Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Akipokea msaada wa Vifaa kutoka kwa Afisa Mahusiano wa Mantra Khadija Pallangyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Kampuni iliyotolewa na MANTRA chini ya Kampuni ya ROSATOM ya Urusi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge akisalimiana na Mwenyekiti wa uhamasishaji kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa Ruvuma ndugu Mkude katika viwanja vya jengo Dawati la Police wanaewake Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa kituo cha police wilaya ya Songea akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mara alipo tembelea Dawati la Jinsia la Police Mkoa wa Ruvuma
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge ametoa angalizo kwa jeshi la Police kuhakikisha Dawati la Police Wanawake lina kuwa na wataalamu wanao wiana na umahiri wakuweza kutatua matatizo yanayo ikabili jamii kwa kuweka watu wenye umakini wa kufanya kazi kwa kulinda heshima na utu wa mtanzania na sio kuweka mtu yeyote ili mradi Askari pasipo kujali uwezo wake
Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji ameahidi mbele ya mkuu wa mkoa kutoa wataalamu wenye uwezo kushugulikia dawati kwa umakini na usiri kutegemea cheocha mtu aliye kwenye dawati huku akizingatia uwezo alio kuwa nao katika kusaidia jamii.
Mwenyekiti wa kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya jamii ya watanzania Renatus Martias Mkude alinukuu suala la maendeleo yaliyo tolewa na Rais Benjamini Wiliam Mkapa wa awamu ya tatu kuwa jambo jema linalo anzishwa na mtu mmoja ni budi liungwe mkono na watu wengine ili liweze kuletaufanisi na maendeleo kama hili linalofanywa na Dawati la Police katika kupinga ukatili wa kijinsia miongoni mwa jamii.
Mwenyekiti wa kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia bwana Renatus Martias Mkude akiainisha mafanikio yaliyopatikana katika kuhdumia watu walio athirika na vitendo vya ukali wa kijinsia, pamoja na mama aliyekuwa anaishi Peramiho ambaye alijichongea jeneza lililovunjwa na kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia, lakini hatimaye mama huyo wiki mbili zilizopita alifariki ambapo na kamati iliweza kuchonga sanduku lingine na kumzika mama kwa ushirikiano na wananchi wa Pearamiho
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema utafika wakati wa kuchimba madini yaliyopo Aridhini pale tutakapowapata watanzania ambao wanaweza kusimamia na kuelekeza madini hayo ya saidie wananchi wote, Ndivyo alivyofanya dada Khadija Pallangyo kwa kusimamia kampuni ya Mantra inayomilikiwa na Kampuni ya ROSATOM ya Urusi inayochimba madini ya uran na faida inayopatikana ikilenga kusaidia jamiii inayozunguka Maeneo ya igodi. MANTRA imekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 12 chini ya Afisa Uhusiano Mzalendo Khadija Pallangyo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Bilinith Satano Mahenge akisikiliza taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo iliyoainisha hali ya vitendo vya ukatili mkoani Ruvuma
Hivyo ni vifaa vilivyotolewa na Kampuni ya MANTRA yenye makao yake makuu wilaya ya Namtumbo katka mgodi wa Urenium One Mkuju
sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa
Vifaa kama vinavyoonekana hizo ni Sacana na Printa
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika makabidhiano ya vifaa vilivyotolewa kwaDawati la jinsia la Police wanawake ili kurahisisha utendaji wa kazi za dawati. Kutoka kushoto ni Mussa Homera na kulia kwake ni Mratibu mhamasidhaji wa ujenzi wa jengo la dawati Bw. Juma Nyumayo
Mdau mkubwa wa Dawati la jinsia Frenk Mchina akiwa wadau wengine akiwemo Mr Zuberi ambao wameshiriki kwa karibu katika kuchangia masuala mbalimbali ya dawati la jinsia la polisi hapo wakifuatilia utoaji wa vifaa vitakavyosaidia utendaji kwa jamii ya wana Ruvuma
Mhamasishaji maarufu mkoani Ruvuma Meki Mguhi akiendesha mapokezi ya vifaa kutoka Kampuni ya Uranium one
Kamati ya ulinzi na usalama wakishuhudia vifaa vikipokelewa baada ya kutolewa na MANTRA
wadau mbalimbali wa Mkoa wa Ruvuma wanaounga mkono Dawati na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia Mkoani Ruvuma
Kutoka kushoto ni kamanda wa Police Mkoani Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji na katikati Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge
Picha ya Pamoja kati ya Dawati la Police Wanawake na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Binilith Satano Mahenge
OCD na Mwenyekiti wa Dawati la kupinga ukatili wa kijinsia Anna Tembo wakipongezana kwa kuendesha Dawati la Police Wanawake
Mwenyekiti wa kamati ya kupinga ukatili Mkoa wa Ruvuma Mkude akisalimiana na Mwenyekiti wa Uhamasishaji wa Jengo la Police Wanawake Adamu Mzuza Nindi ambaye pia ni mkurugenzi wa Blog ya Songea Habari
Khadija Pallangyo akiwa katika Viwanja vya Police muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa kwa Dawati la Jinsia la Police Wanawake Mkoani Ruvuma.
Sehemu ya Caunter ya Dawati la Police wanawake ambayolimejengwa na kampuni ya uchimbaji wa Madini ya Uran One machimbo yaliyoko Mto Mkuju wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma
No comments:
Post a Comment