki zoezi la kufyeka Bangi iliyokuwa imeoteshwa katika Shamba hilo Kijiji cha Manyamba Tarafa ya Muhukuru.
Afisa tarafa
wa Tarafa ya Muhukuru amesema wananchi kutokana na kuzungukwa na Hifadhi za
Misitu minene za wanyama na milima mikali ndiyo sababu hutumia kulima bangi
wakijua hakuna mtu anayeweza kutambua uwepo wa mashamba hayo.
Kazi ya uteketezaji wa zao la Bangi ikiendelea ikiongozwa na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Muhukuru Salma Mapunda akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema kwa kushirikiana na Vijana wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Songea.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji amesema kampeni ya kuteketeza madawa
ya kulevya inaendelea Mwananchi yeyote mwenye Taarifa za kuwepo kwa mashamba ya Bangi au taarifa za uwepo wa Biashara ya Madawa ya Kulevya atoe taarifa Jeshi la
Polisi.
Mpaka sasa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limeshafanikiwa kuteketeza Mashamba ya Bangi Ekari 34
Namna Kilimo cha bangi kinavyohudumiwa kwa umakini hapo shamba lenye ukubwa wa Ekari mbili likiwa limeoteswa bangi pekee pasipo kuchanganya zao lolote. Wakulima wa kilimo hiki sasa wamebuni mbinu ya kulima maeneo ya mbali yenye milima na misitu mizito wakiamini si rahisi vyombo vya dola kuyafikia maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment