Mradi wa Kilimo Hifadhi kwa vikundi vya wakulima Vijijini umewanufaisha zaidi ya watu 45,000 katika kipindi cha miaka mitatu 2014/ 2017 katika wilaya za Mikoa ya Ruvuma na njombe.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika la ACTN Deogratias Ngotio wakati wa sherehe za Siku ya Mkulima Shambani zilizofanyika katika Kijiji Litapwasi Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.
Mradi wa Kilimo Hifadhi ni utoaji wa Elimu ya urutubishaji wa Udongo kwa wakulima na wagani kazi ili kujenga uwezo kwa wakulima kuachana na kilimo cha mazoea kisicho na tija na kulima kilimo hifadhi ambacho mkulima hupata tija katika mavuno kwa kupata gunia 20 - 25 kwa hekari.
Mkulima Kiongozi Sesilia Twitbet Nindi kutoka Kata ya Litapwasi Songea Vijijini akielezea mafanikio ya Elimu waliyoitoa kwa wakulima wa Kata ya Litapwasi katika kufuata Kilimo Hifadhi chenye kurutubisha udongo. Amesema changamoto wanazozipata ni kukosa ushirikiano wa moja kwa moja kutoka kwa viongozi wa Kata na Vijiji kwa kuona kazi wanayoifanya ya kuelimisha wananchi katika kilimo ni kama wanafanya siasa ameomba jamii kuacha kukatisha tamaa wananchi wanapojengewa uwezo katika masuala ya Kilimo kwa kuchanganya na Siasa.
Mratibu wa Shirika la ACTN Deogratius Ngotio amesema katika kipindi cha misimu mitatu ya kilimo cha uteklelezaji wa Mradi wa kuelimisha vikundi vya Wakulima kupitia Mashamba Darasa ya wakulima wameweza kuwafikia watu zaidi ya elfu 45 kupitia mashamba
No comments:
Post a Comment