Jumla ya Mizinga 2000
imetundikwa katika Mikoa ya Kanda ya Kusini ikiwemo Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Kaimu Meneja wa
Wakala wa huduma za Misitu kanda ya
kusini Bowazi Sanga amesema kutokana na
wananchi kujua faida ya kufuga Nyuki na wamejitokeza kwa wingi siku ya
kutundika mizinga na kufanikiwa kutundika
mizinga 2000.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Kusini Bowazi Sanga amewaomba Wananchi
kuitunza Misitu kwa kutochoma moto
Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu amesema kuchoma misitu moto kunasababisha
kuwakimbiza Nyuki pia kuharibu Mazingira.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Robert Magen kushoto akiwa na Afisa Ufugaji Nyuki wakitundika Mzinga katika Uzinduzi wa utundikaji wa mizinga wilayani Mbinga.
Kulia ni Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Mkoa wa ruvuma Manyisye Mpokigwa akionyesha namna ya kutundika mizinga kwa ufasaha mbele ya wananchi wanaohitaji kunufaika na ufugaji wa kisasa.
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Mkoa wa Ruvuma Manyisye Mpokigwa akionyesha Mfano wa Mizinga ya kisasa kwa wale wanaotaka kuingia katika ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kujipatia kipato.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Mahenge
amewaasa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujikita katika ufugaji wa Nyuki kwa kuwa
hauna gharama, gharama yake ni kuchonga mizinga tu.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Mahenge amewaomba wafugaji wa Nyuki kuunda vyama vya ushirika ili wawezed kupata Soko zuri la Asali.
ufugaji wa nyuki endapo utazingatiwa unatoa tija kwa mfugaji kwa kuwa mazao yanayotokana na nyuki yananunuliwa kwa bei nzuri, ni jukumu kila mwananchi kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiongezea kipato.
Aidha, Dr Mahenge amewaomba viongozi wa vijiji kuweka ulinzi kwenye vyanzo vya Maji kusichomwe moto, atakayebainika kuchoma moto mtu wa kwanza kuchukuliwa hatua atakuwa Mwenyekiti wa Kijiji.
Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Mhandisi Dr Mahenge akibadilishana mawazo na Maafisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Kusini.
Wadau wa Ufugaji wa Nyuki wilaya ya Mbinga wakifurahi kusletewa uzinduzi wa Utundikaji wa Mizinga katika Kijiji cha Mahande wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akikagua mizinga kuona teknolojia iliyotumika katika kuboresha mizinga ya kisasa.
Mhandisi Dktr Binilith Mahenge katika Kijiji cha mahande wilayani Mbinga akipokea taarifa ya ufugaji Nyuki katika maadhimisho ya siku ya Utundikaji Mizinga ya Nyuki iliyofanyika kikanda wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma.
No comments:
Post a Comment