Wakala wa Misitu Kanda ya Kusini wameweza kutoa Madawati 580
katika Shule za Msingi za Mkoa wa Ruvuma, Madawati hayo yakiwa na thamani ya
shilingi Milioni 43.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiwa na wanafunzi wa shule ya majiamaji akiwa uliza maswali
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema ili kufikia uchumi wa kati,
ni lazima kuimarisha miundo mbinu ya Elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha Eneo la
Kusomea kuwa na Walimu wenye wito, wazazi na Serikali kushirikiana kulinda
Miradi ya Elimu
Wanafunzi waliopewa Madawati
wameweza kushuuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka
mikakati ya kuweza kuwafanya wanafunzi wasikae chini waweze kusoma vizuri.
Afisa Elimu Manispaa ya Songea amewaomba wazazi na Wanafunzi
kulinda Madawati yaliyotokana na wadau ili Madawati hayo yaweze kudumu kwa
Vizazi vingi.
Mkoa wa Ruvuma kwa kiasi kikubwa wameweza kufikia lengo la
asilimia 99 ya watoto kukaa kwenye Madawati. Vita iliyopo kwa sasa ni
kuhakikisha watoto wanatumia vyoo bora vyenye hali ya kisasa pamoja na kuwa na
Benki ya Tofali ili kukiwa na kazi yoyote ya Ujenzi tofari hizo ziweze
kutumika.
Viongozi waliohudhuria zoezi la kukabidhi adawati 580 kutoka kwa wakala wa Misitu kanda ya kusini katika Ukumbi wa Maliasili Mkoani R
mshauri wa kisheria Fatuma Misango akieleza changamoto zinazo mpata mtoto wa kike
mtalamu wa mbegu za nafaka kutoka katavi Joanthan akitoa elimu ya jinsi ya kutumia mbegu za kisasa
Mtalamu wa mbegu kutoka katavi akitoa elimu mbegu zinazo faa koa wa ruvuma ambazo zime fanyiwa utafiti wa kutosha |
Kaimu Meneja wa Wakala wa Misitu Kanda ya Kusini Embrantino
Mgiye amesema pamoja na kutekeleza Amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuwataka wanafunzi wote wa Shule za Msingi na Sekondari kuwa asiwepo
mwanafunzi wa kukaa chini lakini Wakala wa Misitu wameona ni vyema Wananchi
wafaidi Rasilimali zao kwa kutoa Madawati kwa Wanafunzi ili tupate wataalamu
wazuri kwa kukaa watasoma kwa utulivu.
Kaimu Meneja wa Wakala wa misitu Kanda ya Kusini amesema
utoaji wa madawati kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari ni somo tosha
la kuwawezesha wanafunzi kujua kumbe
misitu inasaidia kila mtu hivyo wanafunzi
wataweza kukua na kujua faida za
misitu.
mkurugenzi wa manspaa ya Songea akiwa na katiu tawala wilaya ya Songea Pendo wakati wamakabidhiano wa madawati kutoka kwa wakala wa hifadhi ya misitu kanda ya kusini
No comments:
Post a Comment