Ndege hizo zimeanza kutua Uwanja wa Songea kuanzia
tar 30 Mwezi wa nne mwaka huu, baada kukamilika kwa matengenezo makubwa yaliyofanywa katika
Uwanja wa Songea ili kukidhi sifa za kutua Ndege hizo na kuwa miongoni mwa Viwanja Bora katika Tanzania.
Shuhuli za Uzinduzi wa Usafiri wa Ndege za ATCL ziliongozwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Katika Uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge
amewaomba
wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kutumia Ndege yao katika kuongeza Mapato ambayo hapo
baadaye yanarudi kwao katika kujinufaisha kiuchumi na utalii.
Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiendelea na majukumu yao katika ghafla ya uzinduzi wa safari za Ndege za ATCL uwanja wa Songea Ulioko Ruhuwiko Manispaa ya Songea.
Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma Mhandisi Dr. Binilith Satano Mahenge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa kuweza
kufufua Shirika la ATCL , kuanza kwa usafiri wa ATCL kutarahisisha usafiri
kwa Nchi jirani za Malawi na Msumbiji na kuunganishwa kiuchumi na mikoa jirani.
Abiria wakishuka uwanja wa Ndege wa Songea katika Uzinduzi wa Safari za Ndege za ATCL Mkoani RuvumaNaibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani Akisoma Risala kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Safari za Anga za Mkoani Ruvuma kwa kutumia Usafiri wa Ndege za Shirika la Taifa la ATCL.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Mahenge amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kutumia ipasavyo fursa ya usafiri wa ATCL katika kutangaza Vivutio vilivyopo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa ili kuongeza mapato ya wilaya Mkoa na taifa kwa ujumla kupitia watalii wa mikoa jirani na nchi za nje.
Mwonekano wa Ndege za Shirika la Taifa la ATCL ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Ruhuwiko Manispaa ya Songea.
Ndege ya Taifa ya ATCL ikizindua safari zake kwa Mikoa ya Ruvuma na Mtwara pichani ni uwanja wa Ndege wa Songea.
Ndege ya Taifa ya ATCL ikiwa imetua katika uwanja wa Songea wananchi wakisubiri kwa hamu kuanza kwa safari zake ili kurahisisha safari za kwenda Muhimbili na safari za Kibiashara Jijini Dar Es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema(kulia) amesema kutokana na Mkoa wa Ruvuma kuwa mstari wa mbele katika kuzalisha mazao ya chakula hakuna shaka kwa wananchi wake kushindwa kumudu uwezo wa kupanda Ndege hizo kutokana na Uchumi walionao kupitia Kilimo.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani akisalimiana na Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma mara baada ya Kushuka katika Ndege tayari kwa shughuli ya uzinduzi wa Usafiri wa Ndege za ATCL.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr binilith Satano Mahenge mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Songea tayari kwa ghafula ya Uzinduzi wa safari za ATCL. Pembeni ni viongozi wa Bodi ya ATCL na Viongozi wa Bodi ya Utalii na wadau wa usafiri wa Anga.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Ruvuma wakihakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika Uzinduzi huo wa Safari za Ndege za Shirika la ATCL
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania amewataka wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuiunga Mkono Serikali kwa kutumia Usafiri wa Anga wa Shirika la
Ndege la ATCL ikiwa ni pamoja na kuongeza uchumi wao kwa kurahisisha Biashara
zao.
Naibu Waziri wa ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Edwin Ngonyani akisoma hotuba ya Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim
Majaliwa katika Uzinduzi wa Usafiri wa Ndege za ATCL za kutoka
Dar-es-Salaam hadi Songea Waziri Mkuu
amesema Usafiri wa Anga unasaidia sana kuinua Uchumi wa Mwananchi wa Mkoa wa
Ruvuma.Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani akisoma taarifa ya Waziri Mkuu amesema kufika kwa ndege Moka wa Ruvuma ni moja ya kufungua biashara kwa mikoa jirani pamoja na nchi jirani zinazo tuzunguka.
Naibu waziri wa Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano amesema mpaka kufikia mwaka 2018 uwezekano wa kuongeza safari kwa nchi za jirani za Kenya DRC, Malawi Rwanda, Burundi, Kenya na Msumbiji utawezekana
Naibu Waziri wa Ujenzi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakikata Keki ya ikiwa ni ishara ya kuzindua safari za Usafiri wa ndege za ATCL Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilithi Satano Mahenge amewaomba Watanzania na Wananchi
wa Mkoa wa Ruvuma kutumia Ndege za ATCL katika kuongeza vipato vyao kiuchumi katika kumunga mukono Rais wa Tanzania
nilazima kila mtanza nia atumie ATCL
Uzinduzi wa
usafiri wa Anga kwa kutumia ndege za ATCL umeshirikisha Wadau mbalimbali
wakiwemo Wafanya Biashara,
Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi wa Kawaida
Aidha waziriri Mkuu awewaasa wafanyakazi wa Shirika la Ndege la ATCL kutunza
Ndege hizo.Wahudumu wa Uwanja wa Ndege wa Songea wakiendelea na majukumu yao katika kuhakikisha mizigo ya Abiria wa ndege ya ATCL inahifadhiwa sehemu husika
Viongozi mbalimbali waliohudhuria tukio la uzinduzi wa usafiri wa Ndege za ATCL Mkoani Ruvuma, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Dr Osca Albano Mbyuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Mahenge akiongoza akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko na Katibu wa CCM Mkoa na Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma na Mkuu wa Wilaya ya Songea wakiwa katika uwanja wa ndege muda mfupi kabla ya kuwasili Ndege ya ATCL
Naibu waziri na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakikata Keki kuashiria uzinduzi wa usafiri huo uliosubiriwa kwa hamu na wananchi wa mkoa wa Ruvuma
Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge na wa mwisho kulia ni Mbunge wa Lushoto Mkoani Tanga mh Rashid Shangazi aliyeambatana na Mbunge wa Madaba Joseph Mhagama kushuhudia ghafla hiyo muhimu katika kukuza fursa za kiuchumi baina ya mkoa na mkoa, nchi na nchi.
