KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, May 16, 2013

WAANDISHI WA HABARI MKOA WA RUVUMA WANA KOSA GANI KWA SEREKARI YA JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA

 Hii ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambayo ina simamia haki zote za wana Ruvuma wapatao 1,400,000 wakiwemo Waandishi wa Habari wapatao 39 walioko Mkoa wa Ruvuma.
Jambo la kushangaza watu mbalimbali wamekuwa wakilaani wakiona Mwandishi ameuwawa, Laana huwa kubwa kupita kiasi. Sasa Waandishi wa Mkoa wa Ruvuma wanakabiliwa na Changamoto ya kuvunjiwa Ofisi yao ambao ni Tegemeo lao. Jee hii Ofisi ya Serikali Mkoa wa Ruvuma itasaidia vipi Jengo hilo lisivunjwe?
 Ofisi hii ni ya Mkuu wa Wilaya ya Songea ambapo ni Makao Makuu ya Mkoa wa Ruvuma kwa ukaribu huo ni juu ya Ofisi hii pia kuangalia Haki za Watu mbalimbali wakiwemo Waandishi wa Habari ambao wana Changamoto ya kuvunjiwa Ofisi yao. Jee nayo Ofisi ya Wilaya inachukua Hatua gani kuwasaidia Waandishi? au inangoja kulaani?
 Hizi ni Barabara ambazo zinatakiwa ziweze kufuata Taratibu, Kanuni na Sheria lakini kuna Majengo ambayo yamezuia kuzifanya Barabara hizo zichanue kwa kuwa zinawasaidia Wananchi katika kupata huduma mbalimbali katika Majengo yaliyoziba kupita kwa barabara hizo Serikali haina kelele na wala Wananchi hawasemi chochote.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Thabit Mwambungu ndiye mhimili mkuu wa kuwalinda watu mbalimbali, Jee katika Changamoto hiyo inayowakabili Waandishi wa Habari unawasaidia vipi badala ya kungoja mpasuko kati ya Waandishi na Watendaji.
 Jengo linaloonekana mbele yako ndiyo Ofisi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma ambalo linategemewa kuvunjwa hivi karibuni na Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Jee ni uhasama gani uliopo kati ya Waandishi wa Habari na Halmashauri ya Manispaa ya Songea? Majengo yaliyopo ambayo yamejengwa kinyume cha taratibu mbona hayaguswi?
 Hili ni Tangazo linalowataka Waandishi wa Habari wahamishe vitu vitu vyao ndani ya siku 14 vinginevyo mali zitaharibiwa pamoja na Jengo kuvunjwa. Jee hii ni halali? kuwanyanyasa waandishi wa Habari wakati Wananchi walioko pembezoni mwa Tanzania wanategemea kupata habari kutoka kwa Waandishi.
 ?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????

No comments:

Post a Comment