Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Tanzania
Thobias Andengenye amewataka amewataka Askari wa Zimamoto kuwa waadilifu na
kufanya kazi kwa uaminifu ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya Tano.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa Habari Mkoani Ruvuma, amesema
Ziara yake inalenga kutaka kujionea changamoto zinazolikabili Jeshi la
Zimamoto.
Akizungumzia kuhusu Vifaa vya kuzimia moto na jinsi ya kutoa
Elimu kwa wananchi ili wasiweze kupatwa na Majanga ya moto amesema, ni vizuri
unapopata kiwanja kabla ya kujenga ukawasiliana na Viongozi wa Zimamoto na
uokoaji ili wakupe elimu jinsi ya kuepukana na Majanga yanayotokana na Moto.
Askari wa Zimamoto Briged ya kusini 401 KV wakitoa heshima kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na ukoaji akiwa Ziarani Mkoani Ruvuma.
Kamishna Jenerali wa
Zimamoto Thobias Andengenye akielezea kuhusu Vifaa vya kuzimia moto katika
maghari, ametoa ufafanuzi kuwa fedha zinazolipwa TRA ni kwa ajili ya ukaguzi na
sio za kununulia mitungi ya gesi. Jambo linalowachanganya wengi.
Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Ziamamoto na Uokoaji amesema kwa hivi sasa changamoto inayolikabili
Jeshi la Ziamamoto ni kukua kwa miji ambako ujenzi hauzingatii kujikinga na majanga.
Amesema kiutaratibu kinachotakiwa kila baada ya kilomita 15 kuwe na kikosi cha zimamoto.
Askari wa Jeshi la Ziamamoto na Ukoaji wa kikosi cha Briged ya kusini 401 KV wakiwa katika Ofisi za Kikosi hicho Manzese Manispaa ya Songea.
Vitendea kazi vya Jeshi la Zimamoto uokoaji vinavyotumika pindi majanga ya moto yanapotokea.
Magari ya Zimamoto yakiwa katika eneo la Kikosi cha Jeshi la Ziamamoto na uokoaji manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Askari wa Jeshi la Zimamoto wametakiwa kushirikiana na Vyombo vya habari katika kutoa Elimu ya kujikinga na Majanga ya moto badala ya kusubiri majanga yatokee kwa kuwa wao ndio wana wajibu wa kuzuia majanga kwa kuelimisha jamii kujikinga na majanga ya moto.
No comments:
Post a Comment