Jumla ya watu 35,000
hufa Nchini Tanzania kutokana na Maambukizi ya VVU na UKIMWI na watoto 600,000
huachwa katika hali ya uyatima kila mwaka.
Akisoma Taarifa ya Takwimu za maambukizi ya UKIMWI kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr. Binilith Satano Mahenge amesema Takwimu ni kubwa hivyo ili kuweza kupunguza ongezeko hilo inabidi kutumia njia shirikishi itakayo kuwa na idadi sahihi ya maambukizi
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Mihayo Bupumba amesema njia
ya kwanza ni kuhakikisha wale wote walioathirika wanajulikana kwa asilimia 90%,
njia ya pili ni kutambua kama hao walioathirika wanapata dawa za ARV kwa
asilimia 90% njia nyingine ni kufahamu
na kudhibiti maambukizi mapya kwa asilimia 90% kwa kufanya sense ya kitalamu
bila kumlazimisha mtu
Katika utafiti huo Mkoa wa Ruvuma utahusisha katika wilaya zote kinachotakiwa ni wale wanaotakiwa kuwakilisha kushiriki kikamilifu.
Wadau wa Mapambano dhidi ya ukimwi kutoka halmashauri za Mkoa wa Ruvuma, Taasisi za Dini na Asasi zinazoshughulika na masuala ya UKIMWI wakiwa katika mkutano wa kupokea taarifa ya Utafiti wa Viashiria vya Ukimwi unaotarajia Kufanyika Tanzania nzima kwa kaya wakilishi.
Wadau wamesisitizwa kutoa ushirikiano katika zoezi hilo muhimu ili kufahamu Takwimu sahihi za hali ya maambukizi zitakazosaidia Serikali kujua namna ya kupanga Bajeti katika kuhudumia waathirika wa VVU
Wataalamu wa Afya kutoka Kitengo cha Utafiti wa Viashiria vya VVU na UKIMWI
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akitoa taarifa ya namna walivyoandaa maeneo yatakayohusika na utafiti huo kwa kushirikiana na waratibu na watakwimu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino Mihayo M. Bupamba akielezea teknolojia itakayotumika katika utafiti kwa kutumia electronic ambayo itatoa usahihi wa data.
No comments:
Post a Comment