Wananchi wa Vijiji vinavyopakana na Mbuga ya Seluu
Mkoani Ruvuma wamepongezwa kwa kuweza
kupambana na Ujangiri na kuweza kuwakamata Wawindaji haramu sugu ambao walikuwa
wakitafutwa zaidi ya miaka 10 kwa tuhuma za Uwindaji haramu.
Mratibu
wa Shirika la PAMS FOUNDATION ambalo
lina fadhiliwa na Shirika lisilo la kiserikali la LIZ CLAIBORNE
ART ORTENBERG FOUNDATION kutoka Marekani amesema watuhumiwa
Yazidu Hassan Chilombo na mwenzake
Said Milinga hivi karibuni walikuwa
katika Mbuga za Seluu walikamatwa na Askari wa wanyamapori kwa tuhuma za Uwindaji haramu wa Tembo.
Shirika la PAMS FOUNDATION pamoja na kupambana
na Ujangiri likishirikiana na Wananchi, pia linawasaidia wananchi kulinda mazao
yao yasiliwe na wanyama waharibifu, , zaidi ya Hekta 1000 za mazao mbali mbali yame salimika baada Shirika la
PAMS FOUNDATION kubuni njia rahisi yakupambana na wanyama wa haribifu kwa
kutumia pilipili ,oil chafu pampja na kufuga nyuki ambao ni adui mkubwa wa Tembo
Mratibu Maxmilan
Jenes wa shirika la PAMS FOUNDATION [Shirika linalo jihusisha na kupambana
na ujangili liliopo mkoani Ruvuma]
ambalo lina fadhiliwa na LIZ CLAIBORNE ART
ORTENBERG FOUNDATION amesema watuhumiwa Yazidu Hassan Chilombo na
Said Millinga hivi karibuni walikuwa katika Mbuga za Seluu walikamatwa na
Askari wa wanyama pori katika doria zao baada ya kukuta wakiwa wamemuua Tembo ambaye walimng`oa meno yake na
kuweza kumkata mkia.
No comments:
Post a Comment