Na Adam Nindi,
Songea
UJIO WA RAIS WA CHINA NCHINI TANZANIA UNATUKUMBUSHA MENGI:
Wananchi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika Ujio wa Rais wa China
unatukumbusha mambo mengi, mambo hayo ni pamoja na Ujasiri, Huruma,
Kuthubutu pamoja na kujiamini kuwa kila kitu endapo utakipanga vizuri kinawezekana.
Wakati
wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema Hakuna Mnyororo ambao
unaweza kumkomboa Mtanganyika ni Ujamaa pekee.
Sera
ya Ujamaa ilitokana na Rais wa China
wa wakati huo Mao Satuni ambaye aliweka mikakati kwa Wananchi wa China kufanya
kazi kwa pamoja jambo ambalo limewapa Ufanisi.
Tanganyika wakati huo kufuatia Siasa
ya Ujamaa na Kujitegemea iliweza kupiga hatua, Ujamaa ulianza JKT hadi kwa
Wananchi ambao walikuwa na mashamba ya pamoja au kundi Fulani kujikusanya na
kulima Shamba la mtu mmoja.
Kinachotakiwa
kwa sasa, tunatakiwa kuangalia Jee hawa wenzetu wa China toka tuachane kipi kimewapa
Ufaulu. Jee Watanzania tufanyeje tusiishie kupiga Ngoma na Ngonjera nyingi huku
tukiwa hakuna tunachojifunza.
Kipindi
cha Mwalimu Nyerere tuliiga Mvao wa watu wa China ya chonlai, pia Ujamaa halisi.
Hivyo
kufika kwa Rais wa China
kuwe ni ufunguo wa kuweza kupata Maendeleo.
|
No comments:
Post a Comment