· Abubakar Karsan
Furaha ya kufa bila makuu ni kuzikwa bila sifa na utukufu uliopindukia ubinadamu.Furaha ya kuzikwa kwenye kaburi lisilokuwa na ufahari kiasi ambacho miaka ikipita utakumbukwa kwenye nyoyo ya watu na sio kwenye miundo mbinu ya kifahari,

kaburi ambalo dahari na dahari litaonekana na jina lako,Mungu nijaalie nisizikwe hivo,nizikwe kwa kufukiwa udongo na wala kaburi langu lisiandikwe chochote.
Mungu nijalie niache sifa kwenye mioyo ya watu,sifa zitakazodumu milele,watu ntakaowaacha hawatanitafuta kwenye makaburi bali katika mapindo ya historia ya matendo makuu ya binadamu
·
Abubakar Karsan
Asante Mungu kwa uhai ulionipa kwa miaka hii 51,nimeitumikia hivi:miaka 8 Mwanza Press Club,
·
Abubakar Karsan
Asante Mungu kwa uhai ulionipa kwa miaka hii 51,nimeitumikia hivi:miaka 8 Mwanza Press Club,
miaka 7 Media Council of Tanzania,miaka
12 Mwanza Non Governmental Organization,miaka
3 Non State Actors Support Programme,UTPC naitumikia kwa mwaka wa 7 sasa.Miaka hiyo yote inaingiliana.Kwa miaka 30 iliyobaki nimeweka malengo yafuatayo:
1.Kuijenga UTPC na klabu yake kuwa asasi bora kabisa Duniani
2.Kuchangia kukuza uwezo wa kitaaluma na kipato kwa waandishi wa habari Tanzania
3.Kuwawezesha watoto wangu na mke wangu kuishi maisha bora yenye uhakika
4.Kufa na kuzikwa bila madoido,isirafu au kutukuzwa.MUNGU wangu nijaalie nitimize hayo
No comments:
Post a Comment