Wadau wa Maendeleo na viongozi mbalimbali Mkoani Ruvuma
Mkurugenzi wa Halmashauri wa wilaya ya Nyasa Dr. Osca Albano Mbyuz amesema kuanzishwa kwa usafiri wa anga ni fursa nzuri kwa watalii kutembelea wilaya ya Nyasa na kuona fusa zilizopo katika uwekezaji wa utalii kwa kuwa sasa safari ya kutoka Dar Es salaam hadi kufika Nyasa haitachukua siku mbili watalii wataweza kusafiri kwa ndege muda wa saa moja hadi Songea na hapo watasafiri kwa basi mwendo wa masaa 4 watakuwa wamefika Mwambao wa Ziwa Nyasa ameomba watalii na wadau mbalimbali kuwekeza katika wilaya hiyo.
Mh. Joseph Kizizo Mhagama Mbunge wa Jimbo la Madaba akiwa katika Ghafula ya uzinduzi wa Safari za Ndege za ATCL kwenye uwanja wa Ndege wa Songea.
Wadau wa Usafiri wa Anga waliohudhuria ghafla ya Uzinduzi
Meneja wa uwanja wa ndege kanda ya Songea na Mtwara Esther Mahiga akibadilishana mawazo na mmoja wa abiria aliyekuwa akisubiri kuanza safari mara baada ya uzinduzi wa safari za Ndege uwanja wa Songea.
Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) Mhandisi Ladislaus matindi amesema miongoni mwa faida zinazopatikana katika kutumia usafiri wa Ndege za ATCL ni pamoja na punguzo la Nauli na kutokwisha thamani kwa tiketi ya Abiria pindi anapokata tiketi na kutokea dharula ya kumfanya ashindwe kusafiri siku aliyokatia tiketi au kuchelewa usafiri basi tiketi hiyo itaweza kutumika katika wakati mwingine.
Kaimu Afisa Rasilimali watu wa Mkoa wa Ruvuma akiwa na Afisa Biashara wa Mkoa wa Ruvuma Nehemia James wakitafakari fursa ya usafiri wa Anga katika kusaidia wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuzingatia wakati katika kujiletea maendeleo.
Mc wa Mkoa Meck Mguhi akisherehesha katika ghafla ya Uzinduzi wa Usafiri wa Ndege za ATCL Mkoani Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Mahenge akiwa ndani ya Ndege ya ATCL mara baada ya kuzinduliwa rasmi safari zake za Songea Mtwara Dar Es salaam.
Usafiri wa
Anga kwa kutumia Shirika la Ndege Tanzania (ATC) ulisitishwa kwa miaka 19
iliyopita, kwa sasa itakuwa ni Ukombozi kwa Mkoa wa Ruvuma kupata usafiri wa
ndege wa bei nafuu.
Wadau wa mkoa
wa Ruvuma wamesema wanaishukuru Serikali kwa kuweza kuanzisha Usafiri wa Anga
ambao utaweza kuraisisha watu wanaosafirisha Wagonjwa na safari za Biashara
Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama na Mbunge wa Lushoto Rashid Shangazi wakiongea na waandishi wa Habari juu ya fursa zitakazo patikana kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia kutumia Usafiri wa Ndege za ATCL mara baada ya uzinduzi wa Usafiri wa Ndege hiyo katika uwanja wa Ndege Songea.
Muhudumu wa Abiria ndani ya Ndege akifungua Shampeni ishara ya kufurahia kuzaliwa safari za ndege za ATCL katika uwanja wa Ndege wa Songea.
Viongozi waliohudhuria ghafla hiyo ya uzinduzi wakiinua glass za shampeni katika kusherehekea uzinduzi wa safari za Ndege.
Viongozi wakigonga chairs ishara ya upendo katika ghafla ya uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Viongozi wengine walioshiriki katika uzinduzi huo wakifurahia kurahisishwa kwa usafiri wenye kutumia muda mfupi kutoka Dar-Es-Salaam tofauti na usafiri wa Mabasi unaotumia zaidi ya masaa 12 hadi kufika Songea ukitokea Dar-es-Salaam.
Muhudumu wa Ndege za ATCL akiwa katika sura ya furaha baada ya kuona wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wakiifurahia fursa ya kuletewa usafiri wa Ndege za ATCL
Wadau wakishuhudia zoezi la kukata Keki maalum ya uzinduzi wa Safari za ndege Songea - Mtwara-Dar-Es-Salaam.
Zoezi la kukata Keki likiendelea
Viongozi wakifurahia kufunguka kwa usafiri wa anga wakiamini hii ni hatua ya kupanua mawasiliano kwa haraka na mikoa jirani na nchi jirani jambo ambalo litasaidia kuingiza fedha za kigeni kupitia watalii na fursa zingine za kibiashara.
Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma akifuatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kupitia kufufuliwa kwa usafiri wa Ndege za Shirika la Taifa la ATCL ikiwa ni shemu ya Ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli wakati wa kampeni zake.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Amina Himbo amesema kupatikana kwa huduma ya usafiri wa Anga kupitia Shirika la Ndege la taifa la ATCL ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi katika ahadi zake wakati wa uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment