AJIRA YA JESHI LA POLICE IENDANE NA MAADILI YA UKOO WA MWAJIRIWA.
Adamu Mzuza Nindi - Songea
Kwa namna ya pekee napenda kutoa pole kwa Familia ya Askari
wa Jeshi la Polisi P.C. Yohana aliye uwawa na Raia wenye hasira kari baada ya
asikari huyo kumpiga risasi Mkisio Ngonyani 27 aliye pakizwa na dereva wa
bodaboda na yeye kuuwawa na wananchi wenye hasira kali .wote wawili walipatwa na mkasa huo katika
Kijiji cha Kwinde Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa tarifa zilizo tolewa na kamanda wa police Mkoa
wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki zina sema Mkasa huo ulimpata asikari huyo baada ya
kumsimamisha dereva wa bodaboda ambaye alipakiza watu wawili kinyume cha
sheria, lakini dereva huyo hakuweza kusimama ndipo Asikari Police Pc Yohana
number 7771 alipo inua bunduki na kufyatua risasi iliyo mpata Makisio
Ngonyani kichwani na kufa papo hapo.
Wananchi
wamekuwa wakichukua Sheria mkononi kutokana na Busara zinazofanywa na Askari wa
Usalama Barabarani.
Ukiangalia
tukio lililotokea Ngwinde ni tukio ambalo linatakiwa Askari kujishauri kabla ya
kufanya Tukio la Mauaji.
Mtuhumiwa
amebeba Abiria wawili na umemsimamisha haja simama, jambo la Busara ni kunukuu
Namba halafu Mtuhumiwa atafutwe, lakini unapofyatua risasi, risasi hiyo inaweza
kumpiga raia ambaye hana hatia. Jee wale walio kuwepo wanakuwa na Mawazo gani ?
Ningeshauri
nikiwa Raia wa Tanzania kabla ya Askari hajapata Ajira Jopo la wanaomteua basi
walau wajue Tabia ya Mtu huyo kabla ya kuajiriwa, kujua Tabia ya Ukoo inaweza
kusaidia kupata Askari Bora.
Upande wa Wananchi Tunapoamua kuingia Barabarani kuendesha Vyombo vya
Moto ni lazima tujue hatuko juu ya Sheria ni lazima tufuate Sheria, kwenda
kinyume cha Sheria Tuone kuna tunalazimisha
vyombo vya Dola kutumia Sheria na Sheria
zingine ni hizi zinazosababisha vifo kwa Raia.
Wananchi wenzangu ni lazima tuwe tunasahihisha yale Mabaya yanayotokana
na Ubongo wetu kuutumia vibaya kuna methali isemayo you must think before doing the things. Mitihani haisahihishwi shuleni
tu hata katika ubongo wa binadamu tuna takiwa kuwa na kawaida hiyo
Watu wanachoangalia ni kifo cha mtu na siyo kufikiri jinsi ya kuepuka
Vifo hivyo.
Wananchi tujitahidi kufuata Sheria ili kuweza kulinda Roho zetu.
No comments:
Post a Comment