Vijana waendesha Boda
boda Manispaa ya Songea wameiomba Serikali kuendesha Mafunzo ya Udereva wa
Pikipiki na Magari Vijijini badala ya kuendesha Mafunzo hayo katika Vyuo vya
Veta.
Vijana wapatao 238 waliomba Ombi hilo wakati wa ufungaji wa
Mafunzo ya Madereva wa Bodaboda katika Vijiji vya Matimila na Mwenge Mshindo.
Vijana hao wamesema Ajali nyingi zilikuwa
zinatokea kwa Vijana kutojua sheria za Usalama Barabarani, wapo vijana
waliopoteza Maisha kwa kuwakimbia Askari wa Usalama Barabarani, wengine
kutokana na mwendo kasi na wengine
kutokujua kusoma Alama za Barabarani
Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ruvuma Abell Swai amewataka waliohitimu Mafunzo ya Udereva kuwa Makini kwa kufuata Sheria za Usalama Barabarani.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ruvuma Abell Swai amesema Mafunzo ya Udereva wa Pikipiki na Magari katika Mkoa wa Ruvuma umeweza kupunguza Ajali kwa asilimia 60% baada ya Madereva kutumia Alama za Barabarani na kuendesha kwa Mwendo wa Pole
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Songea Gideon Ole Lairambe amewaomba Vijana na
Wazee wanaotaka kuingia katika Fani ya Udereva waepukane na watu wanaowaahidi
kuwapa leseni, kwa sababu Leseni
inatolewa kwa Madaraja yote baada ya Mtu kupitia Chuo cha Veta,
Amesema wapo Madereva waliopoteza Ajira kwa kuwa na Leseni
Feki hivyo kila anayetaka kupata Leseni iliyo safi ajiunge ajiunge na Vyuo vya
Ufundi VETA ambavyo kwa sasa vinatoa Mafunzo hata Vijijini.
Vijana waliohitimu Mafunzo ya Udereva wakiwa katika Kata ya Mwenge Mwenge Mshindo wakisikiliza mafunzo kwa makini.
No comments:
Post a Comment