Waachi hao walifurahi kumuona Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhadisi Dkt Biilith Mahege akiwatembelea katka maeneo yao ya uzalishaji mali na kuwasisitiza kufanya shughuli za Maendeleo wakati alipokuwa ziara wilayai Nyasa hivi karibui.
Hapo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Mahenge akikagua shughuli za Ununuzi wa mahindi katika kituo cha kununulia Mahindi cha Tingi wilayani Nyasa, wananchi wameiomba Serikali iongeze kiwango cha ununuzi kutoka Gunia 500 hadi kufikia gunia 1000 kwa vijijini kwa kuwa uzalishaji ni mkubwa..
Akiwa Ziarani wilayani Nyasa Dr Mahenge alikagua shughuli mbalimbali za mendendeleo na namna wananchi wanavyohudumiwa na viongozi wanaosimamia utekelezaji wa maagizo ya serikali katika kuwatumikia.
Wananchi wa Wilaya ya Nyasa wakitumbuiza ngoma ya Kihoda wakati walipotembelewa na mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuona changamoto zinazowakabili na hali ya chakula katika Msimu huu wa kilimo wa 2015/2016.
Dr Mahenge akisalimiana na wananchi na viongozi wa chama na Serikali waliojitokeza kumsikiliza alipotembelea wilayani Nyasa.
wananchi wakimkaribisha Mkuu wa mkoa kwa Ngoma na furaha
Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Mahenge ukiingia katika Eneo la Machimbo ya Dar Pori wilayani Nyasa
Wananchi wa Dar Pori wakifurahia kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvua
Mkutano wa Hadhara baina ya viongozi wa wilaya ya Nyasa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na wananchi wa Dar Pori.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge
ametoa agizo kwa wakazi wa dar Pori kuheshimu sheria za mipakani na
kutokuingiza Siasa pakani.
Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Madini Nchini Msumbiji ameuomba
Uongozi wa Serikali mkoa wa Ruvuma kuwaomba wachimbaji wanaotoka Tanzania
kuacha kuingiza mambo ya Siasa katika Mipaka ya Tanzania na Msumbiji.
Mwenyekiti wa Wachimbaji kutoka Nchi Jirani ya Msumbiji katika mpaka wa Dar – Pori na Turo Msumbiji
ameyasema hayo wakati alipokaribishwa katika kumpokea Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge aliyetembelea katika Makazi ya Wachimbaji
wa Dar pori Wilayani Nyasa.
Amemwomba Mkuu wa Mkoa kuendeleza amani hiyo kwa kukemea
watu wanaogeuza Mipaka kuwa sehemu ya
Siasa. Mwenyekiti huyo alitoa Mchango kuchangia Zahanati ya Dar Pori kwa kutoa
Dhahabu gramu 5 yenye thamani ya shilingi 375,000.
Mwenyekiti
wa Wachimbaji Mpakani katika Kata ya Turu Nchini Msumbiji ameushukuru uongozi
wa Serikali ya Tanzania kwa kudumisha Amani na Utulivu katika Mipaka ya
Tanzania na Msumbiji. Viongozi waliohudhuria Mkutano uliohusisha pande mbili za Tanzania na Msumbiji wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Viongozi wa Msumbiji wakiwa katika Mkutano wa hadhara na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na wananchi wa Tanzania waishio Mpakani mwa Msumbiji alipotembelea kujionea hali ya mahusiano katika kudumisha amani.
Mkuu wa Wilaya ya
Nyasa Isabela Chilumba amesema zoezi la ununuzi wa Mahindi katika Wilaya ya
Nyasa linaenda vizuri
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa wachimbaji madini kutoka Msumbiji jinsi ya kukomesha biashara ya ngono kwa watoto wadogo katika maeneo ya Machimbo.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Inginia Dr Binilith Mahenge aiwa na mkaazi wa Dar Pori Joseph Msigwa akihoji kuhusu mapato yanayo pitishwa mpakani
Wananchi wa Dar Pori wakisikiliza Hotuba ya Mkuu wa Mkoa mhandisi Dr Mahenge wameomba kusaidiwa vifaa vya viwandani katika Ujenzi wa Zahanati wanayoijenga kwa nguvu zao.
Wazazi wakiwa
katika kutano wa hadhara uliofanyika katika Mpaka wa Msumbii na Tanzania katika
kata ya Unyere Tarafa ya Mpepo uliohudhuriwa na Viongozi wa Msumbiji na
Tanzania ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Satano mahenge
wameomba Serikali kuthibiti Mipaka na kuwakemea wafanya Biashara kuacha
kuwatumikisha watoto walio chini ya miaka 18
Mmoja wa Wazazi waliotoa maoni yao wamesema wao wakiwa kama
wazazi wanaona huruma kuona watoto walio chini ya miaka 18 wakifanya kazi za
ngono ili waweze kujikimu na Maisha.
