KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo
UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Sunday, May 5, 2013
WABUNGE WETU MKOANI RUVUMA UMOJA WENU UPO WAPI KIMAENDELEO
Mheshimiwa Jenista Mhagama 1.Kutoa Pongezi kwako kwa kuweza kutuwakilisha katika Bunge ukiwa Mwenyekiti. Kuteuliwa katika kamati mbalimbali zenye kupigania maendeleo. 3.kuweza kujenga makao makuu ya Halimashauri ya Wilaya Songea Vijijini .lakini la mwisho jaribu kurudisha umoja wenu wawa bunge ili wananchi wapate maendeleo
Mheshimiwa Kazi unayo, umeapa kwa katiba kuwa utatekeleza ilani ya chama Wananchi wana ngoja Barabara ya Namtumbo - Tunduru kuwa na Lami, Pamoja na kazi ulizo fanya za kuweza kuweka bei nzuri ya Korosho, Wananchi wana ngoja barabara ya Lami.
Mheshmiwa Vita Kawawa Umenyosha juu ilani ya Chama cha mapinduzi kuleta Maendeleo kwa Wananchi wa Namtumbo, 1. Swala la Barabara umesimamia vilivyo. 2.Juhudi za Kuweka umeme wilaya ya Namtumbo umefanikiwa. Vitu unavyo daiwa Nikuwa na Hospitali ya Wilaya Namtumbo. Pia Uchumi wa Wananchi wa Namtumbo wana Tegemea Tumbaku Simamia Bei ya Tumbaku iwe Nzuri. Mwisho simamia kutoa Mfumo Dume ulio kithiri wilaya ya Namtumbo
MheshimiwaMtutula Mtutula na Jua una mambo mengi ya kufanya lakini una jua jinsi ulivyo weza kuwa fanya wananchi wa wilaya ya Tunduru kuwa kitu kimoja, Jambo la Mhimu kwako ni kutokomeza siasa zinazo ingizwa katika Dini ukifanya hilo uchumi wa Tunduru uta kuwa kama ulivyo lenga Mwenyewe
Cap.John Komba wewe ni Mwamba wa Mashairi Juhudi zako Zimetufanya Mkoa wa Ruvuma Tuishi vizuri na Majirani Msumbiji,Malawi, na Hata Zimbabwe.Tunaomba uliyo fanya Wilaya ya Mbinga basi Hamishia wilaya Mpya ya Nyasa ukiweza Kuijenga Wilaya ya Nyasa kwa Ujasili ulio nao mwaka 2015 ni wako
Mheshimiwa Gaudence Kayombo wewe una jijua kuwa Fani yako ni Uchumi jitahidi achana na Hasira endeleza yale uliyo panga kwa wananchi wako hivi sasa Mbinga ina Umeme ,Barabara za Lami,Pia hata uchumi una zidi kupanda, Watu wasio na Furaha na Maendeleo ndio wanao kukatisha Tamaa, Chukua Moyo wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa na Uvumilivu.Hasira za Mkizi furaha ya Mvuvi.Makaa ya Ngaka yana ngoja Busara zako
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment