Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akizindua wiki ya Unywaji wa Maziwa kwa kuonyesha Mfano wa kunywa Maziwa ikiwa ni njia moja wapo ya kuhamasisha Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujenga Mazoea ya kutumia kinywaji cha Maziwa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akikagua Mabanda ya Maonyesho ya Bidhaa mbalimbali za Maziwa katika sherehe za Uzinduzi wa Wiki ya Maziwa ambazo Kitaifa zimefanyika Mkoani Ruvuma. Kulia ni Dr Ruth Rioba Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu akipokea Maelekezo ya Matumizi ya Bidhaa zinazotengenezwa kwa Maziwa alipokuwa akikagua Bidhaa zilizoletwa na wazalishaji na wasindikaji wa Maziwa
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu (aliyeshika maiki) akitoa nasaha kuhamasisha Unywaji wa Maziwa wa mazoea kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma badala ya kusubiri mpaka kuugua ili kuboresha Afya zao. Hayo ameyasema katika Viwanja vya Manispaa ya Songea wakati wa Maadhimisha ya Uzinduzi wa Wiki ya Maziwa Kitaifa Mkoani Ruvuma, amesema Mkoa wa Ruvuma una Ng`ombe 371,000 kati yao wa Maziwa ni 12,032 tu ambao huzalisha lita 96,256 kwa mwaka.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu kushoto akisisitiza utumiaji wa Bidhaa zinazotokana na Maziwa. Amesema wastani wa unywaji wa Maziwa Kitaifa kwa mtu kwa mwaka ni lita 45 wakati viwango vilivyopendekezwa kimataifa (WHO) na (FAO) ni angalau lita 200 kwa mtu kwa mwaka, wastani wa unywaji wa maziwa katika Mkoa wa Ruvuma ni lita 11.6 tu kwa mtu kwa mwaka.
Dr Ruth Rioba Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Taifa akifafanua lengo la kuyaleta Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa Mkoa wa Ruvuma katika Uzinduzi wa Wiki ya Maziwa uliofanyika Viwanja vya Manispaa ya Songea.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, Asasi, Taasisi na Mashirika waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya Maziwa Mkoa wa Ruvuma wakitathmini kwa makini kiwango cha chini cha unywaji wa Maziwa katika Mkoa wa Ruvuma.
Ng`ombe wa Maziwa akiwa katika Banda Maalumu katika viwanja vya Manispaa ya Songea yanapoadhimishwa Maadhimisho ya wiki ya Maziwa ambayo kilele chake kitakuwa 1/06/2013
No comments:
Post a Comment