Mganga Mkuu wa wilaya ya Nyasa Dr Papalika akitoa ufafanuzi kwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma nama walivyowafikia wananchi waaoishi mpakai mwa msumbiji na Tanzania katika suala la huduma za NHIF
Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kununua Tani 12 za Mahindi kutoka Wilaya ya Mbinga Vijijini, Jambo lililopongezwa kwa Serikali kuweka Vituo vya kununu Mahindi badala ya kuweka Mjini jambo ambalo lilikuwa ni adha kwa Wananchi
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akipokea zawadi ya gramu 5 za dhahabu yenye thamani ya shilingi 375,000 ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi wa Zahanati inayojengwa na wananchi wa Dar Pori wilayani Nyasa.
Dhahabu inayopatikana katika Machimbo ya Dar Pori na Turu Nchini Msumbiji kama inavyoonekana.
Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Madini Nchini Msumbiji mara baada ya kukabidhi mchango wa gramu 5 za dhahabu katika ujenzi wa zahanati ya Tanzania amesea hii ni kiashiria kuwa mahusiano baina ya Nchi za Tanzania na Msumbiji ni mazuri.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge ameuomba uongozi wa Serekari ya Msumbiji kushirikiana na Serekari ya Msumbiji kukomesha biashara ya Ngono inayo fanywa na wafanyabisara wa Machimbo mpakani mwa Msumbiji na Tanzania wakwana kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandithi Dr Binilith Satano Mahenge na aliye kushoto ni Mwenyekiti wa Machimbo Nchini Msumbiji Alezanda Alexander
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dktr Mahenge akiwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Msumbiji.
Viongozi wa Msumbiji wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji
Msumbiji wamesema watafanya kila jinsi kuhakikisha watoto wanaoihitajika kuwa
shuleni wanarudishwa Tanzania ili waweze kushiriki Masomo.
Katika Ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amepata fursa ya kujionea Mpaka wa Msumbiji na Tanzania na kuomba ushirikiano ulioanzishwa na Waasisi Samora Mahehe wa Nchini Msumbiji na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uimarishwe katika kulinda mipaka yake na kudumisha mahusiano mema.
Mkuu wa Mkoa Dr Mahenge akikagua Mawe ya mpaka wa Tanzania na Msumbiji.
MKuu wa koa wa Ruvua Dkt Binilith Satano Mahenge amesema
FRELIMO na CCM ni watu waliodumisha Amani kutokana na vyama vyao kuwa na Sera
mzuri. Umoja uliojengwa kati ya Saora Mashehe na Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ni lazima ulindwe.
Mpaka wa Tanzania na Msumbiji unahitaji kuimarishwa kwa faida ya vizazi vijavyo wa maendeleo ya Nchi mbili zinazopakana. Huo ni upande wa Tanzania kama inavyoonekana.
Viongozi wa Msumbiji wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji
Msumbiji wamesema watafanya kila jinsi kuhakikisha watoto wanaoihitajika kuwa
shuleni wanarudishwa Tanzania ili waweze kushiriki Masomo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Mahenge mara baada ya kukagua uimara wa mipaka katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji hapo akiwaaga wenyeji wake Askari wa Msumbiji wanaolinda usalama wa mipaka hiyo akiomgozwa na mwenyekiti wa wachimbaji.
Mkuu wa Mkoa akiagana na Askari wa Masumbiji wanaolinda Mpaka wa Tamzania na Msumbiji mara aada ya kukagua maeneo ya mipaka hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji alipotembelea mpaka wa Tanzania na Msumbiji kupitia wilaya ya nyasa. Kama anavyoonekana kwa ukakamavu akiwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji kutoka Msumbiji.
Aidha katika Ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma handisi Dkt Binilith Satano Mahenge amepiga Marufuku kwa watu wanaofanya biashara ya kusafirisha watoto ili wafanye biashara katika Mabaa na kufanyishwa Biashara ya Ngono.
Dr Mahenge amewataka Viongozi wa Vijiji, Watendaji pamoja na wananchi wa kawaida kuingia katika Vita ya kupambana na Biashara haramu ya kusafirisha watoto.
Wananchi wanaoishi
mpakani mwa Msumbiji na Tanzania wameiomba Serikali kukomesha biashara ya Ngono inayotumika kwa watoto walio chini ya miaka
17 na kusababisha watoto hao kukosa masomo.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma akionyeshwa maeneo wanayo chimba madini ya Dhahabu katika eneo la Msubiji
Afisa uhamiaji kutoka Tanzania akisalimiana na Askari wa Ulinzi wa Mpaka wa Msumbiji
Mwandishi wa Habari wa Star TV na Redio Free Afrika Mkoani Ruvuma Tanzania Adam Mzuza Nindi kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Msumbiji na Askari wa Tanzania katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji
Mkuu wa Mkoa katika kudumisha Mahusiano ya undugu kati ya
Wananchi wanaoishi Mpakani kati ya Msubiji na Tanzania aliweza kutembelea
mipaka ya Tanzania na Msumbiji na kuweza kutambulishwa kwa viongozi walinda
Mipaka ya Msumbiji.
No comments:
Post a Comment